Friday, September 19, 2014

KINANA AWAPONDA WAPINZANI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Maneromango leo wakati wa ziara yake wilayani Kisarawe, Pwani ya  kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wananchi wa Kata ya Maneromango wakisikiliza kwa makini hotuba ya Kinana katika mkutano huo. ambapo aliwananga wapinzani kuwa wapo kwa ajili ya kupanga maandamano, kutukana, kutoa manaeneo machafu klwa Serikali wakati CCM ipo kiutendaji zaidi katika masuala ya maendeleo ya wananchi.
 Kinana akihutubia baada yakuweka jiwe la msingi katika jengo la Zahanati ya Palaka Kata ya Malumbo wakati wa ziara yake wilayani Kisarawe leo.
W
 Kinana na Nape wakitoka kugfua ujenzzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe.
 Kinana akimjulia hali mama aliyekuwa anauguza mwanawe alipotembelea hospitali hiyo
 Kinana akiangalia wauguzi wakimtibia mtoto katika hospitali hiyo
 Kinana akisidia kujenga marumaru katika jengo jipya la wodi ya wazazi katika hospitali ya Kisarawe.
 Jengo la zamani la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Kisarawe.
 Kinana akifunua pazia alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo jipya la Zahanati ya Palaka, Kata ya Malumbo, Kisarawe
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kisarawe, Dk. Happiness Ndosi akimuelekeza Kinana kuhusu maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo.
 Wananchi wa Kijiji cha Palaka, wakimshangilia Kinana alipokuwa akihutubia baada ya kuweka jiwe la msingi katika zahanati Palaka.
 Wananchi wakiwa katika hafla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa zahanati hiyo pa Palaka
 Kinana akisaidia kufyatua matofali ya kujengea maabara katika Shule ya Sekondari ya Gongoni, katika Kata ya Gongoni, wialyani Kisarawe.Matofali hayo yanafyatuliwa na wanakikundi cha vijana chas wajasiriamali.
 Kinana akiondoa tofali alilolifyatua katika mradfi huo wa matofali wa vijana.
 Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Maneromango.
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Suleiman Jaffo akielezea kwa wananchi jinsi miradi mingi iliyokamilika ujenzi wake kwa kuata Ialani ya Uchaguzi ya CCM.

No comments: