Saturday, July 11, 2015

NEC YA CCM YAKUTANA KYCHAGUA TATU BORA LEO

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wajumbe baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, leo katika Ukumbi wa jengo la White House mjini Dodoma. Kikao hicho ni cha kuchagua wagombea watatu kati ya watano waliopitishwa na Kikao Cha Kamati Kuu ya CCM kwa ajili ya kuwania kugombea Urais kwa tiketi ya CCM. Watatu watakaopatikana leo, watapelekwa kuigiwa kura katika Mkutano Mkuu wa CCM ili kupata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo mkuu. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utanguzi kumkaribisha Kikwte kufungua mkutano huo. Kushoto ni Dk. Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao hicho
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao hicho
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kushoto_ alipoingia ukumbini. Waliosimama mbele ni Wajumbe waalikwa wa kikao hicho kutoka Baraza la Ushauri la Wazee Marais wastaafu Ali Hassani Mwinyi na Benjamin William Mkapa na wengine ni Makamu Wenyeviti wastaafu Mzee John Malecela na Mzee Pius Msekwa
 Kikao hicho kikiendelea

No comments: