Monday, March 22, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!


Master J Aeleza kwanini mastaa wa BSS wanachemka sokoni!
Ijumaa iliyopita, safu hii ilipata ngekewa ya kutembelewa na Prodyuza galacha in Bongo Music, Joachim Kimaryo ‘Master J’ na kufanya naye interview katika maeneo kadhaa muhimu.

Akiwa mjengoni kwetu, Jay ambaye ni mmoja wa Maprodyuza walioishep Bongo Fleva wakati inasimama na kukubalika pamoja na aina nyingine ya muziki, alizungumzia mambo yafuatayo. Mosi, alielezea BSS, pili ni kuhusu Bongo Fleva ilipotoka na inapokuja na tatu ni yanayohusu studio yake, lebo na wasanii anaowasimamia kwa jumla. Kuhusu BSS, Jay aliiambia Abby Cool & MC George over the weekend kuwa washindi wa taji hilo linaloheshimika kwa Watanzania hivi sasa, hawaoneshi cheche sokoni kwa sababu hawawezi kuandika. Anasema:

“Tatizo si BSS, Benchmark, Madam Rita wala majaji, tatizo ni wasanii wenyewe kwa sababu hawana uwezo wa kuandika na kuandaa nyimbo zao ili zikubalike. “Wasanii wanaposhiriki BSS, wanaimba nyimbo za watu, kwahiyo wanaonesha uwezo wao kwa kuimba tu, hivyo wanakubalika na wanapigiwa kura lakini kwenye kutunga hakuna.

“Hii ndiyo sababu Jumanne Idd (mshindi mwaka 2007), Misoji Nkwabi (2008) wameishia njiani, unaona hata Pascal Cassian (2009) bado hajasimama, angalau Peter Msechu (1st runner up 2009) anaokoa jahazi.

“Nilitoa ofa ya wasanii wote walioingia Top 5 kurekodi nyimbo kwenye studio yangu (MJ Production) ili kuonesha mwanga ili Watanzania waone kwamba kumbe inawezekana Staa wa BSS akawa mfanyabiashara mzuri wa muziki nchini.

“Hilo tumeliangalia kwa mapana na mikakati ya BSS mwaka huu ni pamoja na kutafuta watu watakaowaandikia nyimbo washindi na kuwachagulia ala, kwahiyo baada ya shindano wataingia studio na kufyatua mawe yenye akili.” Ni hilo tu, wiki ijayo Master J atazungumzia Bongo Fleva zamani, sasa na ijayo.
******************

Wagosi Waachiwa huru na serikali
Wakali wa maneno ndani ya Sanaa ya Muziki wa Kizazi Kipya, Fred Malick ‘Mkoloni’ na Dk. John wanaounda Crew ya ‘Wagosi wa Kaya’ wameibuka na kuipigia makofi hatua ya serikali kuruhusu kwenda kitaani kwa albamu yao mpya ya inayokwenda kwa jina la ‘Miaka Kumi ya Maumivu’ iliyokuwa imepigwa stop awali.

Akisongesha na safu hii, katikati ya wiki iliyopita, Mkoloni ambaye ni mmoja wa wasanii wa kundi hilo, alisema sababu ya kufungiwa mwanzoni ilikuwa ni kuwepo kwa baadhi ya nyimbo ndani ya albamu hiyo, zenye mashairi yanayohofiwa kuchochea vurugu wakati wa Uchaguzi Mkuu, baadaye Oktoba mwaka huu. “Tulilazimika kukubaliana na agizo la serikali na kubadili aina ya maneno tuliyokuwa tumeyatumia ili kupata baraka za kupeleka mzigo sokoni na hatimaye tumefanikiwa,” alisema Mkoloni.

Akaongeza: “Naamini hadi serikali imekuwa makini kuangalia albamu nzima, basi wanafahamu moto wetu.” Imeandikwa na Hemed Kisanda.


*****************************
Mtanga apata uchizi kwa saa 46!
Usije ukadhani hii ni kutoka kwenye moja ya scene ya muvi mpya, kama unadhani hivyo unakosea sana ni true story tunayokupa, ni kwamba yule komediani wa ukweli Bongo, Khamis Changale a.k.a Mtanga alipatwa na uchizi uliodumu kwa saa 46, Hemed Kisanda ana makabrasha yooote.

Full story iko hivi, mwanzoni mwa wiki hii mida ya saa mbili usiku, Mtanga akiwa amechili home kwake pande za Buguruni, Dar homa ya maralia ilimpanda ghafla na kujikuta akitoka nje na kupiga kelele huku akiokota makopo, lakini majirani waliokoa jahazi na kumuwahisha katika Hospitali ya Amana.

Mmoja wa majirani waliohusika katika zoezi zima la kumkimbiza Mtanga hospitalini alisema: “Jamaa alikuwa na homa kali sana, tulipomfikisha Amana alikutwa na malaria saba, lakini sasa tunashukuru anaendelea vyema.”

"Ni kweli kaka nilipatwa na uchizi ghafla baada ya malaria kupanda kichwani, lakini kwasasa nipo mwake, Mungu mkubwa,” ndivyo alivyosema Mtanga baada ya Abby Cool & MC George Over the Weekend kumuibukia home kwake na kupiga naye stori kuhusu msala huo.

****************************************

Kidumu Apagawa na Marlaw
Mwanamuziki kiraka raia wa Burundi, Amosozi V’urukundo ‘Kidumu’ usiku wa Ijumaa aliwadhihirishia Watanzania kwamba yeye na mwana Bongo Flava almasi, Lawrence Malima ‘Marlaw’ ni ‘mabesti’ ile mbaya.

Kidumu akiwajibika kwenye Klabu ya San Cirro, Sinza, Dar ambapo alikuwa na shoo ya ukweli usiku huo, baada ya kupiga mzigo wa nguvu jukwaani, alimkaribisha Marlaw na kumtambulisha kwamba ni rafiki yake. Mbali na kumtambulisha, pia Kidumu aliimba wimbo wa Marlaw “Pii pii” kabla ya kumuachia ‘dogo’ huyo kuendelea nao, hivyo kuwafanya mashabiki kupandwa na wazimu katika shoo hiyo ambayo ilifunga nyomi la nguvu na Mrundi huyo anayeishi Kenya, kutoa burudani halisi ya muziki.

********************
Afande Sele atoa somo kuhusu umoja wa wasanii!
Mfalme pekee wa mashairi ndani ya Bongo Flava, Seleman Msindi a.k.a Afande Sele amechana ujumbe maalum kwa artists wa field hiyo kuacha tabia ya kusepa vikao vya kujadili mwenendo wa game vinavyoendelea hivi sasa ambavyo kwa kiasi kikubwa vimekuwa vikijadili kuhusu umoja wa wasanii, Hemed Kisanda anashuka mstari kwa mstari Afande ambaye amejituliza Morogoro kama maskani yake aliiambia Abby Cool & MC George Over the Weekend last week jijini Dar, muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha kujadili muziki huo ambacho kilihudhuriwa na nyota kiduchu.

“Jamaa wanatakiwa wafahamu kwamba hivi vikao vina umuhimu, hakuna wa kutusaidia kudai haki zetu kama sisi wenyewe tutashindwa kuwa na umoja. Nawasihi sana washkaji wasisepe, waje tuweke mikakati,” alisema Afande ambaye anapenda kuitwa Baba Tunda.

Members wa chama hilo, ambao tayari wameshajisajili BASATA ikiwa ni pamoja na kulipa ada hukutana kila wakati kujadili mambo mbalimbali ya muziki huo, lakini wasanii upcoming wamekuwa wakitia timu kwa wingi, huku masupastaa wakikacha kiaina.

*******************
Mashonda: Akomaa na mmoja tu, aporwa!
Ebwana Dah! Wiki hii ipo hewani tena na kama kawa inakupa mbili tatu kutoka kwa mastaa wa mtoni, leo inadili na mwanamuziki wa R&B anayekwenda kwa jina la Mashonda Tifrere.

Tofauti na mastaa wengi wa mbele ambao wamekuwa wakiripotiwa na mtandao unaodili na uhusiano wa kimapenzi kujikunja na mapatna kibao, stori ni tofauti kabisa na kimwana huyu mwenye mvuto wa kutosha ambaye ametoka na msela mmoja tu! Jina linaloonekana katika mtandao huo ni la prodyuza na mwanamuziki, Swizz Beatz, ambaye baadaye alikuwa ni mumewe wa ndoa na kufanikiwa kupata mtoto mmmoja kabla msanii Alicia Keys hajaisambaratisha ndoa yao.

Mashonda na Swizz walianza kudondoka on bed pamoja tangu 1998 hadi 2008 ambapo penzi lao lilianza kusuasua baada ya Alicia kumpora Beatz na kumuweka ubavuni mwake hadi hii leo.

Lakini pamoja na Mashonda kubaki mpweke mpaka sasa hajawahi kuripotiwa kutoka na kidume mwingine yeyote other ways iwe kwa kuibana kwa siri sana. Historia ya Mashonda kwa kifupi kwenye mtandao haioneshi sehemu aliyozaliwa wala umri wake, hiyo inawezekana ikawa ni kwasababu zilizo nje ya uwezo wake.

*************
compiled by mc george/ijumaa wikienda