Thursday, August 9, 2007

Mrembo auawa!


NA DOTTO MWAIBALE
Mhudumu wa Baa ya Salama Beach iliyopo Kiwalani Bombom jijini Dar es Salaam, Lightness Johnson (17), amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu shingoni na kijana mmoja aitwaye Good luck Saria nayedaiwa kuwa mpenzi wake kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mrembo huyo amekumbwa na mauti usiku wa kuamkia Agosti 7, mwaka huu majira ya saa 5.00 za usiku, wakati wateja wakiendelea kupata vinywaji katika baa hiyo.

Akiongea na Mwandishi Wetu mhudumu mmoja wa baa hiyo aliyeshuhudia tukio hilo aitwaye Amina Mbaraka alisema kuwa, siku hiyo akiwa na marehemu walifika kazini majira ya jioni.
Amina alisema walipowasili walianza kuwahudumia wateja wao huku wakitolewa vinywaji na Good luck Saria mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye alikuwa 'counter'.

Aliendelea kusema kuwa Good luck na Lightness walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa zaidi ya miezi miwili na wote walikuwa wafanyakazi wa baa hiyo.

Shuhuda huyo aliongeza kuwa, waliendelea kuwahudumia wateja waliofika katika baa hiyo hadi saa 8.30 usiku ambapo wengi wao waliondoka na kubakia wachache wakimalizia vinywaji vyao.

Amina alisema wakiwa wanawasubiri wateja wamalizie vinywaji vyao, Good luck alitoka 'counter' na kwenda kusimama nyuma ya kiti alichokuwa amekaa marehemu.

Shuhuda huyo aliongeza kuwa baada ya dakika kadhaa kupita, mtuhumiwa aliingia 'counter' kisha baadaye akatoka na kwenda kusimama eneo alilokuwa amesimama awali ndipo walimsipomkia Lightness akilalamika kuwa alichomwa kisu na Good luck.

Aidha aliongeza kuwa, mwanzo walifikiri aliwatania lakini waliamini baada ya kumuona amelala chini huku damu nyingi ikichuruzika sakafuni ndipo walimwita mmiliki wa baa hiyo, Respis Francis Mrosso.

Mmiliki huyo alitafuta gari kwa ajili ya kumpeleka majeruhi hospitalini, lakini kwa bahati mbaya alifariki njiani.

Shuhuda huyo aliongeza kuwa baada ya Good luck kufanya mauaji hayo, alitoroka na kwenda kusikojulikana ambapo mpaka sasa anasakwa na polisi.

Akizungumza na Ijumaa, mmiliki wa baa hiyo, Mrosso alisema kuwa, Good luck ni mwenyeji wa Old Moshi mkoani Kilimanjaro na kwamba alimpatia kazi baada ya kuletwa kwake na kijana mmoja wa kijijini kwao.

"Good luck aliletwa kwangu na kijana mmoja wa kijijini kwetu ambapo nilimpatia kazi, lakini baada ya muda wakawa na uhusiano wa mapenzi na marehemu, hivyo wakawa wanaishi pamoja," alisema Mrosso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Masindoki Masindoki amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kuahidi kufuatilia suala hilo kwa ukamilifu.


Mtanzania huyu kumponza Mengi
  • Ni mropokaji, anayeandika bila kufanya utafiti
Na Mwandishi Wetu
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Aberdeen, Scotland, Evarist Chahali huenda akamponza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, ambaye pia ni mmiliki wa gazeti la Kulikoni, kufuatia habari potofu aliyoiandika kwenye gazeti hilo dhidi ya gazeti la Risasi.

Kwa mujibu wa habari hiyo, mwandishi huyo ambaye ni Mtanzania anayedai kuchukua kozi ya Udaktari wa Falsafa (PhD) katika chuo hicho, aliandika makala ya kuyashutumu magazeti ya Udaku kuwa yanaandika habari feki na kutolea mfano gazeti la Risasi.

Katika makala yake ya Jumatano Agosti 8, mwaka huu, Chahali alidai kuwa habari zilizoandikwa kwenye gazeti la Risasi ambalo ni dada la hili, zilizoambatana na picha hazikuwa na ukweli wowote.

Chahali alitolea mfano wa habari iliyochapwa kwenye gazeti hilo la Julai 18-20 iliyokuwa na kichwa cha habari 'Warembo wa TZ wapiga picha za X tupu'.

Habari hizo ambazo chanzo chake ni mtandao, zilieleza kuwa wasichana hao ni Watanzania waliopiga picha wakiwa watupu kwa nia ya kutangaza biashara ya kuuza miili ambapo waliweka bayana mawasiliano yao.

Hata hivyo, Chahali alidai kuwa habari hiyo ni ya uongo (feki), kwani picha zilizotumika ni za nyota wa sinema za ngono (porn star) wa Marekani na si Watanzania.

Mwandishi huyo alieleza katika makala yake hiyo kuwa, aliamua kuandika hivyo baada ya kuambiwa na rafiki yake anayeishi Marekani.

Akiongea na gazeti hili, Meneja Mkuu wa Kampuni inayochapa gazeti hilo, Abdallah Mrisho, alisema kuwa amesikitishwa na makala ya gazeti la Kulikoni ambayo haikufanyiwa utafiti wa kutosha.

"Habari iliyoandikwa na gazeti la Risasi ni ya kweli, hatujawahi kuandika wala haturuhusu wahariri wetu kuandika habari za uongo ndani ya magazeti yetu, ila Chahali ameropoka.

"Kimsingi mwandishi wa makala hayo, (Chahali) ameonyesha udhaifu mkubwa kwa kuandika habari bila kufanya utafiti na kufikia uamuzi wa kushambulia gazeti letu bila kuwa na uhakika na alichokiandika", alisema Mrisho.

Mrisho aliendelea kusema ana wasiwasi hata na shahada alizonazo Chahali, kwani mtu mwenye elimu kama yake hawezi kuandika habari za kuambiwa bila kufanyia utafiti, hivyo kuupotosha umma na anaweza kumponza mmiliki wa kampuni inayochapisha gazeti hilo, ambaye anaheshimika sana.

"Chahali hakupaswa kutoa shutuma nzito kama zile kwa maneno ambayo hakuyafanyia uchunguzi na kuchapa kwenye gazeti, kwani anaweza kumponza mmiliki wa kampuni hiyo tunayemuheshimu, anapaswa kuona aibu (shame on him)," alisema Mrisho.

Kuthibitisha kuwa habari iliyoandikwa ni ya kweli, wahariri wa gazeti la Risasi wamelazimika kutaja anuani ya tovuti ambako wasichana hao wanapatikana, ili umma kwa ujumla uelewe nani mkweli kati ya Chahali na gazeti la Risasi, ingawa haikuwa kusudio lao kufanya hivyo.

Anuani hiyo ni http://swallowmyjuice.hi5.com ambako picha zilizotumika, mahali wanakoishi na utambulisho wa wasichana hao vinapatikana.

Aidha, kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari cha kuaminika kilichoko ndani ya chuo cha Aberdeen, Chahali ni miongoni mwa wanafunzi wasiofanya vizuri sana katika masomo yao.

"Chahali sio miongoni mwa wanafunzi wanaofanya vizuri sana chuoni," kilisema chanzo hicho.

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma kozi moja na Chahali katika chuo hicho ni pamoja na Timofei Agarin, Gordon G. Davidson, Joyleve Elliat, Anna Gustavon, Jeremy Lamoreaux, Giseong lee, Yang Lia, Khristus Vassis, Lortraine Whitty na Anna Zawak.

Mrisho alimtahadharisha mhariri wa gazeti hilo kuwa asipokuwa makini na waandishi wanaoandika makala zao kwa chuki binafsi kama Chahali, wanaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa.

Akiongea na mwandishi wetu kwa simu juzi, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya This Day na Kulikoni, Evarist Mwitumba alisema kuwa hana habari kuhusu makala hayo.

"Nipigieni kesho asubuhi, kwa sasa niko barabarani naendesha gari na sijasoma gazeti lililoandika habari hiyo," alisema Mwitumba.

17 comments:

Anonymous said...

Mrisho

Mimi sio mtaalam wa masuala ya mtandao, lakini hakuna mtandao ambao unavurugwa sana na watumiaji kama hi5.com. Kama hichi ndo chanzo chako pekee cha hiyo habari, nasikitika kuwa nitakuwa upande wa chahali kukusuta kuwa picha zile ni za Wamarekani na kuwa nyie mmedanganya watanzania.

Tupe mitandao yenye URL zinazoeleweka sio hi5.com. Mtu anaweza kuweka picha ya mtu yeyote kwenye hi5.com. Na kama nakumbuka kuhusu maelezo ya ile habari, ulisema kuwa kuna namba za simu, eno wanakopatikana hao wadada na mambo kama hayo. Lakini kwa hi5.com ambayo ni mtandao wa marafiki tu, bado hajani conivnce kuwa ulikuwa na source nzuri ya habari.

Najua unaweza kuamua kutotundika hii comment, lakini ujumbe utakuwa umeupata.

Asante

Anonymous said...

Nyote mnahitaji kuwa makini.Mbona hakuna cha ajabu katika hizo picha mnazozizungumzia?Bikini ni nguo za kawaida tu jamani..tuache ushamba na ushambenga watanzania.

Anonymous said...

Nimeangalia picha zile pale Hi5, nina wasiwasi kuwa naweza kukubaliana na chahali kuwa wale ni pornstar wa kimarekani. mambo matatu yanawezekana:

(a)wasichana wa kitanzania wametumia picha za mastar hao.

(b) mastar wameamua kudanganya kuwa wako Tanzania.

(c) mastar hao ni watanzania.

Picha hizo hazikupigwa katika mazingira ya Tanzania. Baadaye nitakutafutia picha nyingine za yule anayejiita Melanie ndipo utakapogundua kuwa siyo za kutoka mazingira ya Tanzania.

Anonymous said...

tumesikitishwa sana kuona vyanzo vyetu vya habari havina uhakika na habari zao. hiyo website iliyotolewa na gazeti la ijumaa inaonyesha moja kwa moja kuwa hao watu mmoja ni MGANDA na wote ni GAYS/ LESBIANS!
mbili ni kuwa hamkuhakikisha kama hizo picha ni za hao MNAOWAITA WAREMBO wa KIBONGO na MMEWASILIANA NAO. Mnauhakika gani kama ni picha za wabongo???? mpaka mkaamua kuandika gazetini?? ....au ndo mnafanya chochote kuuuza magazeti yenu?

Anonymous said...

website mliyotupatia inahakikisha kuwa muandishi wa RISASI hana uhakika na alichokisema, kwa vile website hiyo inaonyesha kuwa wale ni GAYS/LESBIANS na pia HAILAZIMISHI kuwa zile picha ni za hao walioziweka na wala hamkutupa ushahidi kuwa mlihakikisha hao mlowapigia simu ndio wenye picha zile.

Anonymous said...

na kwa vile hakuna uhuru wa kujielezea , na jua nilichokiandika hutokipublish

Anonymous said...

nyote hapo juu nahisi mnamiss point, chahali aliamua kuwakandia wenzake bila kujua kama zile picha kweli zipo na wahusika wamejitambulisha kama wabongo, hivyo ishu sio kama ni wabongo au sio wabongo, ila ishu iliyopo hapa ni kwamba kwa nini Chahali amewakandia jamaa wa risasi na kudai wanaandika habari feki? kwa nini, wakati vitiu hivyo vipo? kama jamaa angefanya utafiti kidogo, angekuwa na ishu tofauti ya kuwabana.. hapa nawaunga mkono jamaa wa risasi..

Anonymous said...

Mimi naungana na Chalali kuwa magazeti hayo mara nyingi wanaandika habari za uongo ili watu wanunu e magazeti, utakuta mtu anaandika eti kapigiwa simu na mtu wanaandika habari kwenye gazeti je hii ni sawa??? unatunia uongo kupata pesa za watu???? I think tuungane watanzania tuanzishe kampeni za kutonunu magazeti ya udaku!!! Hongera chalali, najua unaweza usitoe hii lakini msg will be sent

Anonymous said...

kwanza hii habari mbona imepindishwapindishwa jamani, kichwa cha habari cha muhusu Mengi, Ndani ya habari main content gazeti la Risasi.Mambo tofauti tofauti.

Simtetei Chalali...ila swala la kutofanya vizuri darasani linawahusu nini hasa, au linahusika vipi na habari yenyewe?...Huo ni mpindisho tosha na ni kupakana matope. Hatuelewi huyu jamaa anasoma katika mazingira gani, isitoshe level anayosoma Phd. haijadiliwi tena kama anafanya vizuri au vibaya darasani. Watanzania tuangalie cha kuandika.
Last point, magazeti ya udaku yapo hata Ulaya, ila cha muhimu ni kuandika mambo ambayo kweli yapo, au yametokea, si kubahatisha ili kuuzisha gazeti.

Anonymous said...

kama hiyo website ya porn iliyowekwa , chahali alikuwa na haki ya kupinga maelezo ya RISASI kwa vile hao watu hawapo TZ bali wanafanya kazi ya porn Marekani.
tusingefurahi kudanganywa na magazeti kwa kutofuatilia vyanzo vyao vya habari kikamilifu.
kosa la RISASI ni kutokufuatilia kikamilifu hao waliotowa namba zao na wapi wanapatikana kama ni sawa na hao walioweka picha za uchi kwenye Hi5. ushahidi mkubwa unaonyesha kuwa walitumia picha za hao watu tu kujipa umaarufu na kinachoshangaza ni kuona RISASI haikusema kuwa haikutuambia kuwa kuna uwezekano kuwa zile picha si zao.

Anonymous said...

..Hapa wala tusidanganyane!!haya magazeti ya udaku nayo yamezidi!yaani kweli mnapokosolewa basi lazima muje na jipya!kwanza elimu ya jamaa inawahusu nini nyie!kwa level yake mtu mzima na akili zako unajadili na kuandika gazeti kuwa hafanyi vizuri darasani!hapa ndo tunagundua kuwa tuna waandishi wa habari vihiyo wengi!jiteteeni kwa point za msingi!kumbukukeni kuwa mtandao unasomwa na watu wengi duniani
Pili kama kweli chanzo chenu cha habari ni hicho tu basi nyie ndio mmechemsha kabisa na wala hamna uzoefu na haya mambo ya mtandao!wewe kuona tu kuwa hometown ni Tanzania basi unapeleka kwenye gazetu hivyo hivyo!kumbuka kuwa mtu ana uhuru wa kuweka picha yeyote katika mtandao wa Hi5 na hata usishangae kuona mtu kaweka picha yako wewe mwenyewe na hapo ndo macho yatakutoka!
Hapa ninachotaka kusema ni kuwa lazima waandishi wawe makini na kazi zao sio tu kutuletea habari za kutaka kuuza magazeti kwa habari feki na pale mnapokosolewa ni muhimu kukubali makosa sio kuja na habari mpya ya kumkomoa yule ambaye amewakosoa!

Anonymous said...

Niliweka link nyingine inayoonyesha picha za yule anyejiita Melanie ambaye mimi binafsi namjua kuwa anaishi Miami na huwa anatumia muda mwingi kule South Beach akijiuza mwili wake, lakini kwenye hiyo website mliyotoa inaonyesha anaishi Dar-es-Salaam, mbona hamkumweka?

Link yake ni hii
http://www.wannawatch.com/hosted/index.php? wsc/xnxxporn/tinysblackadventures63>



Ninadhanani Chahali yuko right kabisa

Anonymous said...

Ningekuwa ndio chahali basi muda huu ningekuwa viti virefu kujipongeza kwa sababu jamaa wamemletea bingo.Akiwa-sue anashinda bila ubishi coz mie mwanafunzi pia,na japo sisomi PhD naamini kuwa ni vigumu sana,if not impossible,kwa mtu baki kupata taarifa za progress ya student.Inaelekea jamaa badala ya kuthibitisha kuwa picha hizo ni za watanzania kweli kama walivyodai awali,wameamua kumharibia jina mtu alowakosoa.I just wish ningekuwa mimi kwani ningewafilisi mahakamani kwa defamation.

Anonymous said...

Kaka Mrisho,nadhani hutasita kuchapisha maoni yangu.

Inawezekana mmechemsha katika stori ya awali na utetezi wenu.Nimeona picha hii kwenye mtandao........http://www.bikinidream.net/gals/glam0049/15.jpg.Huyu binti nimeshamwona kwenye cover za dvds za porno za States na sio m-bongo.

Halafu nime-google jina la huyo jamaa chahali,nieona kweli anafanya PhD chuoni hapo.Ila kilichonifanya nihisi mmeamua tu kumpaka ni ukweli kwamba wanafunzi wa PhD hawawezi kuwa wanafanya kozi moja bali wanaweza kuwa katika department moja while kila mmoja anafanya utafiti wake binafsi,na si rahisi wanafunzi hao hata kama wako dept moja kufahamu kama mwenzao anasuasua au la.Chekini vizuri hicho chanzo chenu,jamaa anaweza kudai mmemkashifu.Otherwise nawapongeza kwa kutupa news za home.

Anonymous said...

Naona post zangu za nyuma zimepigwa panga sana, kwa hiyo nimeamua kuutoa mjadala nje na kuuweka hapa

Anonymous said...

bwana mrisho !
bwana mrisho na mhariri mwenzio, samahanini sana ila tunaona walengwa wa habari zenu za udaku ni wale wasiokuwa na uwezo wa kupekuwa mitandao kila siku.
maana kwa ushahidi huu ulotolewa na gazeti lenu na ule ulotolewa na kina chahali na kitunguu, hatuna budi kuona magazeti yenu ni ya waropokwaji na yanaficha ukweli kwa vile mnajua watanzania wengi hawataweza kufuatilia ukweli wao wenyewe.
sie WASAFIRI wa nchi za nje, moja kwa moja tupo upande wa CHAHALI kwa vile ushahidi wote upo pamoja nae, hasa ukizingatia mmoja kati ya wale mlowatoa kwenye picha HAKUSEMA kama anaishi DAR bali KAMPALA uganda baada ya kuishi marekani kwa muda mrefu. GAZETI lenu lililifumbia macho hili na halikutaka kuhakikisha kama picha zile ni za hao wenye kujiuza waliopo tz
ukitaka kuonana na MELANIE karibu MIAMI SOUTH BEACH

Anonymous said...

mmezoea kutuletea habari za uongo, kwa sasa tunaziangalia kwa jicho lingine habari zote zilizowahi kuchapishwa na kampuni ya Global publishers, na kwamba most of them ni za kutunga...na za uongo.Mzuka wa Amina Chifupa utawatembelea nyie hadi muombe radhi kwa tena kwa kupitia hayohayo magazeti yenu. Bwana Asifiwe sana.