Thursday, January 8, 2015

WAOMBA KITUO MAALUMU CHA WATOTO WALEMAVU BUHANGIJA KUSAIDIWA ZAHANATI

DSC_0002
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kuelekea kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
Na mwandishi wetu, Shinyanga
MKUU wa wilaya ya Shinyanga AnneRose Nyamubi ameomba jamii ya watanzania kusaidia kupatikana kwa zahanati katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Buhangija ili kupunguza adha wanazopata watoto hao katika huduma za afya.
Kauli hiyo ameitoa katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika kituo hicho akiambatana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukiongozwa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Nyamubi amesema kwamba ingawa hospitali ya mkoa ina dirisha kwa ajili ya matibabu ya watoto hao,wakati mwingine inakuwa shida daktari maalumu anayehusika anapokuwa hayupo.
Aidha alisema kwa namna watoto hao walivyo wanahitaji huduma ya karibu ya kitiba ambayo inawezekana kama kituo hicho kingekuwa na zahanati yake.
DSC_0026
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi kwake, Bi. Chitralekha Massey ( wa pili kulia kwake) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (wa pili kushoto). Wengine katika picha ni Afisa Elimu Sayansikimu, Beatrice Mbonea (wa kwa kulia), Afisa Elimu Msingi wa manispaa ya Shinyanga, Bi. Pudensiana Magnus (katikati kulia), Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga, Festo Kang'ombe pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Shadrack Kengese.
Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2010 kwa ajili ya watoto walemavu wasiosikia na wasiiona kwa sasa kinapokea watoto wenye alibnizim ambao wanaokabiliwa na ujahiri dhidi ya maisha yao.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya kituo hicho ambacho serikali hutenga bajeti kwa ajili ya wanafunzi 50 wasiosikia na kuona, sasa kina watoto wenye albinism 247 ambao hawako katika bajeti na wanaishi kutokana na misaada ya watu mbalimbali.
Alisema kwamba watoto wenye albinism wanahitaji huduma za tiba za karibu zaidi kutokana na mazingira yanawazunguka na dirisha pekee katika hospitali ya mkoa halitoshi kwani wakati mwingine wanalazimika kukaa kwenye foleni kama wagonjwa wengine na hili halipendezi.
Aidha alisema kituo hicho cha Buhangija kwa sasa ni kidogo kuzingatia na uwingi wa wanaohitaji msaada na hivyo serikali inatafuta eneo jingine kwa ajili ya kujenga kituo.
DSC_0053
Mazungumzo yakiendelea ndani ya ofisi za Mkuu wa mkoa wa Shinyanga zinazokaimiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi.
Kufurika kwa watoto hao wenye ulemavu kunatokana na tishio la maisha yao hasa ukanda wa Ziwa ambapo familia zao zimewakimbiza kituoni hapo kwa ajili ya usalama wao.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema kwamba kituo hicho hakina bajeti na kutaka wasamaria wema kuendelea kuchangia ili watoto hao waendeshe maisha ya kawaida.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja Mataifa yaliyopo nchini, Alvaro Rodrigues amesema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kituo hicho na kuwataka wanaotunzwa hapo kutoacha kuishi kama watoto kwani ndio tunu waliyonayo kwa sasa.
Aidha alisema kwamba anauchukua wimbo waliouimba ambao unazungumzia machungu ya maisha yao na kwenda kuwaeleza watu wengine ili nao washiriki katika kubadilisha hali ya kuogofisha na kuleta usalama.
DSC_0068
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema alijumuika kwenye mazungumzo hayo. Pichani akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.
Alisema wao (UN) wamefika katika kituo hicho kuona watoto wanavyoishi na watafanya nini kuwasaidia.
Aliwataka Watanzania kuhakikisha wanakomesha machungu ya albino hao na kuishi nao kama watu wengine wa kawaida.
Aidha Mratibu huyo alipata nafasi ya kuzungumza na Binti wa miaka 19 Masabu masuka ambaye amejifungua mwaka jana kituoni hapo bila msaada wa wauguzi baada ya kulazimika kuondoka kwao akiwa mjamzito kukwepa mauaji dhidi ya albino yaliyofanyika Mei mwaka jana wilayani Bariadi.
Binti huyo alifika kituoni hapo na kaka zake watatu ambao wote ni maalbino kama yeye.
DSC_0075
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi katika picha ya pamoja na ugeni kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa Tanzania na Shirika la UNDER THE SAME SUN.
DSC_0120
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi akiwasalimia watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga kabla ya kumtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
DSC_0150
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza na watoto wenye ulemavu wakiwemo wa ngozi (hawapo pichani) wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho. Katikati ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi.
DSC_0167
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa zawadi ya maziwa kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
DSC_0174
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akishiriki kwenye zoezi la kugawa zawadi kwa watoto hao.
DSC_0186
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya Mratibu huyo, Bi. Chitralekha Massey wakiendelea na zoezi la kugawa zawadi kwa watoto hao.
DSC_0203
Mratibu Mkazi huyo Bw. Alvaro Rodriguez akiwasaidia watoto hao kufungua biskuti alizowapekea kama zawadi alipotembelea kwenye kituo hicho.
DSC_0213
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akieleza jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) alipokuwa akikagua mazingira ya kituo hicho na kuona ni jinsi atawasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili kituo hicho.
DSC_0235
Pichani ni jiko la kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wakiwemo wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
DSC_0248
Wapishi wakiendelea na shughuli zao kuwapikia watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.
DSC_0261
Mwalimu Mkuu wa shule ya watoto wenye maalum ya Buhangija Jumuishi, Peter Ajali akitoa maelezo ndani ya moja ya mabweni kituoni hapo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema.
DSC_0278
Mwalimu Mkuu wa shule ya watoto wenye maalum ya Buhangija Jumuishi, Peter Ajali akimwonyesha baadhi ya sehemu ambazo hazisakafiwa ndani ya mabweni kituoni hapo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
DSC_0308
Baadhi ya matandiko wanayotumia watoto hao wenye mahitaji maalum kulali kwenye sakafu ambayo haijasakafiwa na pia kutokana na uhaba wa mabweni inawalazimu kubanana na kulala bila uhuru.
DSC_0311
Bweni lililojengwa na Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred linalohudumia watoto 48 ambalo linahitaji kumaliziwa ili watoto hao nao waweze kulala mahali pazuri.
DSC_0233
Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodrigues akizungumza na binti wa miaka 19 ambaye ni mlemavu wa ngozi na kutosikia, Masalu Masuka ambaye anaishi katika kituo cha watoto walemavu cha Buhangija baada ya kukimbia kwao Bariadi kukwepa wauaji wa albino. Binti huyo alijifungua mtoto wake akiwa kituoni hapo bila msaada wa muuguzi. Kituo hicho kinahitaji msaada wa kujengewa zahanati. (Picha na Zainul wa Mo Blog)
DSC_0331
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza mpira ambao ni moja ya zawadi alizozitoa kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kukitembelea kituo hicho kinachokabiliwa na changamoto mbalimbali na kuwaahidi kuwasaidia huku akiwashirkisha na wadau wengine wa maendeleo. Kushoto mwenye kofia ni Khassan Khamis na kulia ni Emmanuel Deus.
DSC_0346
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiendelea kucheza mpira na kufurahi na watoto hao wenye ulemavu wa ngozi.
DSC_0386
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Ghoke Maliwa anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kukitembelea kituo hicho juzi mkoani humo.
DSC_0351
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma ujumbe unaosema "DREAM BIG" kwenye T-shirt ya mtoto Agnes Kabika mwenye ulemavu wa ngozi anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho.
DSC_0315
Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya Mratibu huyo, Bi. Chitralekha Massey akibadilishana mawazo na binti anayefanya shughuli za kujitolea Claire Grubbs kutoka nchini Marekani aliyepiga kambi kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
DSC_0428
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiagana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwenye kituo hicho.

No comments: