Monday, August 22, 2016

HITILAFU YA MKONGO WA MAWASILIANO (OPTIC FIBER), YATATIZA HUDUMA ZA TANESCO WILAYANI BAGAMOYO, SHIRIKA LAWAOMBA RADHI WATEJA WAKE

Sehemu ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani
NA MWANDISHI MAALUM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea kuwatangazia wateja wake wote wa Wilaya ya Bagamoyo kuwa, kutokana na kukatika kwa waya wa mawasiliano, (Optic Fiber) kati
ya Dar es Salaam na Bagamoyo, Ofisi ya Shirika hilo wilayani Bagamoyo bado inashindwa kutoa huduma za kupokea malipo na kuuza LUKU kwa muda mpaka hapo waya huo utakapoungwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Uhusiano MakaoMakuu yaTANESCO, Kwa sasa Shirika linawaomba wateja wake wanaotaka kununua umeme au kulipia huduma zingine za umeme kutumia njia mbadala ya mitandao ya Simu na makampuni mengine yenye mikataba na TANESCO.
Jitihada zinaendelea ili kuhakikisha mkongo huo wa mawasiliano unaungwa mapema iwezekanavyo.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.



No comments: