Friday, December 4, 2015

ukumbushane: Magufuli Na Wafanyabiashara...


" Kama kuna mfanyabiashara humu aliyenichangia fedha kwenye kampeni zangu anyoshe mkono!'- John Magufuli, Jana Alhamisi.

Ndugu zangu,
Jana kupitia runinga tumemwona Rais John Magufuli aklizungumza na Wafanyabiashara. Ilikuwa ni hotuba muhimu kwa Rais wa nchi kuonyesha maono yake inapohusu mahusiano ya Serikali na Wafanyabiashara.
Kuna wakati, kwenye kipindi cha kampeni, niliandika yafuatayo kwenye Raia Mwema; "John Magufuli anayekuja, atakuwa na nafasi ya kipekee inayofanana na ya Mwalimu Nyerere kwa kuweka rekodi ya kuingia madarakani kwa kufanya kampeni ambazo hazikuhusisha sana matumizi makubwa ya fedha ambayo mara nyingi huambatana na michango ya wafanyabiashara wakubwa. Hivyo, John Magufuli hatakuwa na wadeni wake wa kuwalipa fadhila, isipokuwa, kuwahakikishia wafanyabiashara hao, uwepo wa mazingira mazuri ya kufanya biashara zao na walipe kodi ili zisaidie maendeleo ya wananchi wengine walio wengi. Kuna haja ya kutenganisha biashara na siasa, kuwa hata watendaji wakiwamo mawaziri, mbali ya Magufuli kuwasainisha mikataba, lakini umma ungetaka pia kwenye mikataba hiyo mawaziri na watendaji wakuu wawe tayari kutenganisha uongozi wa kisiasa/utendaji wa kiserikali na shughuli zao za kibiashara.
Na kwa kweli hili za kampeni za urais kuchangiwa na wafanyabiashara wakubwa lina mifano hai ya athari hata kwa wenzetu walioendelea kidemokrasia mfano wa Marekani.
Kwenye kampeni za kuwania Urais wa Marekani mwaka 1996, ambapo, mbali ya Bill Clinton kupambana na George Bush ( Baba) alikuwepo mgombea binafsi bilionea Ross Perrot aliyegharamia kampeni za urais wake kwa fedha za mfukoni mwake. Wamarekani hawakuwa tayari kutawaliwa na Rais bilionea Ross Perrot, na pamoja na ushindi wa Bill Clinton, Wamarekani walitilia shaka pia michango aliyopewa Bill Clinton na wafanyabiashara wakihofia kuwa wafanyabiashara hao wangenufaika zaidi kwa misamaha ya kodi. Katika hili, Bill Clinton mwenyewe, mwaka ule wa 1996, alikiri udhaifu huo kwa kutamka;
" Mistakes were made in raising money for my re-election campaign, but contributors did not buy influence with me and the system is not corrupt.." ( Mwandishi, The Guardian, Juni 30, 1996)"- Maggid Mjengwa, Raia Mwema.
Na John Magufuli amewaambia wafanyabiashara jana, kuwa fanyeni kazi yenu ya biashara, lakini, ya Kaizari mwachieni Kaizari, akimaanisha anachotaka walipe kodi.
Maggid, 

No comments: