Thursday, August 9, 2007

The Sexiest Girl yawa gumzo!


NA JOSEPH SHALUWA
Shindano la kumsaka msichana mwenye mvuto zaidi wa kimahaba linaloendeshwa na gazeti la Ijumaa (The Ijumaa Sexiest Girl), limekuwa gumzo miongoni mwa wasomaji wetu.

Hilo limedhirika baada ya wasomaji wengi kutupigia simu wakionyesha kimuhemuhe cha kufuatilia shindano hilo, hata hivyo wengi wameshindwa kutabiri mshindi kutokana na washiriki wote kuwa na mvuto wa kimahaba.

"Yaani washiriki wote ni bomba sijui ni nani ataibuka mshindi, yaani hapo sina la kusema, nitafuatilia mpaka mwisho hadi nijue ni nani ataibuka kidedea maana wote ni wakali," alisema Bahati Mlawa mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.

Naye Benedict Joseph wa Moshi mkoani Kilimanjaro, alidai kuwa mshindi wa mwaka jana Jacqueline Ntuyabaliwe 'K-Lyn alikuwa na vigezo vyote vya kuwa mshindi ila mpambano wa mwaka huu hautabiriki.

"K-Lyn yupo bomba sana kwakweli, ilikuwa rahisi sana mwaka jana kutabiri kuwa angekuwa mshindi lakini mwaka huu ni vigumu sana kutabiri mshindi,” alisema.

Katika kuonyesha kuwa wasomaji wetu wanafuatilia shindalo hilo kwa makini na kuonyesha upenzi kwa wale wanaodhani wana mvuto zaidi wa kimahaba, shabiki mmoja alisema kuwa atakuwa tayari
kupiga kura nyingi awezavyo kwa yule anayeamini anavutia zaidi.

“Ni kweli mpambano wa mwaka huu ni mkali sana, lakini pamoja na hayo kwenye mashindano lazima kuwe na mshindi!

“Yupo mrembo mmoja kati yao ambaye nahisi anaweza kuibuka kinara, siwezi kumtaja jina ni siri yangu, nitakuwa nikimpigia kura nyingi kadri niwezavyo," alisema.

Shindano la 'Ijumaa Sexiest Girl' lilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka jana, ambapo Miss Tanzania mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe aliibuka kidedea.

1 comment:

Anonymous said...

Huyu anajiita Melanie wa Dar-es-Salaam unaweza kupa picha zake zaidi hapa

http://www.wannawatch.com/hosted/index.php?wsc/xnxxporn/tinysblackadventures63


Ninaweza kukutafutia picha zaidi na video za Melanie pamoja na za yule mwingine sikumbuki alituia jina gani ila ninajua kuwa anaishi Miami.