Pages

Sunday, January 2, 2011

RIHANA ALIPWA MILIONI 356 KUUKARIBISHA MWAKA MPYA

Rihani akiukaribisha mwaka 2011....three! twoo! Onee!!
Rihanna....katika vazi la kiheshima zaidi
Maisha ya wasanii wetu na wale wa majuu yana tofauti kubwa kama ardhi na mbingu na sidhani kama yatakuja kufanana mpaka mwisho wa ulimwengu huu! Wakati msanii hapa bongo akilipwa milioni 1.5 kwa shoo moja anaonekana ni msanii ghali, mwanadada Rihana amelipwa milioni 356 kwa ajili ya kuhudhuria katika pati moja ya saa moja na kuhesabu zile sekunde za kuukaribisha mwaka mpya (zile Three, twooo, Onee)!

Mpango mzima ulifanyika Pure Nightclub, uliyopo Sin City Venue, katika jiji la maraha na kamari za makasino, Las Vegas, Marekani! Baada ya hapo, aliendelea na safari zake za kwenda kwenye shoo zingine. Utajiuliza akipiga shoo za hivyo tu 3 kwa mwaka, ana shida gani hata asipotoa albamu?

No comments:

Post a Comment