Wednesday, January 4, 2017

WANASHERIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM WAJIUNGA NA PSPF


 Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari, akitoa ufafanuaiz kuhusu kazi zifanywazo na Mfuko huo, hususan
uchangiaji wa hiari, (PSS), mwishoni mwa seina ya mafunzo ya siku mbili, kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, iliyomalizika leo Januari 4, 2017. Baada ya semina hiyo wanasheria hao zaidi ya 35 walijiunga na Mfuko huo kupitia mpangio huo wa PSS.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WATUMISHI wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF baada ya kuhudhuria semina ya mafunzo ya siku mbili iliyomalizika leo Januari 4, 2017.
Semina hiyo iliandaliwa na Mfuko huo kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makodna, kutaka wanasheria wa ofisi yake, wapewe semina ili kuwajengea uwezo wa kutatua kero za wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo watakaofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa shida zinazohusiana na masuala ya Mafao na Pensheni.
Katika senmina hiyo iliyoanza Januari 3, 2017, wanasheria hao walipatiwa ufafanuzi wa kina kuhusu shughuli namajukumu yanayotekelezwa na PSPF.
Meneja wa PSPF huduma kwa wateja, Bi.Leila Magimbi, alitaja majukumu hayo kuwa ni pamoja na  kutambua na kusajili wanachama wapya, kukusanyan michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama, kuwekeza michango katika vitegauchumi mbalimbali na kulipa mafao.
Shughuli nyingine zinazotekelezwa na Mfuko huo ni kulipa mafao kwa wanaostahili kwa mujibu wa sheria, kutunza kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya ubora wa mafao na kufanya tathmini ya Mfuko na kuweka mikakati endelevu, aliongeza Bi. Magimbi.
Pia wanasheria hao walipata fursa ya kuelezwa aina za wanachama wa PSPF ambao ni Watumishi wa Umma, sekta binafsi ambao hawa watachangia katika mfumo wa uchangiaji wa lazima na watu wote walio katika sekta isiyo rasmi, ambao wao watachangia katika Mfumo wa uchangiaji wa Hiari.
Aidha faina apatazo mwanachama wa PSPF, kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mafao, Bw.Haji Moshi, ni pamoja na Fao la uzazi, mkopo wa elimu, mkopo kwa mwajiriwa mpya, mikopo ya viwanja, mikopo ya nyumba, mkopo wa fedha taslimu, mikopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu, mafao ya muda mrefu, fao la ulemavu, fao la mirathi, fao la kufukuzwa au kuachishwa kazi, na bima ya afya.
Akifunga semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewataka wanasheria hao kutumia busara wanapohudumia wananchi kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
“Huko mtakutana na watu wa aina mbalimbali, wengine wamesoma zaidi yenu, wengine hawakupata fursa ya kusoma kama nyinyi, kwa hivyo mnao wajibu wa kutunmia busara katika kuhudumia wananchi wa kada tofauti tofauti.” Aliwaasa Bw. Mayingu.
Aidha mwakilishi wa wanasheria hao, Bi.Georgia Ephraim Kamina, amesema semina hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwao, na kuishukuru PSPF kwa kuandaa semina hiyo na kuuomba uongozi wa Mfuko, kujenga mahusiano ya kudumu baina ya Mfuko na wanasheria hao katika utendaji kazi wao wa kuhudumia wananchi.
Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Bw. Magira Werema, akifafanua masuala kadhaa yahusuyo shughuli za Mfuko na faida zake kwa wanachama
 Afisa wa idara ya Pensehni ya Mafao wa PSPF, Bw.Andrew Dayson akitoa mada
 Kaimu Meneja wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko huo, Bi.Sophia Mbilikira, akielezea faida za kuwa mwanachama kupitia uchangiaji wa hiari
 Baadhi ya washiriki (wanasheria), wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu wa PSPF
 Baada ya kuelewa "somo" hatimaye ilifika wakati wa wanasheria hao kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), na hapa wanajaza fomu


 Obote Simon, akikabidhiwa kadi ya kujiunga na uanachama wa PSPF, kupitia mpango wa PSS, kutoka kwa Kaimu Meneja wa PSS, Bi. Sophia Mbilikira
 Bw. Mahfoudh K. Mohammed (kushoto), akipokea kadi yake
 Bw. Emmanuel S. Nyanza, (kushoto), akipokea kadi yake
 Bw. Albert Nyange, (kushoto), akipokea kadi yake
 Kongozi wa Wanasheria wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Georgia Sphraim Kamina, akizunguzma
 Bi. Kissa, akiuliza swali kuhusu mikopo ya elimu

 Meneja Masoko na Uhusiano wa PSPF, Bi. Costantina Martin, (kulia), akiwa amejiungana wanasemina wakati semina hiyo ikielekea ukingoni


 Sehemu ya utunzaji nyaraka kwenye mfumo wa makabati yanayoendeshwa kielektroniki

 Msaidizi maalum wa Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Bw. Daniel P. Jenga, (kushoto), akifurahia kuonyeshwa faili lake ndani ya dakika moja
 Afisa wa PSPF akiwa kazini
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akitoa nasaha zake wakati wa kufunga semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na uendeshaji, Bi. Neema Muro
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akitoa nasaha zake mbele ya wanasemina hao wakati wa kufunga semina hiyo
 Wanasemina wakitembelea kitengo cha kutunza kumbukumbu cha PSPF

 Meneja Huduma kwa Wateja, PSPF, Bi. Leila Magimbi

No comments: