Monday, April 19, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

G5 Click.com yagombea heshima na Dj Choka, Fetty
XXL Teen extra Awards inazidi kuleta mzozo, categories ni nyingi na kila moja inavutia ila kuna moja ipo interesting kwa namna yake, hii ni Music Website of the Year ambayo imepewa herufi D.

Katika category hiyo, vichwa kadhaa vimesimamishwa, DJ Choka (D2), Bongo5 (D3), DJ Fetty (D4), Babkubwa (D5) na G5 Click (D1). Kwa kuichambua category hiyo, this day tunao G5. Huu ni mtandao unaoundwa na vijana wadogo wane ambao wote wanagonga shule pande za UG ndani ya Kampala International University na NCC Learn IT.

Madogo wanaounda G5 ni Mustapha Suleiman, Ombeni Phiri, Desy Ernest na Nelson Kisanga ambao kupitia ubunifu wao, wameweza kuitengeneza G5click.com ambayo itavuma anga za kimataifa kiasi cha wengine kuifananisha na Facebook.

Usipime! G5 Click limeleta mapinduzi kwa kasi yake ya kupasha habari za burudani kwa wakati kupitia mtandaoni. Ndude zinazoifanya site hiyo ivutie ni kama kuwepo kwa ngoma mpya na kali on time, mashabiki kuwasiliana na kuchati, kupata historia za wasanii, pia kujionea video na picha za matukio mbalimbali.

Akigonga matamshi kwa niaba ya wenzake, Mustapha alisema nasi wikiendi iliyopita kuwa wapo serious ndiyo maana wanagonga mambo makubwa na akaongeza: “Hivi sasa tunajipanga kwa ajili ya kutambulisha njia mpya ya kutangaza, kusambaza na kuuza kazi za wasanii ili waondokane na kilio plus lawama kwa mdosi.” Jinsi ya kupiga kura kwenye category hiyo, unaandika SMS yenye neno TN unaacha nafasi ikifuatiwa na namba yake ya utambulisho (code) halafu unatuma kwenda 15551. Unaikubali G5? Gonga SMS yenye maandishi, TN D1 halafu unaitupa kwenda namba 15551. Pia unaweza kutembelea Nipe5.com ili uweze kupiga kura kwa internet.
****************
Sean Kingstone Abemendwa kingono na Paula DeAnda
Guy ambaye ana deserve kukanyaga Walk of Fame, Sean Kingston yupo ndani ya kuta za wadaku wajanja, hapa anachunguliwa kuona nyendo zake za faragha zimepita wapi na aliangukia kwa nani, Ebwana Dah!

Kwa mujibu wa site ya kiwanja ambayo ime specialize katika kuchungulia nyenendo za kimapenzi za mastaa, Sean anatajwa kutoka kimapenzi na mwanadada mmoja tu, Paula DeAnda. Ndani ya site hiyo, things hazipo open kama Sean na Paula still wanakwenda pamoja horizontal ila inakosolewa kuwa dogo huyo wa Beautiful Girl kuvamia penzi la mdada huyo ni kama anabendwa.

Ishu ya umri inatajwa ya kwanza ingawa si kihivyo coz mwanadada huyo anamzidi mwaka mmoja tu ‘dogo-bonge’ lakini inakolezwa kuwa Paula anayajua mapenzi na amekwishatoka na jamaa wa kutosha tena ambao wapo aged.

Kutokana na hilo, ndiyo maana inasemwa hivyo kuwa Sean ni bwana mdogo sana na wanapokuwa horizontal ni kama anabemendwa. Jina lake kamili ni Kisean Anderson, alizaliwa February 3, 1990, Miami, Florida, US. Ana umri wa miaka 20, taifa lake ni Marekani.
********************


Kili Music Awards 2010: Offside Trick ni kilio cha samaki
Mastaa kutoka Zenji, Offside Trick wanaong’ara na Samaki ambapo wimbo huo umewapeleka moja kwa moja kwenye kinyang’anyiro cha Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania ambayo ni category iliyopewa herufi H.

Offside Trick wakiwa na namba yao ya ushiriki (code) 64, wanakamuana na mastaa wenye ‘aka’ nyingi kwenye game kama Machozi Band na Mrisho Mpoto. Machozi Band ambayo code yake ni 43 inaingia kundini kupitia wimbo wake Mtarimbo, wakati Mpoto mwenye namba 54 yeye anachukua nafasi kwa wimbo Nikipata Nauli.

Wasanii wengine wanaowania award hiyo ni Wahapahapa Band na wimbo wao Cheichei (76) na Omar Omar kupitia ngoma yake Kupata Majaaliwa (65). Kupiga kura, unatuma SMS ukianza na neno KILI unaacha nafasi halafu unaambatanisha na herufi ya kipengele (category) kisha namba ya msanii baada ya hapo unatuma kwenda namba 15723. Mfano, kuchagua Samaki wa Offside Trick kuwa Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania. Unaandika KILI H64 kisha unatuma SMS yako kwenda namba 15723.
****************

Mzee Yusuf wa longtime vs mpya
Legendary wa kizazi kipya cha Taarab, Mzee Yusuf ‘Mfalme’ atafanyiwa bonge la tathmini na wadau wa muziki huo ili kupata ukweli, kati ya zamani na sasa wapi alikuwa anagonga mawe ya maana? Event yenyewee ni April 25, 2010 kwenye Ukumbi wa Travertine, Migomigo, Dar.

Katika kufanikisha kitu kamili, tathmini hiyo itaambana na show kali ambayo imepewa jina la Acheni Mfalme Aitwe Mfalme! Mzigo kamili umeandaliwa na Said Mdoe, yule Mkurugenzi Mtendaji wa Screen Masters.

Katika event hiyo, Mfalme hatotakiwa kuchoka na yeye ameahidi hatochoka jukwaani ili kudhihirisha ufalme wake, halafu akiwa on the stage, ataporomosha mawe ya zamani na sasa, yaani tangu anaanza taarab mpaka alamba.

“Siku hiyo mfalme ataanzia mwaka 2003 alipowashika mashabiki na kibao chake cha Kipendacho Roho na kutiririka na nyimbo zake zote mpaka 2010, Omar Tego na Diamond watakuwepo kumpa sapoti ya nguvu,” alisema Mdoe.
**************

Rich One afufuka!
Brothermen aliyepewa mkono wa kushoto na Kundi la TMK Wanaume Halisi, Richard Shauri ‘Rich One’, amefufuka na sasa anataka kuthibitisha kwamba anaweza kusimama bila Juma Kassim Ali Kiroboto ‘Sir Nature’.

Baada ya kimya kirefu, Rich ameachia wimbo unaokwenda jina la Apple la Kijani ambao amegonga collabo na kachaa wa reggae dancehall, Abdul Sykes ‘Dully’. Ngoma hiyo, Rich ameifanyia audio kwenye Studio ya Fish Crub kwa Lamar na kwa sasa video ipo sawa. Hivi karibuni, Sir Nature alimuengua Rich One na wasanii wengine kibao ndani ya Wanaume Halisi na kubakiwa na Dollo, Baba Levo na G Sun.
********************
COMPILED BY MC GEORGE/WIKIENDA NEWSPAPER

No comments: