Wednesday, August 23, 2017

MWENYEKITI WA BODI IKUNGI SEKONDARI AMSHUKURU DC IKUNG

BMG Habari
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu ameendelea kupokea pongezi baada ya kuanzisha ligi soka ya "Ikungi Elimu Cup 2017" ili kuhamasisha wananchi wa wadau mbalimbali ili kusaidia utatuzi wa changamoto za elimu wilayani humo.


Kwenye uzinduzi wa ligi hiyo uliofanyika jumamosi Agosti 19,2017 uwanja wa shule ya sekondari Ikungi, Mhe.Mtaturu alikabidhi mifuko 100 ya simenti na kuungwa mkono na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali waliochangia mifuko 194 na hivyo kusaidia upatikanaji wa mifuko 294 kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Ikungi ambao ulikwama tangu mwaka 2009.


Siku hiyo pia ulifanyika uzinduzi wa zoezi la kufyatua matofali ambapo Kata zote wilayani Ikungi zimedhamiria kufyatua matofali 10,000 kila Kata ili kusaidia ujenzi wa madarasa, nyumba za waalimu, maabara pamoja na vyoo.
Tazama video hapo chini

Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu (wa pili kushoto) akikabidhi mifuko 100 ya simenti ya kwa ajili ya ujenzi wa maabara shule ya sekondari Ikungi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Mtaturu akishiriki zoezi la uzinduzi wa ufyatuaji matofali kwenye Kata zote wilayani Ikungi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, maabara, vyoo na nyumba za waalimu ambapo kila Kata itaanza kwa kufyatua matofali elfu kumi
Mgeni Rasmi, Katibu Tawala mkoani Singida, Dkt.Angeline Lutambi akizindua zoezi la ufyatuaji matofali wilayani Ikungi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Dkt.Rehema Nchimbi.
Mgeni Rasmi, Katibu Tawala mkoani Singida, Dkt.Angeline Lutambi (kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Mtaturu (kulia), wakisogeza tofali wakati wa uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji matofali wilayani Ikungi

No comments: