Wednesday, May 3, 2017

MAONYESHO YA SITA YA MADINI YA VITO YAANZA RASMI LEO JIJIJI ARUSHA

 Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akifatilia jambo wakati alipokuwa anazindua rasmi maonyesho ya sita ya vito na madini yanayofanyika katika hotel ya Mounti Meru ilipo jijini  Arusha(habari picha na Woinde Shizza,Arusha)


 Meya wa jiji la Arusha naye aliuzuria katika uzinduzi wa maonyesho haya ya vito na madini


Na Woinde shizza,Arusha



 wananchi wengi wanaoishi karibu na migodi mbalimbali inayochimba madini  ya aina mbalimbali wamekuwa hawanufaiki kupitia madini hayo kutokana na viongozi wao wa maeneo husika kutokuwa na  usiano mzuri na wamiliki wa migodi hiyo.



Hayo yamebainishwa na mbunge wa jimbo la Simanjiro Jemsi ole milya wakati akiongea katika uzinduzi wa maonyesho   vito na madini  yaliofunguliwa leo jijini hapa



Alisema kuwa japo kuwa madini mengi yenye dhamani yanachibwa hapa nchini lakini ukifuatilia maisha ya wananchi wa maeneo ambayo madini hayo hayafanani kabisa nao kwani asilimia kubwa ya wananchi hao ni maskini sana  na wengine awajiwezi



“asilimia kubwa  ya wananchi ambao madini hayo yanachibwa ukifatilia maisha yao hayafai kwani ni duni  hawana maendeleo  yoyote ,kwa ufupi awanufaiki na madini ambayo yanatoka katika maeneo yao hivyo ni wajibu waserikali kuangalia upya swala hili na kuanza kufatilia kwani ni kitu cha kusikitisha unakuta mwananchi mfano wa mererani madini yanachibwa kwao lakini ukiangalia maisha anaoyoishi uwezi sema anakaa sehemu Tanzanite inatokea kwa jinsi anashida”alisema Milya



Naye  kaimu naibu katibu mkuu wa wizara ya Nishati na madini Jemsi Mdoe  alisema kuwa sera ipo na sheria ipo ya kuakikisha wananchi ambaowanazunguka maeneo ya migodi wanasaidiwa  na migodi hiyo lakini ukifuatilia kwa kiasi kikubwa wale wananchi ambao hawanufaiki ni wale ambao unakuta viongozi wao wa mtaa au kijiji awanaushirikiano mzuri na viongozi au wawekezaji waliowekeza katika maeneo yao ,hivyo ni wajibu wawanchi pamoja na viongozi kurikiana kwa pamoja na kuungana ili kuweza kusaidia



Akizungumzia maonyesho haya ya vito na madini   (Arusha Gem Fair )alisema kuwa haya ni maonyesho ya sita kufanyika na yanafanyika kwa muda wa siku tatu   lengo ikiwa   kutimiza dira iliopo  katika sera ya madini ya mwaka 2009  inayosisitiza kuwa Tanzania iwe kitovu cha madini .



Alisema kuwa sekta ndogo ya vito inachangia katika uchumi wa maendeleo ya jamii  hivyo maonyesho haya  ni fursa kwa wachimbaji  na wafanyabiashara wa hapa nchini kuweza kupata fursa ya kujitangaza zaidi



“unajua  wageni wengi kutoka nchi mbalimbali wanauthuria katika maonyesho haya wengine wanakuja kununua madini wengine wameleta madini yao ili yauzwe kwaiyo hii ni fursa ya pekee ya wachimbaji wetu wa ndani kujitangaza na kupanua soko la zaidi kikubwa zaidi  waangalie ni namna gani watayafanya madini yao yawe na dhamani zaidi”alisema Jemsi


 baadhi ya madini yaliyoletwa katika maonyesho

No comments: