Friday, March 26, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!


TID, Ali Kiba Diamond, kuwania ubingwa wa steji!
Wote wanawania tuzo ya msanii bora wa mwaka, mwenye uwezo we kumiliki stage (Stage & Live performance of the year) zilizoandaliwa na Kituo cha Redio cha Clouds FM kupitia program ya XXL inayosimamiwa na prezenta, Hamis Mandi a.k.a B 12, B-Dazan, zikiwa na jina la Teen Xtra Awards 2010.

Artists waliotajwa kuwa katika category hiyo ni Shaa, Chid Benz na Johmakini. Ili kumpigia kura mmoja ambaye unadhani anastahili kuibuka na ushindi, andika neno TN likifuatiwa na namba yake ya utambulisho, kisha tuma kwenda 15551.

Majina ya washiriki na namba zao kwenye mabano ni Diamond (11), Shaa (12), TID (13), Alikiba (14), Chid Benz (15) na Johmakini (16).

Mbali na kategori hiyo, pia watatafutwa mwanasoka bora wa mwaka, mkali wa kucheza kwenye video, msanii bora wa kike, msanii bora wa kiume, msanii bora anayechipukia, video ya wimbo ya mwaka, mtayarishaji bora wa video, mtayarishaji bora wa muziki, kundi bora la muziki la mwaka, blogi bora ya muziki, wimbo bora wa kushirikiana na nyingine kibao.

Ukitaka kuwapigia kura wasanii wengine zaidi endelea kufuatilia magazeti ya Global Publishers kila siku au tembelea mtandao wa www.nipe5.com.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Tunda:naoa soon
Staa the big name kunako Bongo Fleva kutoka pande za Tip Top Connection Manzese, Khaleed Ramadhan ‘Tundaman’ juzi amegoma kuweka plain jina la mtarajiwa wake aliyepanga kufunga naye pingu za maisha.

Katika one on one na Showbiz jijini Dar juzi, jamaa huyo aliyefunika mbaya kwenye ngoma ya ‘Nipe Ripoti’ amefikia solution hiyo kufuatia hofu ya kugonganisha chicks, ishu ambayo anahisi itafanya mpango mzima wa marriage kuyeyuka.

“Natarajia kuoa soon, lakini hata nikitishiwa bastola, simtaji jina lake kwani mambo yanaweza kuwa mengine. Kifupi mke wangu mtarajiwa anamalizia masomo yake katika Chuo cha Ushirika Moshi na baada ya hilo kila kitu kitakuwa mwake,” alisema Tundaman.
xxxxxxxxxxxxxx

Watoto wa koffi wawachanganya mashabiki
Mastaa watatu wa muziki wa dansi waliowahi kulitumikia kwa pamoja kundi mahiri la Quartier Latin Internationale linaloongozwa na Simba wa Afrika, Koffi Charles Antonie Olomide ‘Moppao Sarckozy’, Faustne Lipupa Nsimba ‘Fally Ipupa’, Soleil Wanga na Ferre Gola wameonesha kuwachanganya mashabiki wa game hiyo huko pande za DRC.

Ishu kutoka mtandaoni zinadondosha kwamba, hivi sasa katika Jiji la Kinshasa huko kwa Mzee Kabila, kumekuwa na mabishano makali kutoka kwa mashabiki wa mastaa hao ambao kila mmoja anadai ni mkali kuliko mwenzake.

Mmoja wa mashabiki maarufu wa muziki nchini humo, Lokua Chitela amekaririwa na mtandao wa Congo Planet akikiri kwamba “Kumekuwa na shida kubwa ya kuchagua uende kwa nani kupata burudani kutokana na ubora wa vijana hao wanaopiga Soukouss ya kizazi kipya hasa wakati ambao wote wanapokuwa Kinshasa,” alisema.

Hayo yakiendelea kwa mashabiki kujikuta ndani ya wakati mgumu wa kuchagua nani mkali, nyota hao wako kwenye mishemishe ya kawaida kwa shoo kadhaa za ndani na nje ya nchi hiyo huku wakisikilizia mauzo ya albamu zao zinazopigana vikumbo sokoni hivi sasa.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Staa waMakhirikhiri: Nilitaabika sana kabla sijatoka,
Kutoka pande za Botswana staa wa muziki wa asili, Moses Malapela a.k.a Shumba Ratshega, aliyewaongoza wakali kadhaa wa muziki huo kutoa albamu iliyopata mafanikio makubwa ya Makhirikhiri, ameibuka na kutoa siri kubwa ya kufanikiwa kwao katika game ya muziki huo.

Akipiga story na gazeti la Monitr la pande hizo hivi karibuni, Shumba alisema, kufanikiwa kwao haikuwa kazi rahisi kama ambavyo some people wamekuwa wakifikiri.

ShowBiz inadondosha kuwa, nguvu ya ziada pamoja na kujitolea ndiyo siri kubwa ya washikaji hao hasa lilipokuja suala la kuwashawishi raia kuukubali muziki huo ambao mwanzo ulionekana siyo ishu.

Jamaa aliendelea kuweka wazi kwamba, baadaye ilibidi waweke mikakati mikubwa ya kujitangaza kimataifa ikiwa ni pamoja na kuomba nguvu ya serikali yao ambayo iliwapokea na kuanzisha kampeni maalum za kuwatangaza kama alama ya taifa.

“Kuna kila aina ya ugumu na hila kwenye kutafuta mafanikio, mfano mzuri ukiwa kwangu kwani kuna wakati Radio Botswana iliwahi kuzuia kupigwa kwa muziki wangu kwa muda wa mwaka mzima, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa lilinirudisha nyuma kwani albam yangu ya ‘Kuka Ntsu ‘ iliyokuwa mtaani wakati huo, ilishindwa kufanya vizuri, lakini sikukata tamaa,” alisema Shumba.

Katika hatua nyingine mchizi alitoa wito kwa wanamuziki from Bara la Afrika hasa wa game ya asili kutokata tamaa pia kuepuka utumwa wa muziki kwa kujipanga na kupiga muziki wao badala ya kuiga kutoka kwa nchi za magharibi.

ShowBiz inaweka sawa kwamba, pengine haya yaliyosemwa na Shumba yanaweza kuwa muhimu kwa wakali wa muziki wa asili Bongo kama Wanne Star, Saida Karoli, Sisi Tambala, Inafrika Bend ambao licha ya kupiga kazi mara kadhaa nje ya nchi, lakini bado hawajafikia mafanikio kama ya hawa jaama.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Compiled by mc george/ijumaa newspaper

No comments: