Friday, December 30, 2016

TAASISI YA MO DEWJI YATOA ZAWADI KITUO CHA TUMAINI LA MAISHA

Taasisi ya MO Dewji Foundation imeweza kuwakumbuka watoto wanaopatiwa matibabu ya magonjwa ya kansa katika kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Katika kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwemo kuingia mwaka mpya wa 2017, MO Dewji Foundation imeweza kutembelea watoto wa kituo hicho cha Tumaini la Maisha na kutoa zawadi kwa watoto hao ili kuwasaidia katika kipindi wawapo kituoni hapo wakiendelea na kliniki ya matibabu yao.
Kwa zaidi ya miaka mitatu MO Dewji Foundation imekuwa ikitoa ufadhili na mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto hao, mafunzo kwa watoto hao wawapo kituoni hapo, gharama za usafiri kwa watoto kuja na kurejea kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya matibabu yao katika wodi yao iliyopo Hospitalini hapo Muhimbili. Katika tukio hilo, Mo Dewji Foundation waliweza kutoa vitu mbalimbali kama zawadi kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya kituo hicho. 
Miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na unga wa ngano, sabuni za kunawia mikono, sabuni za kuogea, doti za khanga, mafuta ya kupikia na vitu vingine vingi. Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez amewatakia kila lakheri watoto na wazazi wa kituo hicho katika kuingia mwaka mpya ambapo pia aliwahakikishia wafanyakazi wa kituo hicho kuwa taasisi yao itaendelea kusaidia kituo hicho.
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akimkabidhi Mwalimu Leonard ambaye
ni mwalimu anayetoa elimu kwa watoto wenye kansa wanaopatikana kituoni hapo.
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akikabidhi zawadi hiyo kwa mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho cha TLM
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo hicho, pamoja na baadhi ya watoto hao wa TLM.
Mratibu wa Miradi wa MO DEWJI Foundation, Catherine Decker akiwa pamoja na watoto wa TLM, wakati wa tukio hilo la kuwafariji watoto pamoja na kutoa zawadi.
Mwalimu Leonard wa TLM akiwa na mmoja wa watoto wa kituo hicho wakati wa tukio hilo la kutoa zawadi.
Jengo la TLM

No comments: