Tuesday, March 1, 2016

WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA DAMU KWA HIYARI KUOKOA MAISHA

 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa vipimo na mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kulia) wakati wa zoezi la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari lilifanyika eneo la Karume jijini Dar es Salaam kwa siku mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa wiki.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa vipimo na mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kulia) wakati wa zoezi la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari lilifanyika eneo la Karume jijini Dar es Salaam kwa siku mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa wiki.
 Mfanyakazi wa Maabara ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kushoto) akimfanyia vipimo mmoja ya wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kwa hiyari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
  Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakifanyiwa vipimo katika zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa mkazi wa Dar es Salaam akipimwa presha kabla ya kushiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki. 
Mmoja wa mkazi wa Dar es Salaam akishiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.


Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kitengo cha dharura wametoa rai kwa watanzania kujitolea kwa hiyari kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaopokelewa hospitalini hapo.

Akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililofanyika kwa siku mbili mwishoni mwa wiki katika eneo la Karume jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru amebainisha kuwa zoezi hilo ni muhimu sana kwani litasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji huo wanaopokelewa hospitalini hapo kama vile waliopata ajali, wakina mama wajawazito na watoto.

“Hospitali ya Taifa Muhimbili inahitaji wastani wa chupa za damu 100 lakini tunafanikiwa kupata wastani wa chupa 40 hivyo kuwepo na upungufu wa chupa 60 kila siku. Hali hii inapelekea kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji wa dharura tu huku wengine wakisubiri.” Alisema Profesa Maseru

“Wataalamu wananiambia kuwa kwa kawaida, damu inaweza kuhifadhiwa kwa muda wa takribani mwezi mzima kabla ya muda wake wa kutumika kwisha, na kutokana na uhifadhi wa damu kwa muda mfupi ndiyo maana tunasisitiza umuhimu wa watu kuchangia mara kwa mara.  Kitaalamu mwanamume anaweza kuchangia mara nne kwa mwaka na mwanamke mara tatu kwa mwaka.” Aliongezea Profesa Maseru

“Katika wakati wa kutoa huduma ya tiba ya dharura, haswa kwa wagonjwa wa ajali, watoto na wamama wajawazito, upatikanaji wa huduma ya  Ambulance na damu kwa wakati huongeza nafasi ya kuishi kwa wahitaji kwa kiasi kikubwa mno na huduma hizi huokoa maisha ya mamilioni ya wagonjwa kila mwaka duniani kote,” alisema na kumalizia, 

“Natoa rai kwa wakazi wa Dar es slaaam na Watanzania wote kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara ili nchi iwe na akiba ya damu ya kutosha, kwani asilimia moja ya Watanzania wakiamua kuwa wachangiaji damu wa kujirudia Mpango wa Taifa wa Damu Salama utaweza kukidhi mahitaji ya damu nchini.”

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif, kampuni inayojishughulisha na uuzaji na usambazaji wa ving’amuzi kwa ajili ya matangazo ya dijitali ambao walidhamini zoezi hilo amesema kuwa hii ni mara ya pili wao kudhamini zoezi hilo kutokana na umuhimu wake katika kuokoa maisha ya watanzania wote kwa ujumla.

“Hakuna asiyefahamu katika maisha yetu yanayotuzunguka ajali zimekuwa nyingi zinazopelekea watu kupoteza maisha maelefu kubaki mejeruhi wenye uhitaji mkubwa wa damu ili kupata matibabu. Kama tunafuatilia vyombo vya habari basi tutakuwa tunasikia ni mara ngapi kwa wiki ajali zinatokea barabarani na kuacha majeruhi wengi. Kwa upande wa akina mama wajawazito wanahitaji damu kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kujifungua. 

Hatuwezi kukaa pembeni na kuwatizama wakikosa msaada wakati uwezo huo tunao.” Aliongezea Bi. Hanif


“Tumejisikia faraja sana kuwa wamojawapo wa wadau walioshiriki kufanikisha zeozi hili na tunaahidi kuendelea kushirikiana na Muhimbili katika kuwahamasisha watanzania wajitokeze zaidi. 

Kwa mujibu wa wataalamu tunaweza kujitolea damu mpaka mara nne ndani ya mwaka, nina uhakika kila mtanzania akifanya hivyo basi benki yetu ya damu itajaa na tutaweza hata kusaidia wengine wan chi za jirani wenye uhitaji.” Alimalizia Makamu wa Rais kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania.

No comments: