Saturday, August 1, 2015

Angalia Kipindi Chote Cha 'Nyumbani Na Diaspora' TBC1 Jana Ijumaa.

Nyumbani na Diaspora!
Ni kipindi kipya cha saa nzima chenye kuhusiana na Watanzania wa nyumbani na walio nje ya mipaka yetu. Ni kipindi daraja kitakachowaunganisha Watanzania katika kubaini fursa mbalimbali za kuinuka kimaendeleo, kwa mtu mmoja mmoja, jumuiya na hatimaye taifa. Ni kipindi kitakachoongozwa na mchambuzi na mmoja wa wanahabari nguli hapa nchini. Si mwingine ni Maggid Mjengwa. Jiunge nae kufuatilia mahojiano motomoto na watu wa kada tofauti kwenye masuala ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Ni kila siku ya Ijumaa saa 4 usiku na marudio Jumapili saa kumi jioni, TBC 1, ukweli na uhakika!

No comments: