Monday, May 29, 2017

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AVUNJA REKODI KKKT USHARIKA WA ENABOISHU NA KUFANIKISHA UPATIKANAJI WA MILIONI 39 NA VIONGOZI WAMBARIKI

 
Na Mwandishi Wetu, Arusha

Watumishi wa halmashauri ya Jiji La ARUSHA Kwa kushirikana na Mkurugenzi wao Bwana Athumani Juma Kihamia wamechangia kiasi cha shilingi Milioni 14 kwenye ibada ya harambee ya kuchangia maendeleo ya mtaa iliyofanyika katika kanisa la KKKT  usharika wa Enaboishu
halmashauri ya Arusha .

Katika Ibada hiyo ya harambee ya kuchangia maendeleo mtaa wa Loruvani ambapo mgeni Rasmi alikuwa Mkurugenzi Kihamia amesindikizwa na watumishi pamoja na wadau wake wa karibu  wamechangia Fedha hizo kwa ajili ya kuwatia waumini wa kanisa hilo kwa ajili ya maendeleo yao.

Ibada hiyo ya aina yake ambayo kila Mtumishi alitoa mchango wake papo kwa papo na wengine kwa kuahadi wamesema kuwa wamependezwa na tabia ya Mkurugenzi wao anavyowapa ushirikiano  na Moyo wa Upendo na si kazini tu bali na nje ya kazi ndiyo mana wakamsindikiza katika ibada hiyo.
Hata hivyo amewataka Watanzania kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo bila kujali dini ,kabila ,au Rangi anayotoka.

Kihamia amesema kuwa jamii inapokuwa na ushiriano mzuri hata Mungu anawasaidia watu na kusisitiza suala La Amani ambalo ndiyo msingi Mkubwa katika kuabudu.

Naye mchungaji wa kanisa hilo la KKKT Mchungaji Prosper Kinyaha amemuombea maombi maalum mkurugenzi Kihamia Mungu aendelee kumbariki kwa moyo wake wa ushirikiano na upendo wa kuchangia michango hiyo kwa kushirikana na wadau aliokuja nao.

Katika hafla hiyo mkurugenzi Kihamia alikutana na walimu wake waliomfundisha katika shule ya sekondari magamba Boys iliyoko wilayani Lushoto kwa kipindi 1986 mpaka 1992 ambapo wameshangaa kumuona mwanafunzi wao ambaye kwasasa ni kiongozi wa jiji la arusha na kusema kuwa alikuwa ni moja ya mwanafunzi msikivu kwa walimu wake.

No comments: