Thursday, July 21, 2016

katibu mkuuazungumza na naibu waziri

Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime, leo 21 Julai 2016, amefanya mazungumzo marefu na  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura ofisini kwa Naibu Waziri huyo. katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu wa Shirikisho aligusia mambo mbalimbali yakiwemo, sehemu za kufanyia kazi za sanaa ya muziki (kumbi), matatizo ya utekelezaji wa Hakimiliki, ukubwa wa kodi za vifaa vya kazi za muziki,  na mengine mengi ikiwemo kumkabidhi Naibu Waziri tafiti mbalimbali zilizofanywa zilizohusu menejimenti ya tasnia ya muziki. Mazungumzo haya yaliyochukua zaidi ya saa mbili, yalifikia kwa makubaliano kuwa kutakuwa na ukaribu zaidi kati ya Wizara na viongozi mbalimbali wa sanaa ili kuboresha mazingira ya utendaji wa kazi za sanaa.

No comments: