Thursday, March 20, 2014

RAIS AANDAA HOTUBA AKIWA NDANI YA NDEGE

Rais Kikwete
Wakati wowote na mahali popote ni sehemu ya kazi.
Pichani ni anaonekana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ametulia ndani ya ndege akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma huku akiifanyia kazi hotuba yake ambayo ataitoa katika Kikao cha Bunge Maalum la Katiba, Ijumaa, Machi 21, 2014.

Rais Kikwete amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa Kanuni 7(1)g na Kanuni 75(1) la ya Kanuni za Bunge Maalum.

Picha, maelezo: Ikulu.

No comments: