Saturday, November 21, 2009

CodeRED in Tanzania Tonight!

East Africa No.1 Dj's are here, come to Hotel Kempinski Tonight to experience the difference when upacking at Zanzibar Room! Entrance is just 20,000/=

Friday, November 20, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

IJUMAA SEXIEST BACHELOR top 04
Kupitia mpambano huu wa kumtafuta staa wa kiume mwenye mvuto wa kimahaba, Ijumaa Sexiest Bachelor wiki iliyopita tuliwataarifu kuwa leo tutashuka na Top 3, lakini kutokana na washiriki wawili kufungana kwa kupata idadi sawa ya kura huku Jerry Tegete akiambulia kura chache zaidi, imebidi wanne waingie kwenye Top 4 ambapo baadaye itatafutwa tatu bora kwa ajili ya kumpata mshindi mmoja.

Washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye Top 4 ni Steven Kanumba, Hemed, Yusuf Mlela na Marlaw. Ili kumpigia kura mmoja ambaye unadhani anastahili kuibuka na ushindi andika namba yake kisha tuma kwenda namba 15551. Kumbuka kwamba kura yako ndiyo kila kitu katika shindano hili ambalo limedhaminiwa na maduka ya Zizzou Fashion.
******

KANUMBA
Mimi kama bingwa mtetezi kwanza nawapongeza waandaaji wa shindano hili ambao wamekuwa wakijitahidi kubuni vitu mbalimbali ambavyo vimekuwa vikitunufaisha sisi wasanii na zikiwemo zawadi kwa mshindi kama niliyopata mimi.

Pili nawashukuru sana wote wanaoendelea kunipigia kura mpaka kufikia hatua hii, naamini wataniwezesha kuchukua ushindi kwa mara nyingine tena.
*****

YUSUF MLELA
Shindano ni zuri, binafsi nimevutiwa nalo sana kwakuwa linatupa sapoti ya kutosha na kutufanya tuendelee kufahamika na watu wengi zaidi. Lakini shukrani za pekee ziwaendee mashabiki wote wanaoendelea kuwepo kwenye mpambano huu. Naamini nitaibuka na ushindi mkubwa kwakuwa sijaona mapungufu yoyote kwenye shindano hili.
*******

MARLWA
Nimefurahi sana kuingia kwenye hatua hii, nawashukuru mashabiki wangu walionipigia kura bila kuwasahau waandaaji wa shindano hili ambao wanatufanya sisi wasanii tuendelee kuwa juu zaidi.
Mpaka nimeingia kwenye hatua hii ni kipimo tosha kuwa mashabiki wangu wananipa sapoti ya ukweli, hiyo ni dalili ya kuibuka na ushindi.
****

HEMED
Wote waliofikia hatua hii wana vigezo ndiyo sababu iliyowafanya mashabiki wawapigie kura na kuwafikisha hapa. Nawashukuru sana wadau, wadhamini na waandaaji wa mpambano huu, bila kuwasahau mashabiki wangu nawaomba wazidi kunipa sapoti ili niibuke na ushindi, mwisho wa siku iwe ni jambo la kujivunia. Ni hayo tu.
***************************************Mlinzi wa Jay -Z amfanyia umafia paparazi
Mlinzi mmoja wa mwana Hip Hop Jay- Z au Jigga ambaye jina lake halikudondoshwa mtandaoni mwanzoni mwa wiki hii alimfanyia ‘umafia’ paparazzi aliyekuwa akitaka kumpiga picha msanii huyo kwa kumsukuma na kumpiga chini kitendo kilichomsababishia maumivu ya nguvu mgongoni mwake.

Ishu hiyo ilitokea pande za Hollywood majira ya mchana pale Jigga alipokuwa anasepa kutoka katika baa moja maarufu, ‘Capitol City Sports iliyopo kunako jiji hilo ambayo hupenda kutembelewa na mastaa wengi.

Baada ya mchizi kutoka nje ya baa hiyo, paparazzi huyo aliyefahamika kwa jila la Rick anayepiga mzigo kunako kampuni ya ‘X17 photo Agency’ alitamani kupata picha kadhaa za Jay-Z lakini wakati akijiandaa kufanya hivyo ghafla alivamiwa na baunsa wa staa huyo ambaye alimsukuma na kumdondosha chini (kama anavyoonekana katika picha juu).


***************************************

Busta Kushuka Bongo leo, Fiesta kesho
Ile kitu iliyopewa jina la ‘One Love’ a.k.a Fiesta 2009 sasa imewadia, macho na masikio ya mashabiki wengi yanatarajiwa kuelekezwa kwa mwana Hip Hop Busta Rhymes kutoka Marekani ambaye atadondoka Bongo leo majira ya saa tisa mchana kwa ajili ya shughuli hiyo kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wadau wa burudani.

Akipiga stori na ShowBiz mmoja wa waratibu wa One Love, Godfrey Kusaga alisema kwamba, Busta atadondoka na timu ya watu kadhaa ambao watampa sapoti ya kutosha katika kila atakachokifanya kwenye tamasha hilo na kwamba, kila kitu kinakwenda sawa wakiwemo wasanii kibao wa muziki wa Bongo Flava ambao walikuwa kambini wakijifua kwa ajili ya tukio hilo.
***************************************

Jittaman aibuka!
Kutoka pande za Rock City mchizi aliyenusurika kunako ajali mbaya ya pikipiki iliyotokea huko miezi kadhaa, Liso Katama Ibrahimu a.k.a Jittaman au Nzagamba katikati ya wiki hii aliibukia ofisini kwetu, Sinza Bamaga, Dar es Salaam na kupiga stori mbili tatu na ShowBiz.

Mchizi alisema kwamba, kwanza kabisa amekuja kuwatoa wasiwasi mashabiki wake wengi kufuatia uvumi ulionea kwamba yeye alikufa katika ajali hiyo, kitu ambacho siyo kweli na ishu ni nyingine ni kwamba, amedondoka Dar kwa ajili ya kuendeleza harakati zake katika game ya muziki wa kizazi kipya.

“Kinachofuata hivi sasa ni kazi kwa kwenda mbele, kila ngoma nitakayoachia naamini itakuwa juu kwakuwa nimerudi na idea mpya kibao, ukizingatia kwamba kupitia ajali hiyo nimejifunza mambo mengi. Namshukuru Mungu nimepona kwani hakuna aliyetegea mimi kuwa hivi leo,” alisema Nzagamba.
***************************************


Septemba 11 Yafanya kweli mtaani
Sisi kama ShowBiz tumewahi kushuhudia muvi kibao za Kibongo nzuri lakini kwa upande wa Septemba 11 ambayo imeshuka kitaani hivi karibuni inaweza ikawa zaidi kutokana na kazi iliyogongwa na mastaa wengi waliopata nafasi ya kushiriki kunako mzigo huo.

Unajua nini kinachoendelea kuipa ushindi muvi hiyo? Ndani kuna vichwa ambavyo hujawahi kuviona kwenye filamu yoyote ya Kibongo, umeshawahi kumuona kocha mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo akiigiza kama bonge la daktari, au yule golikipa mzungu wa Yanga? Ndani ya muvi hiyo wanasoka hao wamecheza kama mastaa wa Hollywood, hebu icheki kisha utatuambia.

Bado hatujamaliza, ndani ya Septemba 11 kuna mastaa wengine wa soka kama Juma K. Juma na Mussa Hassan Mgosi. Ukija kwa upande mwingine utakutana na sura za watu maarufu kama Ben Kinyaiya, Jackline Wolper, Frola Mvungi na wengine kibao. Kwa kifupi ni muvi ambayo inasumbua ile mbaya mtaani.

compiled by mc george

Thursday, November 19, 2009

MASHOGA!
Kuna picha hizi za mashoga wa Afrika walipokutana Afrika Kusini tungependa tushee na wadau

Picha zaidi link hii: NIFAHAMISHE.COM

Wednesday, November 18, 2009

MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU TOBI aka JIBABA-(MILTON-KEYNES)- Wednesday, November 18, 2009 8:19 AM From:

Milton Keynes TZ Society invites you for a prayer to commemorate our beloved Brother,Family & Friend TOBY aka JIBABA ,Its 3yrs Since His tragic Death, Ceremony will be held on Sat 21st Nov@ Jesus Celeb Centre,Lloyds Court,Central Milton Keynes,MK9 3AT(Formerly Known as Flames) from 2pm-6pm...

For more info please Contact 07899 784806/07897 362757....

Tuesday, November 17, 2009

Madhara ya unene kiafya


You are what you eat

UNENE umekuwa ni tatizo kubwa na sawa na janga la dunia. Tatizo hili limekuwa adui mkubwa wa binadamu kwa sababu limesababisha matatizo mengi ya kiafya na limeshapoteza maisha ya watu wengi hadi sasa. Kwa lugha nyepesi, unene wenye madhara kiafya ni ule wa kupita kiasi (tipwa tipwa) ambao hutokana na kuzidi kwa mafuta mwilini na mara chache husababishwa na vinasaba vya kurithi (genes).

Kitaalamu, kuna maneno mawaili ya lugha ya kiingereza yanayoshabihiana katika kuelezea unene, Over Weight na Obese.Inaelezwa kuwa mtu akizidi uzito wake wa kawaida kwa asilimia kati ya 10 hadi 19 anahesabika ni overweight. Aliyezidi kwa asilimia 20 na kuendelea huyo anakuwa ni obese na kama inavyoeleweka, uzito wa kaiwada wa mtu unategemea urefu, umri na jinsia yake.

Hivyo basi, unene wa kupindukia huwa ni matokeo ya kujikusanya kwa wingi kwa mafuta mwilini. Nishati inayoingia ikiwa kubwa kuliko ile inayotoka, matokeo yake huwa ni kurundikana kwa mafuta kwenye mwili na unene huwa ni machakato wa tataritibu ambao hautokei kwa wiki moja ama mbili 2. Watu wenye tabia ya kula sana bila kufanyakazi wala mazoezi ndiyo wanaopatwa na tatizo hili. Kanuni ya kudhibiti unene iko wazi.

Ukitaka kupunguza unene, kula kidogo, fanyakazi sana au mazoezi na ukitaka kunenepa, kula sana, usifanye kazi wala mazoezi na ukitaka kubaki hapo ulipo, kula kulingana na kazi unazozifanya au mazoezi unayoyafanya. Unene ni mbaya, huharibu afya ya mtu, kimwili na kiakili pia. Vile vile huwa ni adha unapojumuika na watu wengine ambao mara nyingi huwadhihaki watu wanene. Lakini mbaya zaidi, unene una karibisha magonjwa mengi hatari, yakiwemo ya moyo, kisukari, kiharusi, presha, n.k.

DONDOO MUHIMU KUJIEPUSHA NA UNENE
Weka utaratibu wa kula chakula kisichokuwa na mafuta na chenye mafuta kipunguzwe au kiondolewe kabisa katika orodha yako ya vyakula. Acha kula na kushiba kupita kiasi. Hakikisha siku zote unakula kiasi, usile mpaka ukashindwa kuhema. Unapokuwa kwenye sherehe mbalimbali, pendelea kula vyakula vya asili, kama matunda, saladi ya mboga na jiepushe na tabia ya kula vyakula vyote vilivyopo mezani. Kula kiasi kulingana na shughuli unazozifanya.

Kama ni mtu wa kukaa ofisini, usile sawa na anayefanyakazi nyingi za kutembea kwa siku. Pia fanya mazoezi kila siku, hata ya kutembea tu.


siyo u miss tu, hata u modo anauweza...ni Miss Tanzania 2009 Nasreem Karim

picha adimu..mbunifu wa mavazi nambari one nchini Tanzania Mustapha Hassanali, akiwa na mwanamitindo nambari one duniani, Naomi Campbell wakati wa onesho lake la hisani jijini Dar es salaam wiki iliyopita....ili kuwa ni suprise flani hivi kwa wengi kumuona live Naomi Bongo...!

NELLY AFANYA KUFURU!

Yuko kimya kwa muda mrefu katika anga za muziki, lakini mambo yake bado supa kiasi cha kufanya kufuru ya kufa mtu katika birthday yake aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita. Huyu si mwingine bali ni Nelly! Katika pati hiyo kulikuwa na strippers ambao walikuwa wakimwagiwa dola mtindo mmoja hadi ndani ya chupi na wengine kuwekewa katikati ya makalio...mastaa kibao walikuwepo kama vile JD, Ocean 7, Aries Spears na wengine.... ilikuwa ni kula bata kwa kwenda mbele!!!

NGWEA AINGIZA ALBAMU SOKONI!

Mkali wa free style Bongo na mwana hip hop machachari Albert Mangwea a.k.a Ngwair, kupitia Zizzou Entertaiment, leo anadondosha kitaani albamu yake ya Nge ikiwa full na hits zote zilizompa chati siku za hivi karibuni, kama vile Speed 120, Nipe Dili, Tupo Juu, n.k..hakikisha unapata nakala yako, hii si ya kukosa!!!!

Monday, November 16, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!
Eliza na Remtulla
Eliza Na ishuz za 5star party
Product ya Bongo iliyokuwa ndani ya mjengo wa Big Brother Revolution, Elizabeth Gupta ‘Queen’, wikiendi iliyiopita alifanya sherehe yenye level ya 5stars, ikiwajumuisha mastaa kibao nchini.

Party hiyo kiwango, ilichukua nafasi ndani ya Club Bilicanas kwenye Ukumbi wa Much Mo, usiku wa kuamkia Jumamosi, ikiwa ni maalum kwa kupongeza ushiriki wa Queen Eliza katika mjengo wa Big Brother na kumkaribisha nyumbani.

Mara tu alipodaka kinasa sauti, Eliza aliwashukuru Wabongo kwa kumkubali na kumpa sapoti ya kutosha kwa kipindi chote alichokaa mjengoni kabla ya kutolewa kwa zengwe. Aidha, Queen Eliza alionesha ufundi wa kucheza muziki, na kuuchangamsha ukumbi ambao sehemu kubwa ilikubali kwamba mtoto anaweza kumwaga swaga.

Jokate Mwegelo, Nasreen Karim, Mwanamitindo Ally Remtula, Ambwene Yesaye ‘AY’, Hamis Mandi ‘B12’ ni, baadhi ya mastaa waliokuwepo katika 5star party hiyo. *************************

compiled by mc george

WIKIENDA SHOWBIZ!

Omarion ajikunja na Rihanna!
Ebwana Dah! Ipo hewani tena na leo tunaye memba wa zamani wa Kundi la B2K, Omarion ambaye listi yake si ndefu lakini mtu mmoja ambaye ameweza kutokana naye ni mshangao.

Kwa mujibu wa tovuti ambayo ime-specialize katika eneo la staa gani katoka na nani, mrembo Debra ndiye anayetajwa nambari moja kutoka na ‘bwa mdogo’ huyo mwenye uwezo mkubwa wa kumiliki jukwaa. Mrembo wa pili anayetajwa ni Robyn Rihanna Fenty ambaye alitoka naye mwaka 2007, lakini haitajwi ni lini waliachana.

Kumbukumbu zinaonesha pia kuwa ni mwaka huo huo (2007) Rihanna alianza kutoka na dogo wa R&B na Pop mwenye kismati, Chris Brown a.k.a Ngumi Jiwe. Hii inamaana kuwa kwa mwaka mmoja, Rihanna alikuwa na Omarion, pia Chris Brown, ingawa haijulikani ni nani alianza au pengine alikuwa anawachanganya.

Omarion jina lake kamili ni Omari Ishmael Grandberry, ana umri wa miaka 25, alizaliwa Novemba 12, 1984, Inglewood, California, Marekani. Urefu wake ni futi 5.7, dini yake ni Mkristo.
****************************

Busta Rhymes live ndani ya Fiesta J’mosi
Mkali wa vocal za kigumu nchini Marekani, Busta Rhymes atakuwa live kwenye Viwanja vya Posta, Barabara ya Ali Hassan Miwinyi, Mikocheni, Dar es Salaam na kugonga shoo ya kiwango.

Awali, Busta alikuwa afanye makamuzi hayo wiki mbili zilizopita, lakini iliahirishwa baada ya Kampuni ya Clouds Entertainment Company Ltd inayoratibu shoo hiyo, kupatwa na msiba mzito. Clouds, ilifiwa na Mwenyekiti wake, marehemu Alex Mkama Kusaga, hivyo kusababisha Fiesta 2009 kuahirishwa kwa wiki mbili mbele.

Kwa mujibu wa waratibu, wasanii wote waliokuwa wamepangwa kutumbuiza siku hiyo, watakuwa ndani ya nyumba kwa ajili ya kufanya kile ambacho kinatakiwa na wengi. Hey, hii si ya kukosa, ni pale pale viwanja vya posta ambavyo vinatazamana na Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar.
*******************

R. Kelly ndani ya Kampala very soon!
Mfalme wa R&B asiyepingika, Robert Kelly ameridhia mwaliko wa kutua nchi jirani ya Uganda na kufanya shoo ya kiutu uzima.

Habari kutoka mtandaoni zinasema kuwa, R Kelly atatia maguu Kampala, Uganda na kufanya kweli katika viwanja vya Lugogo Cricket Oval , Januari mwakani. Imewekwa kweupe kwamba ujio wa R Kelly umefanikishwa kwa kiasi kikubwa kwa udhamini wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zain.
***********************

Kuwapa featuring mastaa ni kuharibu kazi
Hili haliwezi kupita, Abby Cool & MC George over the weekend ni lazima itoe salamu kuhusiana tabia ya baadhi ya mastaa kupenda kuharibu nyimbo za underground bila huruma. Yeah, hii imebainika kuwa wengi hufanya hivyo ili kuwabania watoto wasiamke.

Iko hivi, inaelezwa kuwa mastaa wengi wanaposhirikishwa na underground kwenye kazi fulani fulani, hufanya chini ya kiwango kwenye audio na hata video ili kuwabania vijana wasitambulike katika level za wajanja.

Yap, mastaa huboronga na kufanyakazi chini ya kiwango ili kuharibu kazi ya msanii, lengo ni kwamba ikitoka ionekane takataka, na kuwafanya madogo wasijulikane kwa sababu viwango vyao vinaonekana ni vidogo wakati kumbe wamesalitiwa. Mfano ni huu, singo inayokwenda kwa jina la Mariam ambayo ni mali ya wasanii mapacha, Johnson na Jackson a.k.a P. Square wa Bongo, imeharibiwa na mkali wa swaga, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’.

Safu hii, iliiangalia traki hiyo kideoni, pia ikaifutilia katika audio na kubaini kuwa Chid alifanyakazi chini ya kiwango. Vocal ni kama kalazimishwa, kwenye video ndiyo kabisa, swaga hazionekani kabisa.

Hiyo siyo fresh, haipendezi kuharibiana kazi, huko mbele wajanja wakishirikishwa huwa wanagonga standard kama vile ni kazi yake, lakini huku duh! Kuharibiana ndiyo kama kazi. Unaona traki ya mwenzako ikisimama itafanyabiashara, kwahiyo unamharibia.

Mbaya zaidi washikaji wanakuchangia ela ya mafuta ya kwenda na kurudi home, ni vema kama hutaki ukakataa kuliko kuharibu. Ni mastaa wengi wenye tabia hiyo. Safu hii inawaonya kuwa makini, vinginevyo one day itadondoka na ripoti kamili na kutaja madudu yao yote.
****************

Nay agonga kolabo na aliowadisi
Mkali wa Hip Hop anayevuma na traki inayokwenda kwa jina la Itafahamika, Nay wa Mitego ameamua kuunda remix ya ngoma yake hiyo huku akiwa amefanya kolabo na baadhi ya artists aliowadisi.

Itafahamika traki ambayo inasumbua kitaani, huku ikishika chati mbalimbali ikiwemo Bamiza ya Magic FM, ni ngoma ambayo inawagonga live baadhi ya wakali waliovuma kitambo lakini sasa hivi wamefunikwa.

Wakali kama Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’, Haroun Kahena ‘Inspector’, Zainabu Lipangile ‘Zay B’, Paul Matthysse ‘P. Funk’ ni baadhi ya waliochanwa kwenye verse za wimbo huo. Hata hivyo, Nay akipiga stori na safu hii, amenena kuwa amewapa featuring baadhi ya artists aliowadisi ili kuonesha kuwa hakuwagonga kwa bifu, isipokuwa ni mtazamo wa kisanii tu. Katika remix ya Itafahamika, Sister P, Squezeer, O-Ten, Mansulee, Dalaza, Kimbuka na wengine wameingiza vocal.

****************

Sunday, November 15, 2009

NANI NA NANI WAMEOANA WIKIENDI HII?


Kwa picha zaidi zaidi nenda: harusini.blogspot.com

MKONO NA RAIS JK!

Komando Lady jaydee a.k.a Manka, ndani ya 'handshake' ya nguvu na JK. Hii ilikuwa pale Mlimani City mara baada ya Jide ku perform katika shoo maalum ya Mo Foundation usiku wa kuamkia Jumapili, Nov 14, 2009. (Picha: Issa Michuzi)


Mama Mdogo Kuliko Wote duniani Kujifungua Mtoto wa Tatu


Mama mwenye umbile dogo kuliko wote duniani anatarajia kujifungua mtoto wa tatu ingawa madaktari wamemuonya kuwa maisha yake yako hatarini kutokana na tumbo lake kuwa kubwa sana kuliko mwili wake kiasi cha kumfanya ashindwe hata kutembea.

Stacey Herald, ambaye ana urefu wa sentimeta 71 anatarajia kujifungua mtoto wa tatu ingawa madaktari wameendelea kumuonya kuwa maisha yake yako hatarini kutokana na mimba aliyonayo kumuelemea.

Stacey alishayapuuza maoni ya madaktari mara mbili na kufanikiwa kujifungua watoto wawili ambao urefu wao wakati walipozaliwa ulikuwa ni zaidi ya nusu ya urefu wake.

Kwa habari kamili link ni hii:http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3536918&&Cat=7