Tuesday, March 8, 2016

RADIO MPYA KUANZISHWA JIJINI MWANZA

Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Uwekezaji unazidi kuwa Mkubwa Jijini Mwanza. Inadaiwa kuna ujio wa Redio Mpya iitwayo Redio ya Wananzengo ambayo inakuja na mapinduzi mengine makubwa katika tasnia ya habari na burudani Jijini Mwanza.


"Mimi nilipoona hizi picha sikuamini kama redio hii iko Jijini Mwanza ila nimeamini baada ya kusikia watu wengi wanaizungumzia sana mtaani". Anasema John, mmoja wa Machinga kutoka Makoroboi Jijini Mwanza".

Binagi Blog inaendelea kufukunyua fukunyua zaidi ili kujua juu ya ujio wa redio hii ya Wananzengo Jijini Mwanza, kwani taarifa hii ni kwa mujibu wa tetesi za mitaani Jijini Mwanza.

No comments: