Tuesday, August 14, 2007

CHAHALI, NAHITIMISHA MJADALA!

Napenda kuumaliza mjadala huu kwa kusema yafuatayo, kwako binafsi, kufuatia email uliyonitumia, na kwa wachangiaji wote, hasa rafiki yangu ‘Kichuguu, mfuatiliaji’ na wengine, ingwawa wengine nililazimika kuwa ‘delete’ kwa kuandika matusi badala ya hoja:

Nimefuatilia kwa makini sana hoja zilizojitokeza baada ya mimi, kwa niaba ya uongozi, kutoa taarifa maalum na waandishi wetu kuandika stori kuhusu wewe binafsi katika gazeti la Ijumaa na makala ya mhariri wa gazeti la Risasi, ya Jumamosi iliyopita.

Aidha, baada ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa wahariri kuhusu hoja zao katika stori hiyo, naweza kumaliza mjadala huu kwa kusema yafuatayo:

Nia ya Chahali pamoja na Mhariri wa makala yake haikuwa nzuri tangu mwanzo, (you had malicious intentions from the beginning). Wakati unaikosoa habari ile ulikuwa na ‘element’ ya dharau, kuchafuliana na kushushiana hadhi mbele ya wasomaji, hiyo imeonekana kwanza kabisa kwenye headline ya makala yako, ‘Magazeti ya udaku yanaandika habari feki’ implying kwamba ni magazeti yote (kukurekebisha tu, siku hizi yanaitwa magazeti pendwa!).

Asilimia 95 ya makala yako ilikuwa inaongelea masuala mengine kabisa ya hapa nchini na huko ‘ughaibuni’ na asilimia 5 tu ndiyo ulizungumzia gazeti letu la Risasi tena mwishoni mwa makala, kwa mhariri ambaye hakuwa na nia mbaya dhidi yetu, asingeandika headline yake kutoka katika asilimia 5 ya makala yako na kuacha asilimia 95 ambayo ndiyo iliyobeba makala yenyewe.

Katika hali yoyote, makala hiyo, kama uongozi, tuliiona ilikuwa na nia ya kulichafua jina la kampuni, kitu ambacho huwa hatukai kimya na wala hatujawahi kukaa kimya pale tunapoona mtu anataka kutushusha. Kauli yako tunainukuuu:

“Nyie ni watu wazima ambao mmeshatengeneza faida ya kutosha kwa kuandika udaku lukuki wa kweli, sasa tamaa ya nini hadi mfikie hatua ya kunyofoa mapicha kwenye mtandao na kuzusha habari? Shame on you”.

Chahali, inawezekana kabisa You had the target to shoot at, but you missed it! Inawezekana kabisa ulikuwa na hoja ya msingi katika stori hiyo lakini ulishindwa kuiwakilisha ipaswavyo na badala yake ukatia chuki na ubinafsi zaidi, para hiyo ndiyo imeleta haya yote yaliyokukuta, A’m sorry kuona nawe imekuathiri sana, kwani hata sisi kauli yako imetuathiri pengine kuliko hata wewe! (WHICH HAS AS A RESULT SEVERELY AFFECTED NOT ONLY MYSELF BUT ALSO MY SPONSOR-CUM-EMPLOYER, FAMILY, FRIENDS AND RELATIVES). Maneno hayo yaliyoko kwenye mabano ni salamu uliyotutumia iliyoonesha jinsi ulivyoumia!

Naamini kabisa kuwa ulikuwa hujui kama source ya picha za hao ‘warembo’ ni mtandao wa hi5 na wala sio ule wa http://www.wannawatch.com na mingine uliyoitaja na kwa kutolijua hilo hukupaswa kufikia hitimisho kuwa wahariri walichomoa picha za kwenye mtandao na kuandika habari ile kwa lengo la kuwadanganya wasomaji na kuashiria kwamba uongozi unatamaa sana ya fedha na huo ndio mchezo wake.

Kumbuka kwamba, Global Publishers imekuwa katika Media Industry kwa karibu miaka 10 sasa na katika kipindi hicho imeshabadili maisha ya Watanzania wengi sana kuwa bora na wengine wanasoma au wamemaliza kusoma kwa kulipiwa na kampuni hii, tunaheshimika vya kutosha na wanaotuchukia ni wale wasiopenda mabaya na uovu wao kuwekwa hadharani. (angalia picha za ukurasa unaofuata kulelewa tunachokisema kuhusu kubadili maisha ya watu)

Kampuni yetu haina tamaa ya fedha kama unavyodhani, mwezi uliopita tu kupitia gazeti la Risasi tulichezesha Bahati Nasibu iliyorudisha kwa wasomaji wetu kiasi kisichopungua milioni 10 za Kitanzania, likiwemo gari la shilingi milioni 6 alilopewa mmoja wa wasomaji wetu, kama tulikuwa ni watu wa tamaa na wabinafsi, tusingefanya hayo yote.

Namaliza kwa kusema: YOU HAD AN URGUMENT BUT YOU FAILED TO PRESENT IT IN A CIVILISED WAY, SO NEXT TIME IF YOU WANT TO TALK SOMETHING ABOUT US, PLEASE BE CAREFUL !

GOD BLES YOU!

Imetolewa na
Abdallah Mrisho
Meneja Mkuu
Global Publishers Ltd
Aug 14, 2007
3:30 pm EAT

7 comments:

Seba said...

Pongezi nyingi kwa kuisaidia jamii,lakini katika hili mmechemsha kwelikweli.Tuliofatilia mjadala huu tangu mwanzo tunaweza kuhitimisha kwamba ukweli umejulikana lakini nyie mliokosea mnaona aibu kukiri hadharani

Kyoma said...

Mzee Abdallah Mrisho na Mhariri wa Risasi, heshima zenu kwa mpigo!

Jamani, hoja hujibiwa kwa hoja. Hakuna mahala popote katika maelezo yako na maelezo ya uongozi wa gazeti la Risasi ambapo kumejengwa hoja inayo dhoofisha hoja kuu ya Chahali ya kuwa habari mliyoitoa kwenye gazeti lenu haikuwa saihi. Badala yake mmeanza kujenga hoja uchwara zisizo na mantiki za kumshambulia mjenga hoja badala ya kushambulia hoja yenyewe. Eti “makala hiyo, kama uongozi, tuliiona ilikuwa na nia ya kulichafua jina la kampuni”. Kampuni haichafuliwi jina bali hujichafulia yenyewe.

Kilichoonekana kuchafua jina la kampuni yenu sio mwandishi wa makala bali ni ukweli ndani ya ile makala. Alafu Mhariri anatuhubiria mambo ya “Elimu humsaidia mwanadamu kupanua uwezo wa kufanya maamuzi sahihi”. Sasa hiyo elimu mbona haikuusaidia uongozi wa gazeti la Risasi wakati wa kumjibu Chahali? Au Mhariri sio sehemu ya Uongozi? Si wanasema kuwa usibishane na mpumbafu kwani watu wanaweza wasione tofauti? Mbona mmetumia njia ile ile ya kebehi na dharau kumshushua Chahali? What kind of “elimu” do you ascribe to? Au ni yale ya kuazima busara za Kasisi za kututaka tuzingatie mahubiri yake lakini tusiangalie matendo yake? (Yeah right!)

Mhariri wa Risasi anamtuhumu Chahali kwa “kujenga hoja kwa misingi ya dharau na kebehi huku ukionesha kutokuwa tayari kufungua milango ya taarifa kuingia kwenye ubongo wake”. Hakuna dharau na kebehi kubwa kama kuwalisha wasomaji habari za uongo au za kutunga. Hii inaweza kufanyika kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Lakini ikigundulika kwa njia zozote zile kuwa habari iliyochapishwa haikuwa ya ukweli, basi kosa inabidi lisaihishwe haraka sana na wasomaji waombwe radhi bila kujali njia gani ilitumika kugundua huo ukweli. Je mhariri amefungua milango ya taarifa kuingia kwenye ubongo wake? Au bado hajagundua kuwa habari iliyochapishwa ilikuwa ni ya uongo?

Umeandika kwamba “tunaheshimika vya kutosha na wanaotuchukia ni wale wasiopenda mabaya na uovu wao kuwekwa hadharani.” Hii ni dhana ya Mkuki kwa Nguruwe lakini kwa binadamu ni mchungu. Kwa maneno yako, uongozi wa Gazeti la Risasi unaona ni jambo la heshima kuanika maovu ya wengine hadharani, lakini Chahali alipoanika nguo zenu chafu juani ili mzifue, badala yake mnamshambulia. Yaani ninyi mnaona raha kukodolea macho vikalio vya wengine lakini mnavionea nongwa vikalio vya kila mmoja wenu ndani ya uongozi wa gazeti la Risasi. Ama kweli Nyani haoni kundule. Heshima gani unayoiongelea inayopatikana kwa kuondoa boriti ndani ya macho ya wengine wakati mnaleta hoja zisizo na vichwa wala miguu zenye tafsiri ya kuficha vibanzi ndani ya macho ya uongozi wa gazeti la Risasi?

Umeandika kwamba ulilazimika kuwa “delete” wachangiaji wengine kwa kuandika matusi badala ya hoja. Pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia, sioni haja ya kupiga teke mila na desturi zetu. Wanasema ukienda Roma fanya kama waroma wafanyavyo, lakini tusisahau ukweli kuwa Waroma wakija kwetu wanatakiwa kufanya kama sisi tufanyavyo. Kama tumeamua kuuzika utamadunu wetu na kuanza kutukuza ule wa Roma, sijuhi tunaiandaa jamii ya aina gani? Kumbuka hatuwezi kuwa Waroma hata siku moja. Mtanzania atakuwa Mtanzania tu.

Matusi yamekuwepo toka enzi za kale, lakini tulijitahidi kujenga jamii iliyostaharabika isiyo na matusi. Mfano Marekani Baba anamwambia mtoto wake “bring your ass here”, lakini Tanzania tuliyoridhi kutoka kwa wazazi wetu husingesikia maneno kama hayo kutoka kwa mzazi wako. Malezi bora yalianzia kwenye familia mpaka ngazi ya taifa. Watu waliadhibiwa kwa kuwatukana wenzao. Mantiki hii ilieleweka kwenye vyombo vya habari vyote. Tulikuwa na magazeti ya burudani kama Sani, lakini matusi na uchafuzi wa lugha havikuvumiliwa. Wahariri walikuwa wabunifu, hivyo magazeti yao yalinunuliwa kwa wingi bila wao kushiriki katika matendo ya kubomoa malezi mema tuliyojijengea.

Siku hizi mambo yote ambayo yalikuwa yanafanyika jando, yamewekwa hadharani. Mzazi hawezi kukaa sebureni na watoto wake wakiangalia miziki wa kizazi kipya kwenye TV au kusikia maneno redioni. Picha zinazowekwa kwenye baadhi ya magazeti ya kisasa huwezi kuziangalia mbele ya mzazi wako. Zamani hata kutamka neno “matiti” mbele ya kadamnasi ilikuwa haikubaliki. Siku hizi picha zinatolewa kwenye magazeti matiti yakiwa nje nje. Zamani ilikuwa ni matusi kutamka neno lolote la sehemu za siri za mwili wa binadamu. Siku hizi picha za watu wakiwa uchi wa mnyama zinatolewa kwenye magazeti huku sehemu za siri zimewekewa vizibio, lakini ujumbe ni ule ule kwamba huyu mtu yuko uchi.

Frankly speaking, we are promoting and cerebrating ignorance. Huu sio utamaduni wetu bali ni mambo ya kuiga kutoka nje. Nimewahi kuwandika mahala kuwa nachukia unafiki wa kumpinga shetani kwa kutumia mkono wa kushoto na kumhalalisha kutumia mkono wa kulia. Hivi kuna matusi yanayozidi baadhi ya picha zinazochapishwa na gazeti la Risasi? Ni bora kukubali matokeo ya matendo yetu. Kuna mantiki gani ya kuchapisha picha za matusi wakati huo huo tuna “delete” maandishi ya matusi. We are trying to groom hiki “kizazi kipya” kinachofanana na magazeti yetu, na kinaongea lugha inayofanana na picha tunazo ziweka magazetini. Maandiko yao hayawezi kuwa matusi kwetu kwasababu ndio kioo cha matendo yetu kwao. We have to swallow these pills as bitter as they are.

Unasema kwamba magazeti ya namna hii yanapendwa na watu. Lakini hii sio hoja ya maana ya kumjibu Chahali. Tafsiri ya hoja ya Chahali iko kwenye ubora wa haya magazeti na sio kama yanapendwa na watu au hapana. Kama suala la kupendwa ni hoja, mbona pamoja na sheria kali zilizopo kote duniani, lakini bado Bangi inapendwa na watu wengi. Kuna tofauti kati ya kupendwa na ubora wa kitu. Hata Madawa ya kulevya yana wateja wengi tu. Nani kasema Bangi au Madawa ya kulevya ni bora?

Kibaya zaidi, faida ipatikanayo kutoka katika biashara ya Bangi na Madawa ya kulevya inapeleka watu shule, inasaidia vituo vya watoto yatima, inasaidia matibabu ya wagonjwa, inachangia hata pato la taifa-GDP, n.k. Hata wafanya biashara wa haya majinamizi makubwa, wakishapata faida, wanaanzisha biashara mpya na kuajiri vijana wengi tu. Matendo yote yote haya yanafanyika nyuma ya pazia la usamalia wema na kujali utu wa watu katika jamii zetu. Lakini matendo haya yote hayafuti maana nzima ya unyama utokanao na madhara ya Bangi na Madawa ya kulevya kwa binadamu.

To you Chahali, Heshima yako!

Kumbuka, not all that glitters is true Gold. A clarion call inherent of close-mindedness is a monster you have encountered in decent search for truth. For sure that is not the way you should have gone, but who knows, truth seekers have cursed tyrants.

Thanks
Kyoma
e-mail: kyetema@yahoo.com

Anonymous said...

..Huyu jamaa bado anaweka mishangao tu kwa umma!anamchimba mkwala Chahali eti anapangia watu jinsi ya kuandika habari kuhusu wao!sasa nakuuliza swali moja tu WAKATI MNAANDIKA HABARI ZENU ZA UDAKU TENA ZINAZOHUSU MTU BINAFSI HAO WATU WAMESHAWAPANGIA NYIE!??si huwa mnaandika vile mnavyotaka nyie ili umma uone matendo yao maovu!sasa leo na nyie mmewekwa hadharani basi ndo mnakuja juu!hahahah!!KWELI NYANI HAONI KUNDULE
Hebu ndugu zangu nyie acheni kuendelea na hii hoja manake hapa wala hamtaweza kujitakasa hata kidogo!zaidi ya hapo mtaongea pumba tu na kuzidi kupotea!
Big up kwa wadau wote hasa Mr Kyoma kwa kuchangia hoja kwa kujibu hoja zao!kweli jamaa wanazidi kuumbuka tu kwa kuja na hoja hewa!ambapo mengi wanayoongelea yanawarudia wenyewe!tunazidi kupata picha kuwa haya makampuni mengine yanaongozwa na watu ambapo upeo wao wa akili ni mfupi bali wanataka kujiona wao zaidi!ila mwisho wa ni kuumbuka tu!mnasahau kuwa hapa wapo watu wengi na maarifa yao ila wapo kimya tu ila wale ambao wanachangia basi ndo wanatoa kamasi kweli kweli kwa hoja zenu zisizo na msingi kwani matokeo yake zinawarudia wenyewe!hope na nyie mshajua kuwa umma wa wana mtandao hapa ni watu wa namna gani!TUNAIPENDA SANA NCHI YETU NA UKWELI DAIMA UTASIMAMA MBELE KWA HOJA ZA MSINGI NA JAMBO LOLOTE LA UKWELI AMBALO NI KINYUME NA MAADILI TUTAKUWA TAYARI KULIKEMEA KWA NGUVU ZOTE!

erwin said...

huonyeshi kwamba unakubali kosa,ni mtitiriko wa habari tusizozihitaji

Anonymous said...

habari zako za nutrition nazipenda,maana inaelekea unajua unachooongea,hizi nyingine mh sidhani.piga ua hata ukidelete message sent

Anonymous said...

Bwana Mrisho,
Inasikitisha pale unapoonekana kufagilia uongo uwe ukweli. Nimesoma maelezo yako, unadai kwamba Bwana Chahali aliandika news kwa mlengo wa kutaka kuwadondosha/kuwachafulia jina la kampuni yenu kwa kusema kwamba, "MAGAZETI YA UDAKU YANAANDIKA HABARI FEKI". Mhariri wako amekiri kwamba ni kweli mtoa habari aliwadanganya na hilo pekee linaonyesha wazi kwamba anakiri kuwa habari ya hizo picha ilikuwa ni "FEKI"! Wewe ulitaka Chahali atumie kichwa kipi cha habari? Nyie ndiyo mnaotaka watu waseme kijiko kikubwa badala ya kusema ni koleo/beleshi na kupoteza maana halisi. Ukweli utabaki pale pale kwamba news ile ilikuwa fake na haikuwa na ukweli wowote. Hakuna dharau wala kuwachafulia jina la kampuni. Kama uliona kwamba Chahali kachafua jina la kampuni, mahakama zipo kwanini hamkuenda kushitaki? Au kwanini hamkwenda kwenye baraza la habari ili kulishitaki gazeti la KULIKONI na Mhariri wake + mchapishaji wa gazeti? Matokeo yake mkaishia kusema kwamba Chahali atamponza Mengi, kwa lipi? Kwa kusema uongo? Gazeti la KULIKONI na THISDAY yako makini sana na ukiona yamechapisha habari kama hiyo jua kwamba Mhariri ameifanyia kazi ya kutosha na ameridhika kwamba ni habari ya kweli. Niambie ni gazeti gani jingine ambalo limekuwa likiandika skendo za viongozi walio serikalini wa awamu hii au awamu iliyopita? Na wote waliotishia kwenda mahakamani wameishia kutoa vitisho peke yake na kubaki kimya.

Kitu kilichochokuwa muhimu kwako wewe na wahariri wa magazeti yenu ya udaku ni kuongeza juhudi ya kuthibitisha news kama ni za kweli au ni za uongo na siyo kukimbilia kum-attack mtu anayewasaidia kwa kuwapa ukweli. Iko siku mtakuja kuandika news ambazo zitawapeleka mahakamani. Suppose Lundenga na wenzake wangesema wawapeleke mahakamani kwa kusema wanaogombea u-miss kwa ngazi ya vitongozi ni malaya unadhani mngeweza kukwepa hizo lawama? Maana ukiulizwa uwataje majina au kuonyesha picha zao kila mtu atakushangaa pindi ukienda kutoa ushahidi wa picha za kwenye mtandao. Japokuwa mnadai kwamba mlikuwa na hard copies za picha hizo na namba za simu za wahusika (bado nina doubt hukuhu hili). Mshukuruni sana Chahali kwamba amesaidia ili kuwakosoa na kuwarekebisha ili magazeti yenu yaandike habari za kweli.

Kutoa msaada kwa watu hiyo siyo hoja ya kujitetea kwa kutupatia stori za uongo. Ina maana jambazi au malaya akipata hela za hiyo kazi haramu akienda kusaidia watu inafuta dhambi yake ya ujambazi au umalaya wake? Bado atabaki kuwa jambazi na bado atabaki kuwa malaya hata kama anasaidia watu wangapi. Sawa na alivyosema Kyoma kwamba fedha za madawa ya kulevya ndizo zinaingiza watu madarakani na kusaidia watu, lakini madhara yake kwa jamii ni makubwa sana. Kwa hiyo kutupatia orodha na picha za watu ambao wamesaidiwa na kampuni yako siyo utetezi wa uchafu na udaku/u-fake wa news za magazeti ya kampuni yako.

Ustaarab ni kuomba samahani na kukubali kwamba kampuni yako itajitahidi kuboresha na kufuatilia ukweli wa stori kabla ya kui-publish kwenye gazeti. Hiyo ndiyo dhana ya kutoa boriti kwenye jicho lako na ndipo utaweza kuona kibanzi kwenye jicho la mwenzako. Vinginevyo kuanza kumshambulia Chahali na Mhariri wa Gazeti la KULIKONI hakuna maana yoyote maana mpaka mwisho wa LIGI ya ushindani wenu tumegundua kwamba ile stori ilikuwa fake kweli, na tumejua nani kasema ukweli na nani kasema uongo kati ya magazeti yako na Chahali. Wenye macho na akili yetu tumeona na majibu ya mhariri wako na maelezo yako wewe mwenyewe yameonyesha wazi kwamba hamkuwa na hoja kwenye huu mjadala wote. Kwanini watoa maoni wote waegemee upande wa Chahali? Hilo pekee linakuonyesha kwamba something is wrong with your company.

Unaposema Chahali siku nyingine akiwa na hoja atafute namna nzuri ya kuiwasilisha, ni namna ipi? Ina maana kusema stori ile ilikuwa FAKE ni dhambi? Au ulitaka atumie lugha ipi? Akupake mafuta kwa mgongo wa chupa ili uendelee kuwadanganya watu zaidi na zaidi? Kubalini kwamba mlichemsha na hakukuwa na njia nyingine yoyote ya kuwasilisha hoja zaidi ya njia aliyotumia Bwana Chahali kwa kusema ukweli!

mdebwedo said...

tafadhalini shigongo na wenzako AHCENI KUKOPI VITABU VILIVYOTUNGWA ZAMANI NA KUTAFSIRI KISWAHILI UKIWA UMEBADILI MANENO MACHACHE. KUNA MTU WA COPYRIGHTS NIMEMTUMIA KWA DHL KUVITATHMINI PAMOJA NA VILE AMBAVYO NINAHISI UMECOPY FROM !! KAMA NI UBUNIFU WAKO MWENYEWE SAWA, KAMA SI WAKO NAOMBA USIENDELEE, CHANGAMSHA AKILI UTUNGE HADITH ZAKO MWENYEWE, NAOMBA UYAWEKE HEWANI MAWAZO YANGU KWANI NAAMINI ILE KAZI NI YAKO ORIGINAL NA ULIWEKA MPAKA COPYRIGHTS SI NDIO MZEE? NIMEMTUMIA VITABU NA BAADHI YA HADITHI AMBAZO NINA MASHAKA NAZO ASANTE NA KAZI NJEMA YA KUTUDAKUA MKUU.