Wednesday, December 7, 2016

MSD YAZINDUA HUDUMA MAALUMU KWA WATEJA WAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO



Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  Profesa Mohamed Janabi (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu (kulia), akitoa taarifa fupi ya mradi huo mbele ya mgeni rasmi.
Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD, Salome Malamia akizungumza katika hafla hiyo.
Mmoja wa maofisa kutoka Ofisi ya Inayosimamia Utekelezaji wa Mapendekezo ya Maboresho (SMO), Naomi Shangali akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu mpango huo.
Ofisa wa SMO, Frankie Nkone akieleza kazi za eneo lake zinavyofanyika.
Kikosi kazi cha SMO. kutoka kushoto ni Benjamin Mtesigwa, Frankie Nkone, Naomi Shangali, Marko Masala na kiongozi wao, Cosmas Nalimi.
Naomi Shangali (kulia), akiwaelekeza jambo maofisa wenzake.
Wajumbe wa mkutano huo kutoka sekta ya afya wakiwa wameinamisha vichwa vyao kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, marehemu Profesa Idris Mtulia aliyefariki jana.
viongozi  wa sekta ya afya wakiwa kwenye mkutano huo.
mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea.
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya  Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akiwa na viongozi wa sekta ya afya katika uzinduzi huo.
Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.


Baadhi ya wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye mkutano huo.


Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu (katikati), akiteta jambo na mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya wakati wa mkutano huo. Kushoto ni  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Hiiti Sillo.


Viongozi wa sekta ya afya wakiwa wameinua mikono juu kuridhia mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa wakati wa uzinduzi wa mpango huo ulioandaliwa na Bohari ya Dawa (MSD), katika mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa SMO.
Picha ya pamoja ya  viongozi na mgeni rsami.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI  ya dawa (MSD) imezindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wake wakubwa, kama moja ya hatua za kuboresha huduma kwa wateja. 

Mpango huo utawawezesha wateja hao kupata huduma ya haraka zaidi pindi wanapokuwa wanahitaji mahitaji yao.

Wateja hao ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hosipitali ya Sekoutoure Mwanza, Hospitali ya Kibong’oto, Mirembe, Hosipitali za Amana, Temeke, Mwananyamala, KCMC, Hospitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Akizindua mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya amesema mpango huo ni moja ya maboresho yanayofanywa na MSD, ili kuhakikisha huduma zake zinatolewa kama inavyohitajika.

Dk. Mpoki pia amewasisitiza wateja hao wakubwa wa MSD kuhakikisha wanafanya maoteo sahihi ya mahitaji yao na kuyaleta MSD kwa wakati ili kuepusha ucheleweshwaji wa taratibu za manunuzi ambao pia itasababisha dosari kwenye upatikanaji wa dawa kwa wateja. 


Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu  amesema hatua ya kuwahudumia wateja hao kwa kiwango kizuri na cha uhakika itafanikiwa, hivyo Watarajie maboresho makubwa ya huduma ya upatikanaji wa dawa. 

No comments: