Tuesday, August 19, 2008

KIZUNGUZUNGU NI DALILI MBAYA

You are what you eat!
Tofauti na watu wengi wanavyodhani, kizunguzungu huwa ni ishara ya tahadhari inayotolewa na mwili kuwa kuna kitu hakiko sawa, hivyo uchunguzi wa chanzo cha tatizo unapaswa kufanywa haraka.
Kwa mujibu wa utafiti wa kitabibu, kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha kizunguzungu, ikiwemo ukosefu wa usinginzi (insomnia), kuumwa kichwa, kuchomwa na jua kwa muda mrefu, upungufu wa sukari mwilini na upungufu wa damu au maji.

Kwa kawaida, tatizo la kizunguzungu unaweza kulidhibiti mwenyewe kwa kutumia tiba mbadala ya kutengeneza mwenyewe nyumbani na kama tatizo litakuwa sugu, basi unashauriwa kumuona daktari mapema zaidi kabla hali hajawa mbaya zaidi.

Kuna tiba nyingi za nyumbani unazoweza kutumia kujitibu kizunguzungu, ya kwanza ni maji iwapo kizunguzungu kitatokana na kupungukiwa na maji mwilini, hivyo hatua ya kwanza ni kunywa kiasi cha lita moja au nusu ya maji yaliyochanganywa na asali au limau, maji haya yatatibu upungufu wa maji mwilini na kurejesha virutubisho vilivyopotea kutokana na joto kali.

Kizunguzungu kilichosababishwa na ukosefu wa usinginzi, kinahitaji kushugulikiwa na mtaalamu wa masuala ya usingizi au kutibiwa hospitali, ni vizuri kuwasiliana na daktari mara moja kuhusu tatizo hilo.

Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la juu la damu (high blood pressure) huwa hawasumbuliwi na kizunguzungu kwa muda mrefu. Kwa watu wenye tatizo la presha, huwa na dalili zingine kama vile kusikia uchovu, kichefuchefu, kupoteza fahamu na dalili nyingine. Iwapo dalili hizi zitaenda pamoja na kizunguzungu, mgonjwa anashauriwa kuonana na daktari kwa ushauri zaidi.

Kwa wale wanaopatwa na kizunguzungu kutokana kuwa na wasiwasi, kizunguzungu huja pale wanapokuwa katika hali fulani ya mchanganyiko wa mawazo juu ya jambo fulani, wakiwa katika hali hiyo, dawa pekee ni kujipumzisha na kuacha kuwaza kwa muda. Wanaweza kujipumzisha kwa kufanya mazoezi ya kuvuta na kushusha pumzi.

Upungufu wa damu mwilini (Anaemia), nao husababisha kizunguzungu wakati mwingine, hali hii hutokana na mwili kukosa hewa ya oksijeni ya kutosha. Kula vidonge vyenye madini ya chuma na ulaji wa mboga za kijani, maziwa, siagi na jibini husaidia kuondoa tatizo la kizunguzungu.

Si kawaida mtu kusikia kizunguzungu kila mara, ukiwa katika hali hii ujue una tatizo ambalo unashauriwa kulifikisha kwa daktari kwa uchunguzi zaidi. Vile vile unashauriwa kufuatilia dalili nyingine unazoziona wakati unapopatwa na kizunguzungu.

Kwa ujumla, kusikia kizunguzungu mara moja moja baada ya muda mrefu, sio dalili mbaya, hasa kama kizunguzungu chako unakipata baada ya kufanya jambo fulani, kama vile kukaa sana juani au kwenye joto kali ambalo husababisha mwili kukaukiwa na maji, matokea yake huwa ni kusikia kizunguzungu.

Katika hali kama hii, siku zote kimbilia kunywa maji yaliyochanganywa kidogo na limau pamoja na asali ambayo hurejesha maji na virutubisho vilivyopotea mwilini kutokana na joto kali.
Mwisho, ni jambo zuri mtu kujenga tabia ya kuchunguza mwenendo wa mwili na kuchukua hatua za haraka za kudhibiti dalili zisizo za kawaida mwilini ili kujiepusha na maradhi hatari yanayoweza kuwa yanajijenga mwilini.

12 comments:

selaput dara buatan said...

good article and information

Unknown said...

Mimi nina tatizo lakizugugu mpaka nimerazwa mala 2 nawekewa maji napona kazi yangu ni fundi kuchomerea nakaa sana juwani.je inaweza ikawa sababu.nimepima uwigi wa dam iko vizuli naomba msada wenu

Unknown said...

Mimi nina tatizo lakizugugu mpaka nimerazwa mala 2 nawekewa maji napona kazi yangu ni fundi kuchomerea nakaa sana juwani.je inaweza ikawa sababu.nimepima uwigi wa dam iko vizuli naomba msada wenu

anabolic rx24 asli said...

nice blog

Unknown said...

Asante kwa ushauri mzuri

Unknown said...

Asante kwa ushauri mzuri

Unknown said...

Kizunguzungu ambacho damu imepungua je damu inaporudi ktk kiwango chake huondoka kizunguzungu mgonjwa mw/mme alipima amekutwa kiwango 12 na kitaalam asilimia 12 huskii kizunguzungu chakukufanya ushindwe kufanya kazi zako sasa nikiwangao gani kifike cha ili kizunguzungu kiondoke? Naomba majibu

Unknown said...

Mimi huwa sikuwa na tabia ya kusikia kizunguzungu ila hali hii imenianza ghafla tu na sijisikii vibaya ila ni kizungu zungu mara ya kwanza ilikuwa juzi na Leo ni mara ya pili sasa najishaur pengine nikapime Malaria.naomben ushaur wenu

David Modolo said...

Nimejitahidi kunywa maji lakini bado kizunguzungu kinaniandama sana

Unknown said...

Asante sana kwa ushauri.

Dkt Jerry maswaga said...

Yaani mm haya sielewi naona change kama ndo bab kubwa maana hata hapa Niko kitandani nahs kama nabembea

Anonymous said...

inabidi ukapime