Tuesday, July 7, 2009

Unajua umuhimu wa chungwa kwa afya yako?

YOU ARE WHAT YOU EAT
Msimu wa machungwa umewadia na kama mnavyofahamu, unapowadia msimu huu machungwa huzagaa kila mahali na kila kona ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa idadi hiyo ya machungwa na bei huwa nafuu kufikia hadi shilingi 20.

Lakini siyo ajabu pia kuona msimu huu unakwisha bila mtu kula chungwa hata moja. Hii inatokana na kasumba ya binadamu tangu zamani ya kutothamini matunda. Kama wewe ni miongoni mwa watu wenye tabia hiyo, fikiria mara mbili kwa sababu chungwa lina faida nyingi mwilini, zikiwemo zifuatazo:

Chungwa lina kirutubisho kiitwachwo ‘Beta Carotene’ ambacho kina umuhimu mkubwa kiafya kwa sababu hulinda chembechembe hai za mwili dhidi ya maradhi.

Chungwa lina madini aina ya ‘Calcium’, ambayo kila mtu anajua kwamba ni muhimu kwa ustawi wa mifupa na meno, hasa kwa watoto wa shule.

Chungwa lina ‘Folic Acid’ ambayo huhitajika na ubongo ili uweze kufanyakazi yake vizuri ya kufikiri, kutunza kumbukumbu na kuchanganua mambo kwa haraka.

Chungwa husaidia watu wenye matatizo ya shinikizo la damu kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha ‘Magnesium’ ambacho hudhibiti mfumo wa damu.

Chungwa litaulinda mfumo wako wa hewa na kuweka seli za mwili kwenye uwiano unaotakiwa kutokana na kuwa na kiwango kizuri cha madini aina ya ‘Potassium’.

Chungwa huharakisha usagwaji wa chakula na hivyo kupata nguvu mwilini kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho ‘Thiamin’ kinachohitajika kwa kazi hiyo.

Chungwa hutoa nafuu kwa magonjwa ya Pumu, Kikohozi, Kifua Kikuu, Nimonia, baridi yabisi na huzuia ugonjwa wa mawe kwenye figo. Vile vile huondoa hamu ya kunywa pombe kwa wale wanaotaka kuacha unywaji wa pombe na husaidia sana kukata makamasi kwa wale wenye mafua.

Maganda ya chungwa nayo yana kiwango kikubwa cha Vitamin C kama lilivyo chungwa lenyewe. Hivyo ni vizuri kama utaweza kula chungwa na maganda yake au angalau pamoja na nyama zake ili upate virutubisho vyote.

Kama ulikuwa si mlaji wa machungwa mpaka uambiwe na daktari, sasa umefika wakati wa kutambua umuhimu wa chungwa na kuanza kulichangamkia kama vile huna akili nzuri, kwa faida ya afya yako ya sasa na ya baadae.

No comments: