Thursday, July 13, 2017

Bondia Mcongo Atamba Kumkalisha Mbongo Taji la Global TV

KATIKA historia ya mchezo wa ngumi za kulipwa duniani, DR Congo inakumbukwa kutokana na kufanyika kwa pambano kubwa katika uzito wa juu kati ya Muhammad Ali ‘The Greatest’ dhidi ya George Foreman wote wakiwa ni Wamarekani. Pambano hilo lililofanyika Oktoba 30, mwaka 1974 kwenye Uwanja wa Stade du 20 Mai, Kinshasa, ambalo lilipewa jina la ‘Rumble in the Jungle’ Ali alishinda dhidi ya Foreman kwa KO katika raundi ya nane, pambano likiwa ni la raundi 15 ambapo moto wake haukuwa wa kitoto.  
Regin Champion - Congo.[/caption]   Huenda hii ikajirudia Julai 22, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live pale bondia kutoka DR Congo, Regin Champion atakapooneshana umwamba na Mtanzania Idd Pialali katika pambano la kimataifa la kugombania Ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati ambalo litarushwa mubashara na Kituo cha Global TV kupitia www.globaltvtz. com.   Mapambano mengine yatakuwa ni kati ya bondia, Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ atakayezipiga na Israel Kamwamba raia wa Malawi, wakati Nasibu Ramadhan ‘Pacman’ akitarajia kucheza na Bernard Mwango kutoka nchini Zambia. Mapambano hayo yote ni ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati na yatakuwa ni ya raundi kumi.    
Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ -Tanzania.[/caption]   Showbiz Xtra imezungumza na bondia
huyo kutoka DR Congo kuelekea pambano hilo ambapo amefunguka kwa kujivunia historia iliyoachwa na mabondia waliopigana katika ardhi ya nchi yake. Champion alisema: “Baba yangu ndiyo sababu kubwa ya mimi kucheza ngumi za kulipwa nchini mwangu, namshukuru sana kwani nazipenda na zimenipa mafanikio. “Nimecheza mapambano mengi, nimepoteza mapambano matatu mengi nikiwa nimeshinda. “Sitaki kusema sana lakini huyo mpinzani wangu (Pialali) nitampa raundi tatu pekee za kucheza baada ya hapo ni kichapo kikali. “Nadhani shida yangu kubwa ni kushinda huo Ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati kwa sababu nimeshacheza Zambia, Angola, Zimbabwe, Msumbiji, Malawi na Congo na mimi ndiye bingwa wa hapa DR Congo.    
Nasibu Ramadhan ‘Pacman’ -Tanzania[/caption]   Unakuja kucheza ugenini, labda una kipi cha kuwaambia mashabiki wako? “Kiukweli nitashukuru kwanza kwa Watanzania ambao watanisapoti pamoja na Wacongo wote ambao wanaishi huko naomba wanipe ushirikiano ndugu yao. Nakuja Tanzania kwa ajili ya kumchakaza mpinzani wangu. “Mpinzani wangu simjui kabisa na naamini pia hanijui lakini kutokana na maan-dalizi amb-ayo naya-fanya, sina hakika kama ataweza kutoka kwa sababu siku zote huwa sipendi mchezo ninapokuwa juu ya ulingo, kwani kazi yangu ni kuchapa tu. “Sihofii chochote kuhusu yeye, kikubwa nadhani ajipange kwa sababu huenda akawa anafikiria kuwa Champion ni bondia wa kawaida ila nataka nimwambie ajue kuwa tutajuana vizuri kwenye ringi, kiufundi na kimbinu maana siwezi kukubali kupigwa kirahisi hasa ukilinganisha na umbali wa sehemu niliyotoka. “Najua ngumi ni vita ambayo inakuwa ya watu wawili wakipigana kwa mikono sasa nipo tayari kuona nasitisha uwezo na kipaji cha mpinzani wangu katika raundi chache za mwanzoni kwa kumpoteza kabisa hilo anapaswa kulijua hata kama atakuwa anacheza katika ardhi ya kwao.  
Idd Pialali - Tanzania. [/caption]   “Nimeambiwa pambano hilo litakuwa live kupitia Kituo cha Global TV Online ni kitu kizuri hasa kwa upande wangu kwa sababu mashabiki wangu na Wacongo wataweza kuona nitakachokuwa nakifanya katika ulingo huko. “Nimeomba nipewe ‘links’ mapema kwa ajili yao ili waanze mara moja kujiweka tayari kushuhudia mambo ya kutisha nitakayoyafanya, naamini historia ya pambano la Muhammad Ali na George Foreman ambao walicheza kwenye ardhi yetu kuwa itanibeba licha ya kusimuliwa na kuisoma tu,” anasema Champion.  
Israel Kamwamba - Malawi.[/caption]   Katika hatua nyingine, pambano hilo, hakutakuwa na kiingilio na mashabiki wataweza kulishuhudia mubashara kupitia simu zao za mkononi kwani litaoneshwa na Global TV pekee. Wadau na mashabiki watakaopata nafasi ya kuingia ukumbini wataingia kwa kadi maalum za mwaliko.   [
Mikanda ya ubingwa wa Global TV Online.[/caption]   Ili kulishuhudia pambano hilo kwa njia ya simu tena bure, hakikisha unajiunga (SUBSCRIBE) na YouTube Channel ya Global TV Online sasa hivi ili usipitwe. Ingia YouTube, tafuta GLOBAL TV ONLINE, kisha bonyeza neno SUBSCRIBE pia bonyeza kikengele kidogo kilichopo pembeni yake ambacho kitakukumbusha kuangalia pambano hilo mara tu litakapoanza. Kama wewe umeshajiunga, basi hakikisha pia umebonyeza kikengele ili usipitwe na kila kinachoendelea Global TV. Pia unaweza kutupata kupitia mtandao wa www.globaltvtz. com, jiunge sasa na Global TV ili uwe wa kwanza kuona ndondi za kimataifa. Kajiunge sasa kwa kuingia www.youtube.com/user/ uwazii.  

IBRAHIM MUSSA | GLOBAL PUBLISHERS

WATAKAOCHUANA HAWA HAPA

No comments: