Wednesday, March 4, 2015

OLOLOSOKWAN WAFURAHIA UJIO WA KIJIJI CHA DIGITALI ENEO LAO

DSC_0003
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya Tehama, Al Amin Yusuph akiwasilisha mrejesho wa kazi ya kikundi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.(Picha na zote Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa kijiji cha Ololosokwan wamesema kwamba ujio wa kijiji cha digitali katika kijiji chao ni neema kwao kwani kitawasaidia kukabiliana na changamoto kubwa za maisha zinazowakabili.
Kauli hiyo wameitoa mwishoni mwa wiki wakati wa kuhitimisha warsha ya siku saba ya kuangalia fursa na changamoto zitakazoambatana na mradi huo wa miaka mitatu unaodhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake waliohudhuria warsha hiyo ambapo wataalamu mbalimbali wanaohusika na mradi huo walikutana kujadili changamoto na namna ya kukabiliana nazo, Salangat Mako, alisema kwamba tatizo la miundombinu, Afya na Elimu wanaamini litakabiliwa na mradi huo.
Alisema kuna shida kubwa ya elimu kutokana na mazingira yaliyopo ambapo wanafunzi wanalazimika kutembea kilomita 14 kwenda na kurudi shule hali inayodhoofisha ari ya kujifunza.
DSC_0044
Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akitoa mrejesho wa kilichojadiliwa na kikundi chake.
Aidha alisema kwamba kuna changamoto katika zahanati yao yenye wauguzi wawili huku hospitali ya wilaya ikiwa kiasi cha kilomita 50 hali inayowafanya watu wengi kutegemea mitishamba katika matibabu mbalimbali pamoja na wanawake kusaidiwa uzazi na wakunga wa jadi.
Alisema kuwepo kwa mradi huo kutasaidia wanafunzi kuweza kujisomea kwa kutumia mfumo wa mtandao wa intaneti na hivyo kuwa katika nafasi ya kuelimika vyema kutambua wajibu wao na fursa zilizopo zinazowazunguka kwa kuwa hifadhini.
Aidha kuwepo kwa kiliniki ya mtandao kutaongeza ufanisi wa zahanati iliyopo pamoja na kuipa mkono katika tiba na kuondoa watu kutegemea tiba za asili.
Akizungumzia fursa za kiuchumi alisema ni matarajio yao kwamba kuwepo kwa kijiji hicho na utamaduni wake, kutawezesha kutumia vyema fursa za kitalii ili kukua kiuchumi kwa kujua mipango inayostahili katika kuendeleza utamaduni kwa jicho la kibiashara zaidi.
DSC_0036
Mratibu wa shirika la IrikRAMAT Foundation, Salangat Mako akitoa mrejesho wa suluhu za changamoto mbalimbali za kikundi cha uchumi na utamaduni wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya wiki moja.
Naye Mganga mfawidhi wa zahanati ya Ololosokwan Obeid Laizer ambaye yupo katika kijiji hicho kwa miaka 15 amesema ana matumaini makubwa na mradi huo kwa kuwa mchanyato wake unaonekana kujali zaidi sosholojia za watu na afya zao hasa kwa kuwa na kliniki inayotembea na tiba kwa intaneti itakayomuwezesha kuwasiliana na madaktari wenzake ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya afya.
Alisema kwamba kijiji hicho kina magonjwa mengi japokuwa makubwa ni nyumonia, ukosefu wa damu, magonjwa ya zinaa, majereha ya wanyama kutokana na kuchunga mbugani na ugonjwa wa kuhara damu.
Alisema uwapo wa maabara utawasaidia kupata uhakika wa tiba kuliko sasa ambako wanafanya kwa kukisia zaidi.
DSC_0018
Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya afya kutoka UNESCO, Bw. Mathias Herman akiwasilisha mrejesho wa kikundi kazi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Naye Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro Beneth Bwikizo amesema kwamba mradi huo utaleta mabadiliko makubwa kwa wanakijiji hapo kutokana na shughuli nyingi za hapo kuhusanishwa na mradi huo.
Alisema mradi huo ambao unaangalia zaidi kukabili utamaduni unaokwamisha maendeleo kwa kutoa elimu na kuiunganisha na dunia nyingine kwa mawasiliano unaonekana utafanya maisha ya wakazi wa hapo kuboreka.
Alisema mradi huo wa kwanza nchini Tanzania na watatu bara la Afrika umempa hamasa kubwa baada ya kuona unaangalia changamoto zilizopo Ololosokwan ambazo ni za miundombinu katika elimu, afya na uchumi na kuzifanyia kazi.
DSC_0051
Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro, Beneth Bwikizo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya ujumbe wa kijijini cha Ololosokwan uliohudhuria warsha hiyo ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
DSC_0054
Afisa Miradi msaidizi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko (kushoto) na Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Teresia Irafay wakinakili yanayojiri wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji cha kidigital (Unesco - Samsung digital village) katika kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0057
Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la IrikRAMAT linalomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maoni yake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi kijiji cha Kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Warsha hiyo ya wiki iliandaliwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini.
DSC_0066
Pichani jii na chini ni wadau mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi waliohudhuria warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
DSC_0034
DSC_0008
Kutoka kushoto ni Mathias Herman wa UNESCO, Mkurugenzi wa elimu ya msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Sarah Mlaki pamoja na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ololosokwan, Emmanuel Madeje.
DSC_0064
Mkurugenzi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akionesha kwa mifano baadhi ya bidhaa za nje zikivyokuwa na ubora kwenye vifungashio wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha digitali (Unesco-Samsung digital village) kwa wakazi wa kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0118
Mkurugenzi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisikiliza baadhi ya maboresho ya changamoto zilizojadiliwa na kikundi kazi cha sekta ya elimu na wadau mbalimbali wa elimu.
DSC_0070
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues akitoa maboresho ya kazi za vikundi vilivyokuwa vikijadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zilizopo katika kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali.
DSC_0070
Picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo ya wiki moja iliyomaziki mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Read More

Monday, March 2, 2015

NYALANDU AWAAGA WAFANYABIASHARA

Waziri wa Utalii na Maliasili Razalo Nyarandu akitoa nasaha za kuwaaga wafanyabiashara wa Tanzaia wanaoenda Berlin Ujerumani
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akitoa nasaha za kuwaaga wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda Berlin, Ujerumani kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB kuanzia Machi 4-8 mwaka huu.(Picha zote na modewjiblog)
Na Andrew Chale wa modewji blog
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewataka wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB, mjini Berlin, Ujerumani Machi 4 hadi 8, mwaka huu, kubeba uzalendo na kuitangaza Tanzania hususani vivutio vya Utalii na utajiri wa maliasili ili kuvutia wawekezaji.
Nyalandu aliyasema hayo usiku wa Februari 27, wakati wa halfa fupi ya kuwaaga wafanyabiashara hao ambapo alisema kuwa, kwenda kwao huko kushiriki maonyesho hayo makubwa kabisa duniani, ni fursa kama Tanzania kupata kujitangaza zaidi na kuvutia wawekezaji.
DSC_0151
Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
“Leo hii tunawaaga hapa. Nyie ndio Tanzania hivyo mnapokuwa huko mjue mmebeba watanzania wengine zaidi ya Milioni 40. Ni wakati wa kuvitangaza vivutio na uzuri wa Tanzania na ilikuongeza soko letu la Utalii na uwekezaji” alieleza Nyalandu.
Pia aliongeza kuwa, Wizara yake ya Utalii itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linafikia malengo yake yaliyokusudiwa ikiwemo kujitangaza ndani na nje ikiwemo kuendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na Uharamia dhidi ya meno ya Tembo, wanyama na nyara za serikali kiwemo pembe za ndovu.
Maofisa wa T.T.B, Devota Mdachi (kushoto) akiwa na Dorothy Masawe (Kulia) wa wizara ya Utalii, wakifuatilia jambo kwa makini wakati wa halfa hiyo
Afisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi (kushoto) akiwa na Dorothy Masawe (Kulia) kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakifuatilia jambo kwa makini wakati wa halfa hiyo.
DSC_0131
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akibdilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa.
DSC_0202
Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels (kulia), Afisa wa Ubalozi wa Ujerumani kitengo cha habari, John Meirikion (kushoto) wakiteta jambo na mmoja wa wageni waalikwa.
CEO wa DHL ukanda wa  Eastern Africa, Pramod Bagalwadi akisalimiana na Waziri wa Utalii, Razalo Nyalandu
CEO wa DHL ukanda wa Eastern Africa, Pramod Bagalwadi, akisalimiana na Waziri Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu kwenye hafla hiyo.
DSC_0103
Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wafanyabiashara katika sekta utalii wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.
DSC_0237
DSC_0231
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na Afisa wa Ubalozi wa Ujerumani kitengo cha habari, John Meirikion wakati wa hafla hiyo.
DSC_0222
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na wafanyabiashara akiwemo Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Bw. Florenso Kirambata ( wa pili kushoto).
DSC_0101
Mkurugenzi wa Biashara wa Flight Link, Bw. Ibrahim Bukenya akiwa na Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels wakati wa hafla hiyo.
DSC_0145
Wadau wakifurahi jambo.
Read More

LEO NI SIKU YA KUZALIWA YA MDAU OTHMAN MICHUZI

Napenda Kuchukua Fursa hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma na Mwenye Kurehemu kwa kunijaalia Uhai na afya njema hadi kufikia siku hii ya leo,ambapo ninayo furaha kubwa sana kwa kuongeza namba moja katika umri wangu,kwani bila yeye hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika.

pia nitakuwa ni mchoyo wa Fadhila iwapo sitotoa shukrani za kipekee kwa ndugu zangu woote (wakiwemo wazazi wangu wawili,Ankal Issa Michuzi,Ahmad Michuzi,Karim Michuzi,Ramadhan Michuzi,Ismail Michuzi,Ankal Macheka,Ai Michuzi,Zahra,Tatu,Sellah,Bobby,Noreen,Adam,Saleh na wengine wengi ambao sijawataja majina yenu hapa ila moyoni ninayo,na bila kumsahau mtarajiwa wangu wa ubani bi. Farida) kwa kuwa pamoja nami katika makuzi yaliyo mema hadi leo hii kufikia hapa nilipo.


Tanzania Bloggers Network (TBN) pia naomba mpokee shukrani zangu za dhati kwa kuwa pamoja nami kama mwanachama hai siku zote na bila kunitupa,pia nichukue fursa hii kutoa pongezi kwa uongozi wa TBN na wanachama wenzangu kwa kuungana pamoja katika tafrija ya kihistoria  iliyotukutanisha pamoja,kiukweli ile ilikuwa ni siku muhimu sana kwetu kwa kutukutanisha pamoja na kufahamiana zaidi,ile ilikuwa ni bonge la heko kwani kuna wengine walitamani kuwa na umoja kama wetu lakini hawafanikiwi.

pia nawashukuru marafiki,jamaa zangu pamoja na Wadau woote popote pale mlipo ambao kwa namna moja ama nyingine mmekuwa ni mchango mkubwa katika maisha yangu na kunifanya kila siku niwe bize kuhakikisha libeneke halilali mpaka kieleweke.Nawashukuruni sana tena sana na Mungu awabariki nyoote. Nawapenda sana wote na tuko pamoja sana.


TEMBELEA BLOG YA MTAA KWA MTAA Inayomilikiwa na Besdei boy Othman Michuzi kwa kufuata link hii.
http://othmanmichuzi.blogspot.com
 
Hapa ni dole tupi,nikiwa na wadau wangu Anganile na Hellen Kiwia.
Read More

Mazungumzo na Mhe Samuel Sitta (Pt I).......KATIBA

Karibu katika sehemu hii ya kwanza kati ya mbili za mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.
Aliketi nasi kuzungumzia zaidi suala hili la Katiba hii pendekezwa, na mchakato mzima wa kuipata
Karibu
Read More

Wednesday, February 25, 2015

SIMU ZA OBI MOBILES ZAINGIA TANZANIA

S550-Crane-1
Simu ya Obi aina ya S550-Crane.
Na Mwandishi Wetu
MWANZILISHI mwenza wa kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya mawasiliano ya Obi Mobiles, yenye makao makuu yake Singapore, John Sculley amesema ujio wa kampuni hiyo nchini Tanzania, utaongeza wigo wa utumiaji wa tehama na hasa matumizi ya zana za kisasa za mawasiliano.
Obi Mobile inatumia teknolojia iliyobuniwa mjini Toronto, Canada na kampuni ya Inflexionpoint.
John Sculley, ambaye alishawahi kuwa ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Apple amesema teknolojia hiyo mpya ambayo ilizinduliwa India na Mashariki ya Kati mwaka 2014 imelenga kuwanufaisha vijana ambao ndio watumiaji wa kubwa wa simu za kisasa.
Amesema kwa kuingiza bidhaa za Obi nchini Tanzania wanatarajia kuwawezesha vijana kuwa na simu ambazo zinawatumikia wao kwa maarifa na umaridadi zaidi.
S550-Hornbill-2
S550-Hornbill.
“Simu hizi zimepokewa vyema zilikozinduliwa na tunararajia Tanzania nazo watazipokea kwa kasi hiyo hiyo” alisema Sculley .
Kwa mujibu wa ofisa huyo, simu za Mobile nchini Tanzania zinauzwa kati ya sh 50,000 na bei ya juu ni 350,000.
Alizitaja aina hizo za simu kuwa ni Hornbill S551; Falcon S451; Crane S550; Wolverine S501; Fox S453 ; Racoon S401 na Power GO F240 simu ambayo ina betri yenye uwezo wa 2,800mAH na yenye uwezo wa kuchaji simu nyingine.
Amesema watu wa Obi Mobiles wanaamini kwamba teknolojia ni kwa ajili ya watu wote na ndio maana mauzo ya teknolojia zao ni rahisi kwa ajili ya watu wote.
Alisema kwa kuwa na vifaa vya teknolojia ya Obi, vijana watakuwa na nafasi ya kutumia fursa zilizopo za kiuchumi na kijamii.
S453-Fox-1
S453-Fox
Sculley amesema kwa muono wake teknolojia haitakiwi kuwa ngumu kuitumia wala kutengeneza changamoto kwa watumiaji wake kwa kuiwekea vikwazo.
Teknolojia za Obi Mobile zinazotumia mfumo wa Android ni za daraja la juu na wkamba simu zote za Obi zilizoingizwa nchini zina uwezo wa kuwa na intaneti.
Kampuni hiyo inatarajia kuzindua simu hizo nchini Tanzania mwezi ujao .
Akizungumzia mkakati wa kampuni hiyo kwa bara la Afrika , Mkurugenzi Mtendaji wa Obi Mobile MENA, Amit Rupchandani: “Walaji wengi wanataka kujiondoa katika simu za kawaida kwenda katika simu za kisasa. Hata hivyo,gharama za uwekezaji katika teknolojia ya kisasa ni kikwazo kikubwa kwa watu wengi.”
Obi Mobiles, wamesema kwamba kwa kuelewa hilo, wamewezesha kuwa na simu zenye uwezo mkubwa na kwa bei nafuu ili kufikia kila kundi katika bara la Afrika.
Simu hizi ambazo vijana watazipenda zimeelezwa kutengenezwa kumudu maisha yao na kuwapendezesha.
Read More

KIJANA WA KITANZANIA AUNDA REDIO STESHENI - SHUJAAZ

Shujaaz Banner
DJ Tee (19) ni kijana mwenye ndoto kubwa katika maisha yake. Baada ya kuona mahangaiko ya vijana kuelekea kwenye mafanikio, wengi wakiwa wamemaliza shule na vyuo bila kupata kazi, ameamua kuunda redio stesheni ghetoni kwake aliyoipa jina la Shujaaz, ili aweze kushea ideas na vijana wote nchini Tanzania kuhusu mbinu mbalimbali za kuingiza pesa, kuwapa stori za vijana wanaochakarika katika maisha yao pamoja na kuwaburudisha.
"Nimeamua kuiita Shujaaz kwa sababu, naamini kuwa kijana ambaye anajituma na kuweka mfano bora kwenye jamii ni shujaa". Alisema DJ Tee. "Ndoto zangu zinakaribia kuwa kweli".
Story ya kijana huyu inapatikana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kupitia kijarida cha Shujaaz, kitakachokuwa kinasambazwa kupitia gazeti la Mwanaspoti, kuanzia JUMAMOSI HII ya tarehe 28. Kwenye kijarida hicho, utapata ideas mbali mbali ambazo vijana wanaweza kuzifuata na kujiingizia kipato. Pia, kutakuwa na stori za vijana wengine kama Pendo, Semeni na Pepe ambao ni mashabiki wakubwa wa DJ Tee na redio show yake ya Shujaaz.
DJ Tee akiwa studio
DJ Tee akiwa studio.
Kijana huyu ameamua kujiita DJ Tee ili asijulikane na watu wake wa karibu, kwa kuwa ana-hack airwaves za redio stesheni ili aweze kusikika. Sikiliza redio stesheni uipendayo kuanzia wiki ijayo, huwezi jua, inawezekana DJ Tee akawa hewani!
Wewe pia USIKOSE kuwa sehemu ya mafanikio na harakati za kijana huyu kwa kujiunga naye. Pata nakala yako ya Shujaaz kuanzia Jumamosi hii (28/02/2015) kupitia gazeti la Mwanaspoti. Pia, jiunge naye kwenye ukurasa wake wa Facebook kwa jina DJTee255 ili upige naye story na wewe uweze kushea idea zako za hustle. Unaweza pia ukampata Instagram na Twitter kwa jina @djtee255
Studio
Studio.
Read More

Tuesday, February 24, 2015

Picha 54 za Show Nzima ya Yamoto Band Ndani ya Royal Regency UK London Ziko hapa (2)

Vijana wa Yamoto Band jumamosi iliyopita Walipiga Bonge moja la Show huko UK London katika Ukumbi wa Royal Regency na kuhudhuliwa na watu kibao wanaoishi huko, Hizi ni picha za matukio katika Show Hiyo.
Read More
© MRISHO'S BLOG All rights reserved