Friday, April 16, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!


Ze Dudu Azindua harakati za kuwadisi wanaoua muziki!
The Bongo Hip Hop Legend, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ amezindua harakati mpya ya kuitetea Hip Hop na Bongo Flava pamoja na wasanii wake kwa kutoa CD inayoelezea kinagaubaga unyonyaji unaoendelea aliyoipa jina la Nguruwe.

In that CD, Ze Dudu a.k.a Baba Willy anawachana presenters & DJ’s ambao wanatajwa kuishi kimjini kimjini kwa mgongo wa wasanii ambao wanawanyonya.

Mbali na kuwadisi presenters & DJ’s hao, pia Dudu ametoa shut out kwa waandishi na wadau wa burudani Bongo kama Saleh Ally wa Championi, Amour Hassan wa The Guardian, Fina Mango, Masoud Kipanya, MC George na Abby Cool wa safu hii na wengine wachache ambao wanaheshimu taaluma kwa kutokuendekeza rushwa.

Kwa sauti kavu, pia Dudu amewagonga nyundo baadhi ya wana Hip Hop wanaojiita wanaharakati kwamba sifa hiyo haiendani nao kwa sababu ni wanyonge na hawajui kutetea haki.

“Mimi kuna ma-DJ wamegoma kupiga nyimbo zangu tangu mwaka 2006, miaka minne bado nipo. Sijaenda kuomba msamaha na ninaishi, sisi ndiyo ma-legendary wa huu muziki, tumetoka nao mbali halafu watu wanakuja kula kiulaini.

“Mtu unaimba Hip Hop unajiita mwanaharakati, siku mbili nyimbo zako hazichezwi redioni unakwenda kuomba msamaha, unapiga magoti, siku mbili!” Ze Dudu anasikika akigonga sauti ndani ya CD hiyo.

Akichambua umafia wa baadhi ya watangazaji na ma-DJ Bongo, Ze Dudu anamwaga kuwa kuna watu wameweka mkakati kwamba bila shilingi 500,000 hawaruhusu kupiga nyimbo redioni kitu ambacho ni sawa na unyonyaji.

“Hizo laki tano tano msanii atatoa kwa redio ngapi? Kwa uwezo upi? Halafu unatengeneza albamu kwa milioni 4, unakwenda kwa mdosi unalipwa milioni 2, msanii atapata nini?” Anahoji Ze Dudu na kuongeza:

“Mtangazaji anakupigia simu anakuuliza upo wapi? Unamjibu upo baa, baada ya dakika chache anakuja na wapambe, demu wake, wanaagiza vinywaji vya bei mbaya eti ‘bili’ yote juu yako msanii. Watu tuna familia, mimi mwanangu Willy anasoma International School.”

Mengi zaidi kuhusu CD ya Dudu usikose kuchungulia safu hii namba moja ya burudani nchini na ile ya Abby Cool & MC George over the weekend ndani ya Ijumaa Wikienda
**************************************

Kidumu


Blue-3
Kili Music Awards 2010:
Kidumu, Blu3 wasaka heshima Tuzo za Kili 2009
Artist kiraka, aliye na uraia wa Burundi, Amasozi V’urukundo ‘Kidumu’ anasaka heshima muhimu kwenye Tuzo za Kili Tanzania Music Awards.

Kidumu, anawania heshima hiyo katika Kipengele Q ambacho ni cha Wimbo Bora wa Afrika Mashariki ambapo anatoleana macho na Blue3, Cindy na Goodlife a.k.a Radio & Weasel.

Katika category hiyo, Kidumu ameingiza nyimbo mbili ambazo ni Haturudi Nyuma ambao amefanya na Juliana Kanyomozi, pia Umenikosea aliougonga mwenyewe.

Nyimbo zote za category hiyo pamoja na namba zake za kuchagua (codes) ni Where you are (12) wa Blue3 ft Goodlife (Radio & Weasel), Haturudi Nyuma (38), Umenikosea (37), Na Wewe (18) wa Cindy na Bread & Butter (68) wa Good Life (Radio & Weasel).
Kupiga kura, unatuma SMS ukianza na neno KILI unaacha nafasi halafu unaambatanisha na herufi ya kipengele (category) kisha namba ya msanii baada ya hapo unatuma kwenda namba 15723.

Mfano, kuchagua Haturudi Nyuma wa Kidumu na Juliana, unaandika KILI Q38 kisha unatuma SMS yako kwenda namba 15723.

No comments: