Wednesday, July 14, 2010

UNAJUA MAJI NI DAWA?


Maji ni dawa na ni kinga ya maradhi mengi. Kila mtu angekuwa anakunywa maji kama inavyotakiwa, kusingekuwa na maradhi kabisa. Huo ni ukweli wa tangu enzi za mababu zetu na umeshafanyiwa utafiti wa kutosha na kuthibitishwa na wanasayansi wengi duniani.

Ili upate faida ya maji kama tiba, ni lazima unywe maji mengi asubuhi kabla ya kuchomoza kwa jua na kabla hujapiga mswaki wala kula kitu chochote. Ujazo unaotakiwa kunywa ni kuanzia lita 1 na robo mpaka lita 1 na nusu, maji safi na salama na yasiwe ya baridi.

Aidha, ukisha kunywa maji hayo usile wala usinywe kitu kingine hadi baada ya dakika 45 au saa moja, baada ya kupita muda huo, unaruhusiwa kupiga mswaki na kunywa au kula chochote utakacho na kinachokubalika kiafya (rejea makala zetu zilizopita).

Kitu kingine cha kuzingatia ni kwamba baada ya kunywa hayo maji, ni lazima uyanywe ndani ya kipindi cha dakika 5 au 10 tu na usifanye mazoezi hadi baada ya nusu saa. Wakati unafuata tiba hii kwa siku nzima, basi sharti liwe ukisha kula chakula, unywe maji kila baada ya saa 2 na ukae muda huo kabla hujala kitu kingine.

Hata mtu asiye na maradhi yoyote, anashauriwa kunywa maji kwa mtindo huu ili kujikinga na maradhi katika maisha yake yote. Kwa wale wasiokuwa na uwezo wa kunywa kiasi hicho kwa siku zao za mwanzo, wanashauriwa kuanza na kiasi kidogo cha angalau glasi 2 na hatimaye wafikie 4. Usiogope wala usifikirie kutapika wakati ukinywa maji hayo, maji hayatapishi, bali dhana yako ndiyo inayoweza kukufaya utapike!

Orodha ya magonjwa yanayoaminika kutibika, kuzuilika au kudhibitiwa kwa tiba hii ya maji ni pamoja na: Kisukari, shinikizo la damu, maumivu kwenye viungo (Joints Pain), matatizo ya moyo na kuzimia, homa ya uti wa mgongo (Meningitis), matatizo ya mkojo, kansa ya kizazi (Uterus Cancer), kikundu (hemorrhoid), matatizo ya tumbo, kuharisha, nyongo, kikohozi na chunusi.

Magonjwa mengine ni pamoja na kupooza mwili, athma, asidi tumboni, homa, kuumwa kichwa, upungufu wa damu (anemia), utipwatipwa (Obesity), kifua kikuu, magonjwa ya ini, matatizo ya hedhi, mataizo ya kukosa choo na magonjwa mengine mengi!

Iwapo watu wangeachana na unywaji wa pombe na soda, badala yake wakawa wanakunywa maji safi na salama kwa wingi, watafiti wa tiba ya maji wanaamini kwamba idadi ya wagonjwa hospitalini ingepungua kwa kiasi kikubwa sana duniani.

TIBA HII YA MAJI INAFANYA VIPI KAZI MWILINI?
MOSI: Unapokunywa lita moja na robo ya maji ndani ya dakika 5 au 10, baada ya kufunga kwa usiku mzima kwa muda usiopungua saa 8 hadi 10, shinikizo la maji yanayopita kwenye utumbo mdogo, huamsha seli (cells) kwa haraka kuliko kawaida.

PILI: Kutokana na shinikizo hilo la maji la ghafla, masalia na vipande vipande vya vyakula ambavyo huganda kwenye kuta za utumbo mdogo, husombwa na maji hayo pamoja na gesi na vitu vingine ambavyo havikusagwa na kutupwa kwenye utumbo mpana tayari kutolewa kama uchafu. Hali hii huuacha utumbo mdogo ukiwa safi na kuzipa seli uhai mpya!
Itaendelea wiki ijayo....

4 comments:

Disminder orig baby said...

Wow wow wow!! hii ni habari njema sana kaka.

sasa kama mimi nimejiwekea utaratibu wa kutokunywa maji baridi, siku zote nakunywa maji moto.

1. Nikiamka asubuhi nichemshe maji yangu moto ninywe? lakini itachukua more than 10mns kwani inabidi yapoe poe kidogo ndiyo nakunywa.

2. Nikimaliza kula uwa nakunywa maji baada ya nusu saa ya moto hayo hayo. Je naweza kunywa maji moto ninapomaliza kula tu?

3. Kuna mtu kaniambia eti maji moto yanapanua utumbo ni kweli hii?

Ushauri wa kunywa maji moto nilippewa na doctor wa kichina baada ya kuwa nasumbuliwa na meno kwa muda mrefu sana. Aliniambia kama sitafuta ushauri wake nitatoa meno yote mdomoni kwani %kubwa yameharibika.

Ni kweli toka nifuate ushauri wake, siumwi na meno na pia imenisaidia katika mambo mengi sana.
mimi ni mnene lakini sina tumbo kubwa, sina chunusi na hata nilipofanyiwa upasuaji, sikukutwa na mafuta tumboni ukilinganisha na mwili wangu.

Mungu akubariki.

Mrisho's Photography said...

tweety,

kanuni ya kunywa maji baada ya nusu saa ukitoka kula inatumika kote, iwe maji baridi au ya uvugu. kimsingi maji ya uvugu (si ya moto per say) ndiyo mazuri kuliko ya baridi.....si kweli yanapanua utumbo bali navyojua mimi maji moto/uvugu huondoa mafuta kwenye utumbo na baridi huchangia kuganda kwa mafuta...upo hapo...ushahidi unao mwenywe...ulifanyiwa upasuaji lakini hukuwa na mafuta while ni mnene!!!!!!!

Unknown said...

Wow! that good news!
am starting today

Anonymous said...

kaka mrisho nashukuru sana na Allah akuzidishie, uzidi kutujuza zaidi na zaidi yale uliyojaliwa kuwa nayo Inshalah.

tweety.