Tuesday, March 23, 2010

Zijue faida za ajabu za karanga!


Wengi wetu huchukulia ulaji wa karanga kama chakula cha kujiburudisha na kisichokuwa na umuhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuziwa iwapo utajua faida zake kama nitakavyokujuza leo katika makala haya.

Wiki iliyopita, tuliona faida zinazopatikana kutokana na ulaji wa korosho ambapo tuliona ambavyo mtu anaweza kujiepusha na magonjwa hatari ya moyo na hata kuongezeka kwa uzito kwa kula korosho tu, halikadhalika karanga nazo zinafaida zaidi ya hizo.

MAGONJWA YA MOYO
Kama ilivyokuwa kwa korosho, karanga nazo ni chanzo kizuri cha mafuta mazuri aina ya ‘monounsaturated fats’ ambayo yanatiliwa mkazo kutumiwa kwa afya ya moyo. Kwa mujibu wa utafiti, watu wanaokula karanga mara kwa mara hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (cardiovascular heart disease) kwa asilimia 21.

Aidha, katika taarifa iliyochapishwa kwenye jarida moja la Uingereza la ‘Journal of Nutrition’ ambako kuna matokeo ya taarifa nne za utafiti, imeonesha pia watu wanaotumia karanga mara kwa mara, angalau mara nne kwa wiki, hujipa kinga nyingine dhidi ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) kwa zaidi ya asilimia 37.

Mbali ya kuwa na mafuta mazuri yanayotoa kinga kwenye moyo, karanga pia, hasa za kukaanga, zinaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vinavyotoa kinga ya mwili (antioxidants) kuliko hata kile kinachopatikana kwenye tunda la epo na karoti!

Ili kupata kinga hiyo dhidi ya aina hizo mbili za ugonjwa wa moyo, ambao unatesa watu wengi duniani na kugharimu pesa nyingi kwa matibabu, unashauriwa kula karanga pamoja na bidhaa zake kama vile ‘peanut butter’, angalau kijiko kimoja cha chakula, mara nne kwa wiki.

KINGA DHIDI YA KIHARUSI
Ugonjwa mwingine hatari unaosumbua watu wengi hivi sasa ni kiharusi au ‘stroke’, lakini unaweza kujikinga nao kwa kuwa na mazoea ya kula karanga tu. Utafiti umeonesha kuwa karanga ina kirutubisho aina ya ‘Resveratrol’ ambacho hupatikana pia kwenye zabibu na mvinyo mwekundu (red wine).

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa maabara na kuchapishwa kwenye jarida la Kilimo na Kemia ya Chakula (Journal of Agricultural Food Chemistry), umeonesha kuwa kirutubisho hicho huimarisha utembeaji wa damu kwenye mishipa inayokwenda kwenye ubongo kwa kiasi cha asilimia 30.

KINGA DHIDI YA KANSA YA TUMBO
Faida nyingine inayoweza kupatikana kwenye mwili kutokana na ulaji wa karanga, ni kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, unaonesha kuwa virutubisho vya ‘folic acid’, ‘phytosterols’, ‘phytic acid’ (inositol hexaphosphate) na resveratrol’ vinavyopatikana kwenye karanga, huweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo.

Zaidi utafiti huo umeonesha kuwa ulaji wa karanga, hata mara mbili tu kwa wiki, una uwezo wa kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya tumbo kwa asilimia 58 kwa wanawake na asilimia 27 kwa wanaume!

Kwa maelezo hayo kuhusu faida za karanga mwilini, bila shaka chakula hiki kinapaswa kupewa kipaumbele katika orodha ya vyakula tunavyokula kila siku na hakika Mungu ametupenda sana kwa kutupa kinga dhidi ya maradhi yote yanayotukabili kwa njia ya vyakula.

Tuonane tena wiki ijayo.

17 comments:

Anonymous said...

Asante sana kwa habari nzuri.
Napenda sana karanga lakini sasa ntazipangia ratiba nzuri ya kula.

Vipi hazitaharibu mpangilio wa ratiba yangu ya kupunguza uzito?
Nipo katika mkakati wa kupungua uzito kidogo najihisi siko sawa baada ya kufumuka baada ya operation.

disminder.

Mrisho's Photography said...

disminder, kula tu, mafuta yake hayana madhara ni ile aina ya onounsaturated fats’ kama ya korosho....

Anonymous said...

asante kwa maelezo kwa kweli nitaanza kula tena karanga nilishazikinai mwaka huu wa 3 sijala kabisa karanga, hapa nilipo niliziona zile ambazo zimekaangwa na maganda je nazo ni nzuri? wanaziita monkey nuts sijui kwanini wakazipa jina hilo

Mrisho's Photography said...

...nazo ni nzuri tu hazina shida

Anonymous said...

Dokta nashukuru sana kwa kutupa sifa za karanga na musimu wa karanga ndio tayari .Elimu ni bahari kweli faida ulizotoa ni kidogo na nyingi umezificha lakini naomba vilevile utupe upande wa pili unaotokana na madhara ya kukithiri au kutumia wingi.kweli mimi ni mtumiaji mzuri wa karanga lakini mke wangu ananiambia nipunguze sababu ni cholestrol nyingi kwenye karanga je ni kweli?

Anonymous said...

Dokta nashukuru sana kwa kutupa sifa za karanga na musimu wa karanga ndio tayari .Elimu ni bahari kweli faida ulizotoa ni kidogo na nyingi umezificha lakini naomba vilevile utupe upande wa pili unaotokana na madhara ya kukithiri au kutumia wingi.kweli mimi ni mtumiaji mzuri wa karanga lakini mke wangu ananiambia nipunguze sababu ni cholestrol nyingi kwenye karanga je ni kweli?

Anonymous said...

Dokta nashukuru sana kwa kutupa sifa za karanga na musimu wa karanga ndio tayari .Elimu ni bahari kweli faida ulizotoa ni kidogo na nyingi umezificha lakini naomba vilevile utupe upande wa pili unaotokana na madhara ya kukithiri au kutumia wingi.kweli mimi ni mtumiaji mzuri wa karanga lakini mke wangu ananiambia nipunguze sababu ni cholestrol nyingi kwenye karanga je ni kweli?

Anonymous said...

Ubarikiwe sana.


disminder.

Mrisho's Photography said...

jamani nashukuru sana kwa kunisoma na hakika mkizingatia mambo haya maisha yenu mtaona yakuwa tofauti sana...naomba niweka wazi mimi siyo dokta bali ni mwandishi tu na nimeyajua mambo haya baada ya kuyafuatilia kwa vitendo ....nilikuwa sijui mambo haya lakini aliyenifungua masikio ni MAMA TERRY wakati ule akiongea kupitia redio one..kama mtakumbuka...nilipofuatilia kwenye maandiko na tafiti mablimbali nikakuta alichokuwa akikisema siyo kigeni na wanasayansi wameshafanya tafiti zao zote kwa kila tatizo la kiafya na sababu zake kuhusiana na suala zima la lishe...nilpoanza kula, kunywa kwa kuchagua na kuzingatia mambo ya lishe...maisha yangu yamebadilika sana...na nikitu utakiona wewe mwenywe kwa vitendo na utakuwa shahidi wa nafsi yako mwenyewe...binafsi sikumbuki mara ya mwisho nimeugua malaria lini au lini nimelazwa hospitali zaidi ya miaka 10 iliyopita...nijambo la kumshukuru sana Mungu kwa kutupa kila kitu kwa afya zetu...tuvijue na kuvutumia basi jamani..!!!

Mrisho's Photography said...

...kuhusu suala la kuzidisha karanga...nadhani kitu chochote kikizidi kiwango huweza kuwa sumu...ingawa karanga hazina kolestrol...lakini pengine usile kupita kiasi kama unavyosema ananomous hapo juu...il kwa ujumla wake, mafuta yaliyomo kwenye karanga tunaambiwa hayana madhara kiafya wala hayaongezi uzito na badala yake yanapunguza..!

jual obat perangsang said...

greetings
obat perangsang | obat kuat | alat bantu sex

Jual Kondom said...

I came across the serach engine and find your website, you have great and nice blog, Thanks for sharing, God bless you

jual kondom

Obat Perangsang Wanita


Anonymous said...

nashuhudia ni kweli

Unknown said...

Ok

Unknown said...

Je kwa watu wa mazoezi ya kujaza misuli hizo karanga zinasaidia

Idris only one said...

Hata Mimi nauza Karanga nitawashawishi wateja Wangu ahsante kwa makala yako

Unknown said...

Hata mimi ni mlaji mzuri wa karanga km mwandishi alivyosema ana miaka 10 hajaugua malaria mimi nina miaka 18.Mara ya mwisho kunywa dawa za malaria chloroqueen ilikuwa mwaka 2002.Kwa kweli namshukuru Mungu.