Sunday, April 30, 2017

Tigo yasherehekea siku ya Tehama kwa Mtoto wa Kike Afrika kwa kutoa msaada wa Kompyuta 10 shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Ufundi wa Kampuni ya Tigo, Jerome Albou (katikati), akimkabidhi moja ya kompyuta Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Jangwani, Amon Mgongolwa (kushoto), ambao ni msaada wa kompyuta 10 zilizotolewa jana na kampuni hiyo kwa ajili ya matumizi ya shule, kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Dorosela Rugaiyamu na Meneja Huduma za Wateja Halima Okash.


Mkurugenzi Mtendaji wa  Shule Direct, Faraja K. Nyalandu (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusu shule Direct  kwa  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi, Dorosela Rugaiyamu na  Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Jangwani, Amon Mgongolwa mara baadaa ya  makabidhiano ya msaada wa kompyuta 10 zilizotolewa jana na kampuni na Tigo  kwa ajili ya matumizi ya shule.





Wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani wakishuhudia makabidhiano ya  msaada wa kompyuta 10 zilizotolewa jana na Tigo  kwa ajili ya matumizi ya shule,


Dar es Salaam Aprili 28, 2017- Kampuni inayoongoza Tanzania katika maisha ya kidijitali Tigo leo imetoa kompyuta 10 kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wasichana katika Tehama, tukio ambalo linachangia  kuziba pengo la jinsia katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasialiano (Tehama). Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Ongeza Upeo, Badilisha Tabia”.
 Siku ya Kimataifa ya Wasichanaktika Tehama ni mkakati wa Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano ya simu (ITU) ambao unalenga  kuwezesha  na kuwahimiza wasichana na wanawake vijana kuzipa nafasi ajira zilizopo katika sekta ya teknolojia ya habari.
Akizungumza wakati wa tukio la kutoa msaada huo lililofanyikakatika Shule ya Sekondari Jangwani, Ofisa Mkuu wa Ufundina Mawasiliano wa Tigo, Jerome Albou alisema kuwa Tigo imejikita katika kuchangia uwezeshwaji wa wanafunzi, hususani wasichana, ili waweze kuingia katika mtiririko wa ulimwengu katika  habari na uelewa, ambapo watajifunza, na kupanua ubunifu wao na kushirikiana na wenzao kote duniani kupitia mikakati iliyo ndan ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
 “Msaada wa kompyuta hizi upo katika mkakati wa Tigo wa kusaidia kuwawezesha wanawake na wasichana  kupitia  teknolojia za habari na mawasiliano,” alisema Albou akibainisha kuwa Tigo imejikita katika kutekeleza  dira ya serikali ya kuibadilisha nchi kuwa  ndani ya uchumi wa uelewa ifikapo mwaka 2025 kupitia ukuzaji na kuwavutia wanawake kuingia katika  mafanikio makubwa ya  nguvukazi anuai.
 Mgeni rasmi katika  hafla hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, Dorosela Rugaiyama,aliipongeza Tigo kwa mchango huo, akisema kwamba kompyuta hizo zitawafikisha mbali wanafunzi katika kusambaza stadi na uelewa wa Tehama za kisasa kwa vijana, kuwawezesha kukabiliana na changamoto za mwenendo wa mabadiliko ya habari katika jamii na duniani kwa ujumla.
 Shughuli nyingine ambazo  zilifanyika katika Shule ya Sekondari Jangwani, ambayo ni mojawapo ya vituo vya miradi ya Shule-elektroniki ya Tigo tangu mwaka 2015, ni pamoja na uwasilishaji wa program mbalimbali za komputa kutoka kwa wanafunzi vijana  ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao  chini ya  mkakati wa Kidijitali wa Waleta mabadiliko ya Tigo (Tigo Digital Changemakers-TDC)-wakisimamiwa na washindi wa zamani wa TDC, Carolyne   Ekyarisiima, ambaye Mradi wake wa Apps and Girls unaziba pengo katika Tehama kupitia  teknolojia za kidijtali, na Faraja Nyalandu muasisiwa Shule Direct, ambao ni ujasiriamali jamii kidijitali ambao unatoa mada za elimu katika kusaidia kukabiliana na changamoto za uhaba  wa walimu.
Serikali ya Tanzania inazitaka  shule  kufundisha  masomo ya msingi ya kompyuta lakini ni asilimia 5 tu ya shule zina kompyuta nchini kwa sasa. Umahiri katika Tehama  unabakia kuwa mbali lakini  kutokana na Tigo kutoa msaada pamoja na wadau kuchangia malengo ya mabadiliko yanaweza kuhamasisha wadau wengine kuchangia  kufikiwa wa malengo yaliyowekwa na serikali yanayolenga katika kuziwezesha shule zaidi ya 700 na zana za Tehama zikiwemo kompyuta.
Mradi wa Shule-elektroniki ni moja ya  miradi ya kampuni katika mikakati ya uekezaji kijamii na kupitia mradi huu Tigo imeweza  kuunganisha shule zaidi ya 60  za serikali nchini Tanzania na intaneti ya kasi na ya uhakika ya 4G LTE.

No comments: