Thursday, February 25, 2016

UTT-PID YATEMEBELEWA NA MKURUGENZI WA MIPANGO

 Afisa Mtenaji Mkuu wa Taasisi ya Serikali ya Miradi na Manedeleo ya Miundombinu UTT-PID, Dkt. Gration  Kamugisha (kulia), akimkaribisha Mkurugenzi wa Mipango, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Richard Mkumbo, wakati mkurugenzi huyo na tmu yake walipotembelea taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana, kwa lengo la kujua maendeleo ya taasisi na changamoto wanazokabiliana nazo ili kutafuta ufumbuzi wa kuzishughulikia changamoto hizo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Serikali ya Miradi na Manedeleo ya Miundombinu UTT-PID, Dkt. Gration  Kamugisha(aliyesimama kushoto), akielezea mafanikio ya taasisi hiyo na changamoto inayokabiliana nazo wakati timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ilipotembelea taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana. Timu hiyo iko kwenye ziara ya kukutana na watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo hususan Ofisi ya Msajili wa Hazina.
 Mkurugenzi wa Mipango, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Richard Mkumbo, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo
 Dkt. Kamugisha akielezea mafanikiona changamoto ambazo UTT-PID inapambana nazo

Dkt. Kamugisha (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Sheria, UTT-PID, Tuzo Mpiluka, na Mkuu wa kitengo cha Operesheni, Alexsandar Nikolik
 Dkt. Kamugisha na kushoto ni Mkuu wa Operesheni wa UTT-PID, Alexsandar Nikolik
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria, UTT-PID, Tuzo Mpiluka, akifafanua jambo, huku Dkt. Kamugisha (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa miradi, Joyce Mcharo
 Kaimu Mkuu wa Masuala ya kampuni (Head of Corporate Affairs), Eugenia Simon, (katikati), akizungmza huku Mkurugenzi wa Mipango wa wizara ya Fedha na Mipango, Richard Mkumbo, (kulia) na Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa miradi, Joyce Mcharo
 Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa miradi, Joyce Mcharo
 Msabaha A. Msabaha (kulia), Afisa mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, aliyefuatana na Mkurugenzi wa Mipango Richard Mkumbo, akizungumza kwenye kikao hicho. Kushoto ni Afisa Mwingine mwanadamizi kutoka wizara hiyo, Masoud Ridhiwani
 Afisa mwandamizi kutoka Wizara ya Fedhana Mipango, Masoud Ridhiwani akizungumza kwenyekikao hicho. Kshoto ni Mkurugenziwa Mipango, Richard Mkumbo.
 Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi cha UTT-PID, Milton Shango, (kulia), akizungumza kwenye kikao hicho.
 Bw. Shango akifuatilia kikao kwa makini
Bw. Mkumbo akizungumza na uongozi wa juu wa UTT-PID

No comments: