Wednesday, December 31, 2014

TATHMINI YA PAPA KAIJAGE KUHUSU MATUKIO MAKUBWA YA MUZIKI WA DANSI KWA MWAKA 2014…




​​BENDI MPYA
•Vijana Ngwasuma ilizinduliwa ndani ya Letasi Lounge (zamani Business Park ,Victoria) Ijumaa ya tarehe 07-Mar-2014.
•Yamoto Band yazinduliwa rasmi tarehe 21-Sep-2014 ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala.
•Utalii Band yazinduliwa Ijumaa ya tarehe 26-Sep-2014 ndani ya ukumbi wa MRC (Mikocheni Resort Centre)
•Kundi la Chuchu Sound liliibuka tena na kupiga show kadhaa katika ukumbi wa Max Bar Ilala. Baadaye kwa sababu kadhaa bendi ikapotea.
•Pia kulikuwa na bendi ambazo sio mpya lakini ndani ya mwaka 2014 ziliundwa upya. Bendi hizi ni Victoria Sound  na Ruvu Stars.
•Bendi nyingine zilizoanzishwa ndani ya mwaka 2014 ni JJ Band, bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe. Pia kuna Ruby Band. Bendi hizi 2 zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2015.

UZINDUZI WA ALBUM MPYA
•Extra Bongo walizindua album ya “Mtenda Akitendewa” Jumamosi ya tarehe 22-Feb-2014 ndani ya Dar Live Mbagala.
•Talent Band (ya Hussein Jumbe) wazindua album ya “Kiapo Mara Tatu” Jumatano ya 30-Apr-2014 ndani ya Kisuma Night Pub, Temeke (zamani Sugar Ray)
•Christrian Bella azindua album ya “Nani Kama Mama” ndani ya Mzalendo Pub Jumamosi ya tarehe 30-Aug-2014
•Tarsis Masela katika viunga vya Ten Lounge (Business Park) Victoria azindua album ya “Acha Hizo” Ijumaa ya tarehe 21-Nov-2014
•Mashujaa Band yazindua album ya “Ushamba Mzigo” kwenye ziara za mikoani.

KILI MUSIC AWARD
•Kili Music Award 2014 ilifanyika Jumamosi ya tarehe 03-May-2014 katika ukumbi wa Mlimani City. Kulikuwa na jumla ya vipengele (categories) 8  vya muziki wa dansi. Washindi walikuwa kama ifuatavyo;
1. Mwimbaji Bora wa Kiume-Jose Mara (Mapacha Watatu)
2. Mwimbaji Bora wa Kike-Luiza Mbutu (Twanga Pepeta)
3. Rapa Bora-Fergusson (Mashujaa Band)
4. Wimbo Bora-Ushamba Mzigo (Mashujaa Band)
5. Bendi Bora-Mashujaa Band 6. Mtunzi Bora-Christian Bella (Malaika Music Band) 7. Producer Bora-Amorosso 8. Hall of Fame (Individual)-Hassan Rehani Bitchuka (Mlimani Park Orchestra)

WANAMUZIKI WALIOFARIKI
•Mpiga tumba wa Twanga Pepeta Soud Mohamed “MCD” afariki dunia Jumatatu ya tarehe 27-Jan-2014
•Mpiga bass wa Vijana Jazz, Maulid Mwangia afariki Jumatano tarehe 12-Mar-2014 na kuzikwa Alhamis tarehe 13-Mar-2014
•Mwanamuziki mkongwe Muhiddin Gurumo afariki dunia Jumapili ya tarehe 13-Apr-2014 na kuzikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe Jumanne ya tarehe 15-Apr-2014
•Mpiga gitaa wa Skylight Band, Chili Challa wa Skylight Band afariki dunia tarehe 17-Apr-2014.
•Amina Ngaluma “Japanese” afariki tarehe 15-May-2014  akiwa mji wa Phuket, Thailand.
•Mwanamuziki DIGITAL wa FM Academia afariki Ijumaa tarehe 18-Jul-2014.
•Ally Rashid “Mwana Zanzibar” ambaye mara ya mwisho alikuwa mpuliza sax wa Msondo Ngoma afariki tarehe 10-Oct-2014.
•Suzuki Sauti ya Malaika aliyepigia Extra Bongo katika album ya “Mjini Mipango” alifariki tarehe 15-Oct-2014
•Mwanamuziki Khamis Kayumba “Amigoulaus” afariki tarehe 09-Nov-2014.
•Mwanamuziki Shem Ibrahim Kalenga afariki dunia 15-Dec-2014 na kuzikwa tarehe 16-Dec-2014 katika makaburi ya Kisutu.
•Mnenguaji Aisha Madinda afariki dunia tarehe 17-Dec-2014 na kuzikwa tarehe 19-Dec-2014.

MATUKIO MENGINE MAKUBWA
•Mdahalo wa kwanza wa aina yake wa kujadili muziki wa dansi wafanyika katika ofisi za TBC Jumamosi ya tarehe 05-Apr-2014 chini ya u-moderator wa Dacota Khamis, kuhudhuriwa na wadau karibia 30 na kuonyeshwa live na TBC2 na baadaye kuonyeshwa recorded na TBC1 kwenye kipindi cha “Nyumbani ni Nyumbani”
•Bendi ya Msondo Ngoma yafanya sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 50. Maadhimisho yalianza Ijumaa ya tarehe 10-Oct-2014 ndani ya Leaders Club na kuhitimishwa TCC Chang’ombe Jumamosi ya tarehe 01-Nov-2014. Pia wanamuziki wa bendi walikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete, Alhamis ya tarehe 30-Oct-2014.
•Kwa mara ya kwanza tukio la “Usiku wa Msanii” lafanyika tarehe 25-Oct-2014 katika ukumbi wa Mlimani City. Marehemu Father Kanuti alipewa tuzo ya Humanitarian Award.
•Tarehe 09-Dec-2014, siku ya maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru na miaka 52 ya Jamhuri ya Tanganyika (Tanzania Bara), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla maalum iliyofanyika katika viwanja vya ikulu atoa nishani maalum kwa kundi zima la Atomic Jazz Band ya Tanga. Tuzo hiyo ni ya miaka 50 ya Muungano ya daraja la nne. Aliyepokea kwa niaba ya kundi ni mzee Stephen Hiza (Mgosingwa). Atomic Jazz Band imepewa nishani hiyo kutokana na kazi yao kubwa katika kulihamasisha taifa kuenzi muungano hususan kwa kupitia wimbo wao wa  “Tanzania Yetu”.
•Mpambano wa Msondo na Sikinde wafanyika mara mbili kwa kuandaliwa na Fred Ogot na kampuni yake ya Bob Entertainment. Mara ya kwanza ulifanyika siku ya sikukuu ya Eid Mosi (Eid al-Fitr) tarehe 25-Jul-2014 ndani ya TCC Chang’ombe. Mara ya pili umefanyika pia TCC Chang’ombe Christmas tarehe 25-Dec-2014. Kwenye mpambano wa mara ya pili, kwa mara ya kwanza tukio limesindikizwa na bendi ya Vijana Jazz Pambamoto “Saga Rumba”.
•MAONYESHO YA PAMOJA: Bendi 3 za FM Academia, Mapacha Watatu na Ruby Band zapiga pamoja Ijumaa ya tarehe 19-Dec-2014 ndani ya Mzalendo Pub. Yamoto Band mara kadhaa imefanya maonyesho ya pamoja kwa kupiga pamoja na Mapacha Watatu, Skylight Band na Twanga Pepeta. Pia Mlimani Park Orchestra wamepiga pamoja mara kadhaa na Machozi Band ya Lady Jaydee. Ruby Band walipiga pamoja na Twanga Pepeta Jumapili ya tarehe 28-Dec-2014 ndani ya Leaders Club
•Onyesho la Miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta lililokuwa lifanyike Jumamosi ya tarehe 20-Dec-2014 limeahirishwa hadi tarehe 31-Jan-2015 kutokana na kifo cha mnenguaji Aisha Madinda.
•Mechi ya mpira wa miguu kati ya kundi la BONGO DANSI na kundi la WATANASHATI WA MUJINI lafanyika katika viwanja vya Leaders Club Jumapili ya tarehe 23-Nov-2014. Matokeo yalikuwa suluhu 0-0. Kundi la BONGO DANSI mara kadhaa limefanya ziara ya kumtembelea Nguza Vicking na Papii Kocha ambao wapo gerezani Ukonga.
Tarehe 26-Dec-2014, umoja wa wanamuziki wa dansi katika viwanja vya Karimjee wafanya dua maalum ya kumuombea Rais Jakaya Kikwete ili hali yake ya kiafya iimarike.

No comments: