Friday, December 30, 2016

MBUNGE MUSSA WA JIMBO LA TANGA AWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA WANANCHI WA JIMBO LAKE

MBUNGE MUSSA WA JIMBO LA TANGA AWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA WANANCHI WA JIMBO LAKE

Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Mussa Mbaruku amewatakia heri ya sikukuu ya mwaka mpya wakazi wa Jimbo lake  na kuwataka wajitume zaidi ili kuweza kupata mafanikio.

Akitoa salamu hizo kwenye ofisi yake wakati akizungumza na waandishi wa habari leo,Mbunge Mussa aliwataka wananchi hao kutambua kuwa wanashirki kwenye shughuli za kimaendeleo ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Alisema licha ya kushiriki huo lakini pia wakulima watambue katika kipindi hiki wanapaswa kutayarisha mashamba yao ili kuweza kulima kilimo cha kisasa chenye tija.

Aidha pia aliwataka kuhakikisha wanawajibika kusafisha maeneo yao ili yaweze kuwa na muonekana mzuri ili waweze kuepukana na magonjwa ya milipuko yanayoweza kutokana na kuwepo kwa hali hiyo.

 “Lakini pia ni niwatake halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha wanasafisha maeneo yao kwa kuondoa takataka “Alisema Mbunge Mussa.

Sanjari na hilo Mbunge huyo pia aliwataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwenye Jimbo lake kuhakikisha wanaongeza bidhii kwenye masomo ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao

 “Niwaambie wanafunzi wakati wanapokuwa shuleni acheni masuala ya michezo badala yake hakiksheni mnazingatia elimu kwani ndio mkombozi mkubwa kwenye maisha yenu ya sasa na baadae “Alisema.
habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments: