Pages

Thursday, August 2, 2007

HII NI LAANA TUPU !

Na Mwandishi Wetu

Hii sasa ni laana tupu! Akina mama ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja hivi karibuni walitoa kali ya mwaka baada ya kupandwa na mdadi wa muziki na kufikia hatua ya kuvua nguo hadharani.

Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita mchana kweupe katika maeneo ya Manzese Tip Top, jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na sherehe ya kumtoa nje mtoto aliyekuwa akitimiza siku arobani.

Chanzo chetu cha habari kilichokuwa katika eneo la tukio kilishuhudia akina mama hao wakipanda jukwaani kushindana kukata viuno huku wengine wakishindwa kuzuia mizuka yao na kujikuta ‘wakichojoa’ nguo na kubaki uchi wa binadamu.

Kufuatia tukio hilo, baadhi ya wananchi hasa wenye heshima zao waliohudhuria sherehe hizo, walilazimika kuziba nyuso zao na wengine kuondoka eneo hilo kukwepa aibu.

“Hii ni hatari, yaani mwanamke na akili zake anafikia hatua ya kuvua nguo mbele ya kadamnasi bila hata chembe ya aibu, nadhani kuna kila sababu ya sherehe kama hizi kupigwa stop,” alisema Bi. Aisha Shabani mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa, sherehe hizo ambazo wanawake hupanda juu ya meza na kukata mauno huku wakionesha sehemu zao nyeti (Kusasambua) ni miongoni mwa mambo yanayochangia kumomonyoka kwa maadili ya nchi yetu.

“Wewe fikiria mwanamke anavua nguo huku watoto wadogo wakishuhudia, unatarajia kizazi cha baadaye kitakuwaje? Mbaya zaidi sasa watoto hao wanashangilia na kuona ni sawa, kwa kweli inaudhi,”alisema mama huyo kwa masikitiko.

Vitendo vya wanawake kuvua nguo wakipandwa na midadi katika sherehe za kutoa mwali, kicheni pati na nyingine za namna hiyo, hasa kwa baadhi ya makabila, vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara hali inayoonesha kuwa, vichwa vya wengi wao vimetawaliwa na ulimbukeni.

Hata hivyo Amani linaiomba serikali kuhakikisha kuwa, sherehe kama hizo ambazo kwa namna moja ama nyingine zinakwenda kinyume na maadili ya kitanzania zinadhibitiwa.



Joti wa Ze Commedy apigwa stop

Kumezuka tafrani kubwa baina ya wazazi na watoto wanaoiga utukutu na vituko vya mwigizaji Lucas Mhuvile ‘Joti’ kiasi cha kufikia hatua ya kumpiga stop mchekeshaji huyo asiharibu tabia za watoto.

Stop hiyo ya wazazi ni mwendelezo wa ile ya wazanzibari ambao nao walimjia juu hivi karibuni msanii huyo kufuatia maneno yake ya mdebwedo na kubonyeza kizenji ambayo yalitafsiriwa kuwakejeli watu wa visiwani.

Wanzazibari hao walieleza kuwa, jinsi msanii huyo anavyoyatumia maneno hayo yanawafanya baadhi ya watu kuamini kuwa wao ni legelege.

“Sisi tunamuomba Joti aache kutunga na kutumia maneno ambayo kwa namna moja ama nyingine yanawadhalilisha baadhi ya watu na akiendelea na tabia yake hiyo, kwa kweli tutamtolea uvivu,” alisikika kijana mmoja mwenye asili ya Zanzibar akisema.

Aidha Amani limeshuhudia wazazi kadhaa, jijini Dar es Salaam, wakiwacharaza bakora watoto wao baada ya kuwaona wakiigiza miondoko ya mchekeshaji huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini.

“Nimemtandika (fimbo) kwa sababu hana adabu, nilimtuma maji, eti anatembea kijoti joti, unajua huyo Joti anatuharibia watoto,” alisema mama Jackson Mkazi wa Sinza, Dar es Salaam.

Kundi la sanaa la Ze Commedy linalorusha kazi zake kupitia kituo cha East African Television, linaundwa na wasanii kibao akiwemo Joti, Mpoki, Masanja, Macregan na Wakuvwanga.


2 comments:

  1. Hawa jamaa wa Comedy wametoa video? Ingekuwa vizuri kama wanazo hata sisi tulio nje ya nchi tuzione.

    ReplyDelete
  2. Mr. Ebby!
    Hivi Watanzania huwa hawaangalii tv za nchi nyingine
    ili wajue the real definition of "comedy" maana people
    are taking this as a serious matter while in a real
    sense it is an entertainment, hapa USA comedians, they
    make fun of their own president, and no body take it
    serious. Kilichonishangaza ni pale MBUNGE mzima
    anasema eti kipindi kinawadhalilisha
    wazanzibari!!!!sijui anataka kujua maana ya sijui
    kubonyeza kizenji na sijui nini neno lingine, hivi are
    these members of Parliament really serious about what
    they are doing over there??? to me this sounds so
    stupid and they probably got nothing to discuss about,
    and I read in your article onetime you wrote kuwa kuna
    baadhi ya wabunge walikuwa wanaongea ni jinsi gani
    watampata RAY C simply because shes fine!!! ni upuuzi
    mtupu kwenye bunge.Hata kama wapo nje ya bunge, i
    think they need to use that particular time to discuss
    some important matters that brought them over there.

    Nikirudi kwenye mada yangu, Mi nadhani kama wazazi
    wanaona huo mchezo unawaathiri watoto wao, basi ni
    njia mbili za kufanya, either kipindi hicho kiwe
    either kinarushwa usiku pengine around saa nne usiku
    when kids are sleep, au they need to have what we call
    " parental guide control" sijui kama hii system ipo
    uko, unakuwa una set password for some of the channels
    that you don't need your kids to watch from your
    remote.

    Je wewe una usemi gani regarding this matter? correct
    me if im wrong hommie. Halafu pengine ungefikiria kuwa
    na sehemu ya watu kuweka maoni yao, i think ingesaidia
    kidogo hahahaaahahaahaaaa aah kuna mambo yanaudhi sana
    bwana!!

    Hans.

    ReplyDelete