Tuesday, April 20, 2010

Zijue faida za soya, watu wazima na watoto

Kutokana na maombi ya wasomaji wetu wapendwa, nimeamua kukuletea makala haya kuhusu soya na vyakula vinavyotengenezwa kutokana na zao hili maarufu nchini Tanzania, hususan kuangalia majibu na maswali ya ulaji na faida zake kwa watoto.

Nchini China, zao hili limekuwa sehemu ya mlo kamili wa wananchi wake kwa karne nyingi. Kama inavyojulikana, Soya ina faida nyingi za kiafya kutokana na kuwa na kiasi kingi cha protini na madini. Soya huweza kutumika ikiwa katika aina mbalimbali ya vyakula.

Soya ni zao lenye uwezo mkubwa sana wa kupambana na maradhi hatari mwilini, na inalifanya zao hili kuwa muhimu kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha mchanganyiko wa virutubisho vingi vya madini, vitamini, ‘flavoids’, ‘isoflavones’, ‘polyphenols’, ‘terpenes’, ‘saponins’, ‘phytosterols’ na ‘phytate’.

Faida zingine za Soya
Husaidia kuzuia mtu asipatwe na saratani zitokanazo na homoni za mwili, kama vile saratani ya matiti na tumbo. Vile vile Soya ina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa mifupa na matatizo ya wanawake baada ya kufikia ukomo wa hedhi (menopause).

Vyakula na vinywaji vyote vitokanavyo na soya vimethibitika kuwa na kiwango kidogo sana cha mafuta mabaya na kolestrol, hivyo kuwa chakula ama kinywaji chenye faida tupu kwa mtumiaji.

Kwa kawaida Soya hutumika kama zao la kuzalisha mafuta ya kupikia ambayo huwa ni mazuri sana kiafya. Soya imejipatia umaarufu kiasi hicho, baada ya kugundulika kuwa na madini, vitamini na virutubisho vingine vinavyopatikana kwenye samaki, nyama, mayai na maziwa. Kwa maana nyingine, mtu anayekula Soya ni sawa na yule aliyekula vyakula hivyo.

Virutubisho vya Soya aina ya protini na ‘isoflavones’ hushusha kiwango cha Kolestrol mbaya (LDL) mwilini, halikadhalika hupunguza ugandaji wa damu hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya mtu kupatwa na mshituko wa moyo au kiharusi. Vile vile Soya huboresha msukumo na mishipa ya damu mwilini.

Kumbuka kuwa, protini mwilini huongeza uwezo wa mwili kuhifadhi na kunyonya madini ya ‘calcium’ kwenye mifupa. Ni mlo safi kwa wagonjwa wa kisukari na wenye matatizo ya figo. Kamba lishe (fibre) iliyomo, hurekebisha kiwango cha sukari na uchujaji sumu wa figo.

Soya ni nzuri kwa watu wenye matatizo ya kuwa na macho mekundu, ukosefu wa choo na kusikia kiu kila wakati. Aidha, tahadhari inatolewa kwa watu wenye matatizo ya kuharisha, tumbo kuuma, minyoo na kusikia kiuungulia, wasitumie Soya kwa wakati huo.

UPIKAJI WA SOYA
Iwapo unapika Soya, inashauriwa kuloweka kwenye maji kwa muda saa 8 au kuilaza kwenye maji hadi asubuhi. Kisha opoa na suuza na maji safi kisha weka jikoni na maji ya kutosha, hurahisisha kuiva haraka na bila kupoteza virutubisho vyake. Iwapo unataka kukaanga, fuata utaratibu huo huo wa kuloweka kwanza kabla ya kuanika na kusaga unga.

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU SOYA KWA WATOTO
SWALI: Je, kinywaji cha Soya kinaweza kumpatia mtoto madini ya ‘Calcium’ sawa na maziwa ya ng’ombe?

JIBU: Ndiyo, Soya ina madini ya ‘Calcium’, Vitamin A & D sawa na maziwa ya ngo’mbe na inajenga mifupa pia, soya ina faida nyinginge nyingi zaidi ukilinganisha na maziwa.

SWALI: Protini inayopatikana kwenye soya ni sawa na ile inayopatikana kwenye nyama?

JIBU: Soya ina kiwango cha protini chenye ubora wa hali ya juu ukilinganisha na kile kinachopatikana kwenye nyama, kwa sababu Soya ina ‘Amino Acids’ zote muhimu zinazohitajika kwa ukuaji wa mtoto na pia haina mafuta mabaya yanayosababisha lehemu (cholesterol) mwilini kama ilivyo kwa nyama.

SWALI: Soya ni salama kwa watoto?

JIBU: Bila shaka ni salama, hadi sasa hakuna utafiti wowote ulioonesha Soya kuwa na madhara kwa watoto au watu wazima. Soya imekuwa ikitumika maelfu ya miaka katika Bara la Asia bila kuwa na historia yoyote ya madhara yatokanayo na Soya.

Mtoto anaweza asipende kula Soya kama ilivyo, hivyo ni vizuri kumzoesha kwa kumchanganyia na vyakula anavyopenda kula, kama maziwa, uji au kwenye mkate kwa kutenegeneza kama siagi, kwani unga wa Soya unaweza kutengenezwa vyakula mbalimbali.

13 comments:

Dr kanyat said...

Dawa za nguvu za kiume na kurefusha uume...anatibu UTI...PID...UGUMBA...KWA KUTUMIA DAWA ASILI mtafute dr kanyas kupitia 0764839091

Unknown said...

Je soya inapunguza nguvu za kiume?

Nenelwa MP said...

asante kwa somo zuri,wengi tulikua tunasafisha na kusaga tu, bila kuchemsha na kutoa ganda la nje

Unknown said...

Asante kwa somo

Unknown said...

Asante kwa somo kwani nipata kuelewa chakula ambacho ni mbadala wa nyama

Unknown said...

Nimejifunza kitu kusoma c kukaa darasani tu

Unknown said...

Jee hayo maharage ya soya yanafaa kwa kutumia mjamzito? Alafu yanarekebisha homenes?

Unknown said...

Maganda take yanatatizo ukila

Unknown said...

Asante kwa somo zuri

Unknown said...

naomba kujuw faida za nyama ya soya

Unknown said...

Thnx kwa Elimu

Anonymous said...

Je ukitaka kutengeneza soya ya chai unafanyeje?

Anonymous said...

Asante sana Kwa somo