Wednesday, April 11, 2018

MICHUANO YA COPA COCA-COLA UMISSETA YAPOKELEWA KWA SHANGWE MKOANI TANGA

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella akipokea zawadi ya mpira kutoka kwa Meneja wa chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella akipiga danadana katika uzinduzi huo

 Wanafunzi wakipokea vifaa vya michezo. Wanafunzi wakichuana katika mchezo wa soka siku ya uzinduzi.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio ya uzinduzi.
Na Mwandishi Wetu. Mashindano ya shule za sekondari ya Copa Umisseta yanayoendelea ngazi ya mikoa, yamezinduliwa mkoani Tanga, katika uwanja wa Mkwakwani na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali , wadau wa michezo na mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella. Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye alimwakilisha Waziri wa TAMISEMI, aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kutoa udhamini wa mashindano ya ngazi za chini na aliipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kudhamini mashindano haya na kuahidi kuwa serikali itafanya kila jitihada kuunga mkono jitihada za kufufua michezo ya mashuleni ili kuhakikisha inashirikisha wanafunzi wengi. “Serikali itahakikisha inajenga miundombinu ya michezo sambamba na kuhakikisha walimu wanapatiwa mafunzo ya taaluma ya michezo,pia tutahakikisha ratiba za vipindi vya michezo mashuleni zinafuatwa badala ya kutumia muda wa vipindi hivyo kufundisha masomo mengine”Alisema Shigella. Kwa upande wake Meneja wa chapa ya Coca-Cola nchini, , Sialouise Shayo,alisema kampuni ya Coca-Cola kupitia udhamini wake inahakikisha wanafunzi wanaoshiriki mashindano haya wanapatiwa vifaa vya michezo. “Kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikidhamini mashindano haya ya Copa Umisseta kwa kipindi cha miaka mitatu sasa,lengo letu kubwa ni kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo kuanzia ngazi ya chini,tunaamini kuwa michezo mbali na kujenga afya pia ina fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi”alisema Shayo. Kampuni ya Coca-Cola inatarajia kutoa vifaa vya michezo kwa shule za sekondari 4,000 kutoka mikoa mbalmbali nchini. Uzinduzi wa mashindano haya mkoani Tanga ni wa pili kufanyika baada ya kuzinduliwa mkoani Dodoma na unatarajiwa kufanyika katika mikoa mingine sita nchini kabla ya kufanyika katika ngazi ya Taifa mwezi Juni mwaka huu koani Tanga.

No comments: