Wednesday, March 22, 2017

TANZANIA NA CHINA ZATILIANA SAINI MKATABA WA MIAKA MITATU WA MASUALA YA UTAMADUNI

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia) wakibadilishana mkataba wa makubaliano utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya nchi hizo wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena ijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati), akipokea zawadi kutoka kwa  Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Profesa, Elisante Ole Gabariel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto), na Naibu Waziri wa Utamaduni wa
China, Dong Wei wakiangalia zawadi.
Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto), na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei wakisaini mkataba huo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)



No comments: