Monday, April 3, 2017

BREAK NEWS,CHADEMA YAPATA PIGO MUHEZA MWENYEKITI WA WILAYA HIYO AJIUNGA NA CCM


 Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kutangaza azma ya kuondoka Chadema na kuhamia CCM 


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Tanga kimepata pigo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias
Karuwasha kuamua kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kutokana na chama hicho kupoteza dira na mwelekeo.
Lakini kubwa zaidi inatokana na mambo yanayofanywa na chama hicho kwa kuiondoa uhalisi wa chama hicho ambayo wananchi walikuwa wanaitegemea kuwa chama cha kuwa mshindani na CCM ili kuleta mabadiliko.
Hatua ya mwenyekiti huyo kutangaza kujiuzulu inakuja siku chache baada ya maamuzi wa mkutano mkuu wa viongozi wa chama kanda ya kaskazini mjini Tanga uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kuridhia kuvunja uongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya ya mkoa wa Tanga.
Akitangaza uamuzi huo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa BMK uliopo Sahare Jijini Tanga,Rwebangira Karuwasha alisema hayo ndio mambo makubwa yaliyopelekea kuamua kukaa pembeni na kujiunga na CCM ambako anaona kuna sera makini zinazotekelezeka .
Alisema kutokana na matukio mbalimbali anayoyafanya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe sitegemei kuendelea kubaki kwenye chama hiki cha watumwa  na watwana hivyo nimeamua kujiunga na CCM kwani ndio chama kinachoweza kutekeleza sera makini na zenye mafanikio.
“Kwa mfumo wa uongozi unaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe haukubaliki na hakuweza kuvumilia.... sitegemei kuendele kuwepo kwenye chama hicho kilichokuwa cha watwana na watumwa hivyo nimeridhia kujiunga na CCM “Alisema.
“Kuanzia leo mimi sio mwanachama wa Chadema  na nitajiungha na CCM ya sasa chini ya Rais Dokta John  Magufuli sababu Chadema wameacha sera na makini kwa ajili ya kuwapa maendeleo wananchi.
Alisema pia sababu nyengine ni kutokana na utendaji wa Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambao umekuwa mstari wa mbelea kujali wanyonge na kusaidia harakati za kimaendeleo hapa nchini.
Aidha alisema wameshindwa kuelewa kuwa Mwenyekiti Mbowe alipangua gia angani kumuondoa dkta Slaa wakati alipokuwa kwenye chama hicho jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa chama hicho. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments: