Monday, January 5, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Janet: Hii ndiyo listi ya wanaume aliyowahi kujiachia nao!

Tukiwa ndani ya siku ya tano tangu tulipoianza 2009, staa wa R&B Marekani na duniani kwa ujumla, Janet Jackson ndiyo anatufungulia mwaka mpya kwa kuapia kunako safu hizi ikiwa ni maombi ya baadhi ya wasomaji ambao wametamani kufahamu msanii huyo amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa gani wa kiume.

Akiwa na umri wa miaka 43 sasa, staa huyo ambaye alizaliwa kwa jina la janet Damita Jackson mpaka sasa ameshajiachia na mastaa wa kiume zaidi ya kumi ambao ni Rob Lowe, Robert DeNiro, James DeBarge, Gary DeVore, Rene Elizondo, Tupac Shakur, Q-Tip, Matthew McConaughey na Wanya Morris.

Vile vile Janet amewahi ‘kujiramba’ na aliyewahi kuwa ‘boyfriend’ wa mwanamuziki Britney Spears, Justin Timberlake na hivi sasa anaonekana kujiweka moja kwa moja kwa mtayarishaji muziki, Jermaine Dupri ambaye aliwahi kuwa na uhisiano naye tangu 2001 kabla ya kuachana na kurudiana tena miaka ya hivi karibuni.

Msomaji, huyo ndiyo Janet Jackson na wanaume aliowahi kujiachia nao, kama utapenda kujua staa gani aliwahi kuwa na usiano na kina nani? Tutumie ujumbe mfupi ukitutajia jina lake kisha tuma kwenda namba 0715-110 173. Pamoja sana.
***********************************************

Maajabu ya Zena
Hii inaweza ikawa ni mara ya kwanza kutokea Bongo kwa binti mdogo mwenye umri wa miaka 13 tu kukamilisha albamu yenye ngoma nane kupitia game ya muziki wa kizazi kipya, ndiyo maana nikatanguliza neno maajabu.

Namzungumzia Zena Salehe ambaye hivi sasa anafanya vyema na ngoma yake, ‘Wanawake wanaweza’, binti aliyeanza kusikika kunako sanaa ya muziki tangu alipokuwa na umri wa ‘kindagateni’ mpaka hivi juzi aliposema na safu hii kwamba tayari amekamilisha albamu yake ya kwanza na hivi sasa yupo kwenye mishemishe za uzinduzi.

Akiongea kwa kujiamini hivi karibuni huku akiwa amezungukwa na wacheza shoo wake wanne ambao pia ni watoto wenzie Zena alisema kwamba. “Natarajia kufanya uzinduzi mwezi Machi, mwaka huu katika sehemu ambayo nitaitaja baadae nikifanikiwa kupata wadhamini”.
***************************************************************************


Sister P (mwenye rasta)
2009 Sister P abaki kuwa shabiki?

Ndani ya mwaka huu mpya wa 2009, ‘Hot Corner’ inakujia kivingine kabisa, tofauti na ilivyokuwa mwaka jana, ambapo ilikuwa inakutana na mastaa mbalimbali wa Bongo na kupiga nao stori huku ikiwagonga maswali ya nguvu na kukushushia wewe msomaji.

Mwaka huu ‘Hot Corner’ itakuwa karibu zaidi na wewe msomaji, itaanzisha mada mpya kuhusiana na mastaa mbalimbali wa Kibongo, kisha wewe unapata fulsa ya kuchangia kadri uwezavyo ikiwa ni njia mojawapo ya kuiinua na kuipandisha zaidi sanaa yetu ili iende kunako levo za kimataifa zaidi.

Kwa kuanza leo, tunacheki na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Happy Thadei Pella a.k.a Sister P ambaye aliwahi kufanya vizuri na kazi kibao siku za nyuma kama ‘Anakuja’, Achana nao na nyingine kabla ya kupotea na kuibuka tena 2007 na ngoma yenye jina la ‘Moja kwa zote’ akiwashirikisha mabinti wa ‘Unique Dadaz’, kazi ambayo ilisikika kwa muda kisha ikatiwa kapuni.
Mwishoni mwa mwaka jana, Sister P alitoka kivingine kabisa na ngoma mpya aliyomshirikisha Mh. Temba wa TMK Family. Yaani badala ya kuchana (Hip Hop) kama alivyofanya wakati anaanza game akaamua kubadilika kwa kuimba, wimbo huo ulisikika mara chache tu na kupotea ghafla kama upepo bila kujua kitu gani kimetokea.

Ishu inakuja kwako wewe msomaji. Je, Sister P abaki kuwa shabiki kama alivyowahi kusema Afande Sele kwenye ‘Mtazamo’ au aendelee kuwepo kwenye game. Na kama ataendelea kuwepo, afanye nini ili afike mbali zaidi? Maoni yako wewe msomaji ndiyo yatamsaidia staa huyo wa zamani kuchagua moja au kubadilika katika game ya muziki. Tuandikie ujumbe mfupi kupitia simu namba 0715-110 173. Maoni yatachapishwa ndani ya safu hii wiki ijayo.

Compled by mc george

No comments: