Tuesday, March 16, 2010

Zijue faida za kula korosho kwa afya yako


Ni zao dogo, lakini maarufu duniani. Kwa mtizamo wa kawaida, una weza kulidharau zao hili. Wengi wetu hatuli korosho na hata pale tunapokula, hula kama kitafunwa cha kuchangamsha mdomo tu, na wala siyo kitu muhimu sana kuliwa.

Utafiti uliofanywa kuhusu zao la korosho, umeonesha kuwa korosho ina faida nyingi sana kiafya, hasa katika magonjwa yenye uhusiano na magonjwa ya moyo, kama ambavyo tutaweza kuona katika makala ya leo, na bila shaka kuanzia leo utaanza kuziangalia korosho kwa jicho tofauti.

KINGA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO
Siyo tu kwamba korosho zina kiwango kidogo cha mafuta (fat), lakini pia zina aina ya mafuta (Monounsaturated Fats) ambayo hutoa kinga kwenye moyo, aina ambayo huweza pia kupatikana kwenye Olive Oil.

Aidha, ndani ya korosho, kuna kirutubisho aina ya Oleic Acid ambacho utafiti unaonesha kuwa kirutubisho hicho huimarisha afya njema ya moyo na huwafaa hata wagonjwa wa kisukari.

Kama kweli unajali sana afya ya moyo wako, basi pendelea kula korosho za kila aina. Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa kwenye jarida la masuala ya virutubisho nchini Uingereza (British Journal of Nutrition), umeonesha kuwa watu waliopendelea kula korosho na bidhaa zake, kama butter, idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa moyo vilipungua kati ya asilimia 11 na 19.

Utafiti huo umeenda mbali zaidi na kubainisha kuwa watu wanaotumia korosho angalau mara nne kwa wiki, walionesha kuondokewa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (coronary disease) kwa asilimia 37! Na iwapo mtu atakula sana korosho, hatari ya kupatwa na magonjwa huendelea kupungua zaidi.

Dondoo moja ya ulaji korosho na kujiepusha na magonjwa ya moyo yote mawili (coronary na cardiovascular), inasema kuwa chukua kiganja kimoja cha korosho tafuna au kijiko kimoja cha chakula kilicho jaa ‘nut butter’, kula hivyo mara nne kwa wiki.

MADINI YA COPPER, UIMARISHAJI MIFUPA, NISHATI
Licha ya kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, korosho pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya copper ambayo ni muhimu sana katika mwili wa binadamu. Halikadhalika, korosho ina madini yanayoimarisha mifupa na kinga ya mwili.

KOROSHO NA UZITO
Kuna imani potofu kuwa kwa kuwa korosho ina mafuta, ukipenda kuzila basi mlaji huenda akanenepa. Imani hiyo si ya kweli kwani utafiti unaonesha kuwa watu wanaopenda kula korosho, angalau mara mbili kwa wiki, hakuna uwezekano wa kuongezeka uzito na badala yake wanaweza kupungua.

Hivyo inashauriwa kupenda kula korosho au butter kwa afya zetu na wala hakuna haja ya kuhofia kuongezeka uzito, badala yaje mlaji ndiye atakaepungua uzito. Elewa kwamba korosho kwa ujumla, ni chanzo kizuri cha madini ya copper, magnesium na phosphorus.

10 comments:

Anonymous said...

Kaka mrisho salama? Natoka nje ya mada. Hivi site yetu ya global publishers mbona inaudhi sana? Yaani ukifungua kusoma habari zaidi.. halafu ukitaka kurudi nyuma ili uendelee na topic zingine basi kila kitu kinatoweka, inabidi uanze upya kufungua website. Kwa kweli inakera sana. Please mwambie webmaster ajaribu kurekebisha hilo tatizo manake ni la kitambo sasa. Kwa kweli inafikia wakati mtu hata unaogopa kuclick ili usome zaidi. Halafu tatizo jingine.. ukiclick mfano picha.. page inakuja iko empty. Ahh kiukweli inaudhi. tafadhali kama mnaweza mkarekebisha hilo itakuwa mmetusaidia sana.

Mrisho's Photography said...

salama kaka,
kwa kifupi hayo matatizo tumeyaona na uamuzi tuliofikia ni kubadilisha template yote, kwani ni ya zamani kidogo na kuna vitu vingi tunataka kubadilisha, hivyo fanya subira mambo mazuri zaidi yanakuja kaka!

Anonymous said...

Korosho kwa afya asante sana.


disminder.

Anonymous said...

its true hata mimi uwa kwanza nafungua habari moja ya zamani, then narudi ile niliyokuwa nasoma.
ni usumbufu.

Mwalimu Shafi said...

Kutoka leo nitakuwa nikila korosho kila asubuhi na jioni.Nilikuwa sijui manufaa haya kwa afya.

Mwalimu Shafi said...

Kutoka leo nitakuwa nikila korosho kila asubuhi na jioni.Nilikuwa sijui manufaa haya kwa afya.

Unknown said...

Asante kaka...makala nzuri sana

Unknown said...

Asante kaka makala nimeielewa, Mwenyezi Mungu akuzidishie maarifa zaid utuoneshe na wengine tufaidike wote

Unknown said...

Bravo

Leonard Masele said...

Iko poa