Tuesday, April 13, 2010

Ndizi ni kinga ya magonjwa haya


Baada ya kusoma makala yangu ya leo na kuzingatia nilichokiandika, bila shaka utaanza kuingalia ndizi kwa mtizamo tofauti na uliokuwa nao hapo awali. Ndizi mbivu ni tunda maarufu sana duniani lakini ni watu wachache wanaojua uwezo, faida na maajabu yaliyomo kwenye tunda hili.

Ndizi ina aina tatu za kipikee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama Sucrose, Fructose na Glucose na vile vile ina kiasi kingi cha ufumwele (fibre) ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.

Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata nishati ya kufanyakazi ya muda wa dakika 90 kwa kula ndizi mbili tu. Bila shaka ndizi ni tunda muhimu sana kwa wanamichezo. na ni tunda lenye uwezo pia wa kuponya na kuzuia matatizo mengi ya kiafya:

MFAIDHAIKO WA AKILI (DEPRESSION):
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama Cha Afya ya Akili cha Taifa (MIND) cha nchini Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tatizo hilo hujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi ina kirutubisho kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.

MATATIZO WAKATI WA HEDHI (PMS)
Kama wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na unaweza kuponywa. Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi, hurekebisha kiwango cha sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.

UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA):
Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina ya chuma (iron), inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upunguvu wa damu kwa sababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.

SHINIKIZO LA DAMU:
Tunda hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango kikubwa cha madini ya potasiamu (potassium) na wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha chumvi (sodium) hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.

Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya Mamlaka ya Dawa na Chakula ya nchini Marekani, iwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.

NGUVU YA AKILI:
Hivi karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule ya Twickenham nchini Uingereza, walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu wakati wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na wakati wa chakula cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao. Utafiti unaonesha kuwa potasiamu iliyojazana kwenye ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi kuamsha uwezo wake wa kujisomea.

KASUMBA (HANGOVERS):
Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover) ni kunywa ‘Milkshake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa na asali, hurejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu ,wakati maziwa hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.

Mbali na matatizo yaliyoelezwa hapo juu, ndizi pia husaidia katika matatizo mengine mengi kama vile kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya tumbo, kuondoa asidi tumboni, kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo ya moyo, n.k

Hivyo ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni bora, ukiilinganisha na Epo (Apple), ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga mara mbili, vitamin A na chuma mara tano na vitamini na madini mengine mara mbili zaidi ya epo. Mwisho; USIWEKE NDIZI KWENYE JOKOFU!

Asanteni kwa kunisoma!


5 comments:

Anonymous said...

Ahsante sana kwa maada hii ya afya na ninakuombea kwa mwenyezi mungu akulinde na akupe afya njema ili uzidi kutuelimisha.
Lakini mimi nina swali.Kuna zile ndizi wanazoziita ndizi kisukari je zinavirutubisho sawa na hizi ndefu????????

Pls msaada

Anonymous said...

Asante sana. Kweli nimesikia wanywaji wengi wakisema ukila ndizi unakata kilevi na pia harufu inakatika, kaka maneno yako sahihi.


disminder.

Anonymous said...

Asante sana kwa makala haya mazuri ya ulaji wa ndizi, lakini mbona inasemekana kuwa ndizi ina mfanya mtumiaji anenepe sana?

Je kuna ukweli wowote juu ya usemi huu? Na je unatakiwa kufanya nini?

Asante sana

Anonymous said...

Hi i frequently visit your blog.Naomba kueleweshwa je mwenye kisukari na pia ana high blood pressure anaweza tuu kula?

Disminder orig baby said...

Inawezekana ikawa sahihi ndizi zinanenepesha kwani ni tunda lenye energy nyingi sana.
lakini kaka tupe zaidi hayo nimepata kwa watu katika mazungumzo ya faida za vitu tunavyokula.