Wednesday, November 17, 2010

ASALI: KIBOKO YA UNENE UNAOWAKERA WANAWAKE

Wiki iliyopita nilipokea simu na ‘sms’ nyingi ambazo zijawahi kupokea tangu nianze kuandika makala mbalimbali kuhusu ulaji sahihi. Wengi nilioongea nao, walikuwa na matatatizo ya unene na walitaka niwaelezee ni vyakula au dawa gani wanaweza kutumia ili wapungue. Maelezo yao yanasikitisha kwa sababu baadhi yao wamefikia hatua ya kukata tamaa na kukataliwa na wapenzi au waume zao.

Nafurahi kuwaeleza kuwa, hasa dada zangu, kuwa tatizo la unene wa kupita kiasi liko mikononi mwa mtu mwenyewe. Ukiamua kupungua unaweza bila wasiwasi wowote na vyakula vya kupunguza unene viko vingi na ni rahisi sana. Lakini pia ukisema huwezi kupungua kwa sababu huwezi kuacha mzoea ya kula ovyo, kweli hutapungua.

Habari njema kuhusu suala la kupunguza uzito ni kwamba, unaweza kupunguza uzito bila kujinyima sana kula, muhimu ni kujua ule nini na wakati gani na uache kula nini, siyo lazima uende ‘gym’ ndiyo upungue.

Katika mfululizo wa makala haya unaoanza leo, nitawaeleza siri ya asali katika suala zima la kupunguza unene. Unaweza kushangaa kivipi asali inaweza kupunguza uzito wa mtu wakati ina sukari ambayo huongeza uzito? Napenda kukutoa wasiwasi kuwa sukari iliyomo kwenye asali siyo sawa na sukari unayoijua wewe. Asali ina uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo mengi sana ya kiafya mwilini na ni moja kati ya maelefu ya vyakula vya maajabu tulivyoletewa na Mungu.

Lakini kabla sijaanza moja kwa moja kueleza kuhusu asali na uwezo wake wa kupunguza uzito wa mwili, ningependa kuelezea kwa kirefu kwanza kuhusu uzito wa mwili na kanuni za kupunguza au kuongeza uzito wa mwili.

Awali ya yote, ili upunguze au uongeze uzito, unahitaji kujua mwili wako unafanyaje kazi, vitu gani vinachangia kuongeza au kupunguza uzito. Upi ni uzito wako sahihi? Mwili wako hufanyakazi kiasi gani kwa siku? Mwili wako unahitaji chakula (calories) kiasi gani kwa siku kulingana na kazi unazozifanya? Pia utajijuaje kama ni mzito sana (overweight) au mwepesi sana (underweight)?

Hivyo ili kufikia malengo ya kupunguza au kuongeza uzito, utahitaji kuwa na taarifa kamili kuhusu mwili wako (Personal Profile) ambazo zitakuwezesha kufanya mabadiliko na kuyafuatilia ipasavyo wakati wa kuanza programu ya kupunguza au kuongeza uzito.

Napenda kukutahadharisha mapema kuwa suala la kupunguza uzito kiafya halina ‘shot kati’, unatakiwa kuwa mvumilivu, kwa sababu huwezi kuona matokeo kama utapuuzia ushauri wa kuacha mazoea ya ulaji mbaya. Kama vile ambavyo hukunenepa au kukonda kwa siku moja, ndivyo ambavyo hutaweza kupunguza au kuongeza uzito kwa siku moja, hivyo usivunjike moyo mapema unapoona hufikii lengo lako mara moja.

Halikadhalika, utatakiwa kufanya mabadiliko ya chakula unachokula na wakati mwingine kukiacha kile ulichokuwa ukikipenda sana, pia lazima ujishughulishe usiwe mtu wa kukaa na kulala tu. Kabla ya kuanza programu ya kupunguza uzito, jipime kwanza kujua una kilo ngapi na jiwekee malengo kupunguza kilo, ya kuanzia wiki moja hadi kumi.

Katika kipindi hicho cha wiki 10, wiki nyingine unaweza kupunguza kilo 2, wiki nyingine unaweza kupunguza kilo 1, lakini katika wiki nyingine unaweza usipunguze hata nusu kilo, ikitokea hivyo usitilie mashaka mpango wako, endelea tu.

Katika kupima uzito, kuna vitu viwili huzingatiwa ambavyo ni uzito na urefu wa mtu. Uzito wa binadamu umegawanywa katika makundi manne: Uzito mdogo (Underweight), uzito bora kiafya (healthy weight), uzito mkubwa (overweight) na uzito wa kupita kiasi (obesity).

Ili uweze kujijua uko kwenye kundi gani, unapaswa kuujua urefu na uzito wako kwa sasa (Body Mass Index (BMI). Mfano, watu wenye urefu wa kuanzia futi 5 hadi futi 6, uzito unaokubalika ni kati ya kilo 60 na 75. Ukizidi hapo utatakiwa kuupunguza. Pia katika urefu huo ni hatari zaidi kiafya kuwa na uzito zaidi ya kilo 110. Halikadhalika, mwenye urefu huo, kuwa na uzito chini ya kilo 55 ni hatari kiafya.

Kama nilivyosema hapo awali, somo la kupunguza au kuongeza unene linahitaji uelewa mzuri ili ufikie lengo lako ulilojiwekea. Tumeshalitambua vyema suala la uzito, wiki ijayo nitaanza kuwaeleza kanuni za kupunguza au kuongeza unene na pia tutaanza kujifunza jinsi ambavyo unaweza kupunguza unene kwa kutumia asali bila kuathiri afya yako – usikose.

14 comments:

Unknown said...

Mrisho nimependa blog yako na mada unazotujuza,thnx bro na tunasubiri muendelezo wa hii topic

Mdau Makini (Houston, TX, USA) said...

Mrisho, kuwa makini sana na ushauri wako. Mimi naishi hapa Marekani na hizi "natural remedies" nyingi zimeshathibitishwa kwamba hazina faida yo yote kisayansi i.e. HAZIFANYI KAZI.

Kwani wewe ni daktari au unaokoteza vitu kwenye Google na kuwadanganya watu? Angalia utakuja kusababisha watu wapate matatizo makubwa sana ya kiafya.

Njia muafaka ya kupunguza unene ni kufanya mazoezi na kuhakikisha kwamba unakula chakula chenye nishati kidogo kuliko mwili wako unavyohitaji. HAKUNA NJIA YA MKATO na hizi hadithi zako za eti asali, mara sijui nini tumeshazizoea hapa Marekani. Hiyo asali yako kama inafanya kazi basi ilete hapa Marekani tuwe mabilionea wa kutupwa kwani unene hapa ni ishu kubwa sana. Unanisikitisha sana unapofanya hivi na kudanganya watu.

Niko tayari kuhojiana nawe na kukutumia baadhi ya studies ambazo zime-refute mambo kibao ambayo nimeshayaona kwenye blogu yako ukiwadanganya watu. Hata hapa Marekani mambo haya yapo lakini watu wanajua kwamba ni ubabaishaji na utapeli tu.

Kama umekomaa, utai-publish hii comment. Ukiiminya napo ni sawa tu lakini naomba nafsi yako ikusute kwa kuhubiri mambo ambayo huna utaalamu nayo na ambayo yanaweza kuwa na hatari kwa afya za wasomaji wako ambao nao bila shaka ni mbumbumbu tu wasioelewa kitu.

Kupunguza uzito waambie wapunguze kula vinono na waanze kufanya mazoezi mara moja. Mengine ni kupotezeana muda tu.

Mdau Makini;

Houston, USA

Mrisho's Photography said...

'MDAU MAKINI'
Siyo kweli kabisa kuwa sayansi imethibitisha 'natural remedies' hazina faida yoyote. HUO NI UONGO!!! Nafikiri wewe sasa ndiyo unataka kupotosha watu...halafu unaposema 'huku Marekani' nashindwa kukuelewa una maana gani, kwani kila kitu kinajulikana mahali popote duniani, hata kikifanyika kwenye sayari nyingine, hivi sasa dunia ni kijiji, kama kuna utafiti mpya umetoka wa kupinga ‘natural remedies’ tungeujua.

Vitu ninavyoviandika mimi siyo vigeni, vipo siku nyingi na vimefanyiwa utafiti wa kisayansi na wanasayansi waliobobea na ni vitu vimekuwa vikitumika tangu enzi za mababu zetu. Mimi pia ni muumini mkubwa wa ‘natural remedies, hivyo vitu vingine siyo vya kuambiwa tu, bali naviona mwenywe kwenye mwili wangu.

Nikija kwenye suala la msingi kuhusu kupunguza unene, Tepic hii ndiyo nimeianza, sijui kama kuna mahali ambako nimehitimisha kwa kusema unene unaweza kupungua kwa kula asali tu peke yake. Bila shaka sijasema hilo, lakini asali ina uwezo huo ukienda pamoja na ulaji sahihi, vizuri ungesoma makala zangu hadi mwisho kisha ukatoa hoja kwa kuthibitisha kama nilichokisema siyo kweli.

Umeziponda ‘natural remedies’ zote kwa ujumla kuwa hazina faida yoyote kwa binadamu…huo ni uongo mtupu….nioneshe utafiti unaoweza kuthibitisha hilo, usitaje natural remedy zote, taja moja tu ya asali kwanza. Mimi naweza kukutajia maelefu ya utafiti zinazothibitisha faida za asali na maelfu ya testimonies za kuthibitisha hilo. Kwanza soma article hii: http://www.benefits-of-honey.com/, kisha soma hapa: http://www.benefits-of-honey.com/the-benefits-of-honey.html

Ukimaliza hapo, soma hapa tena: http://www.tga.gov.au/docs/pdf/cmec/honeysr.pdf

Articles zote hizo pamoja na tafiti za kisayansi, zimeizungumzia asali kwa ujumla, nioneshe mahali ambako wameiponda asali kuwa haina faida yoyote.

Sina haja ya kukwambia asali inaweza vipi kupunguza unene, bali fuatilia makala zangu hadi mwisho halafu ulete hoja za msingi pale ambako utaona nimepotosha watu.

Kauli yako hujaifanyia utafiti na inaonekana unaamini sana modern medicine kuliko kitu kikingine. Hiyo ni sawa, lakini pia hupaswi kupuuzia natural remedies’ kwa kufanya hivyo utajifanya unajua zaidi hata kuliko Mungu, ambaye alipomuumba Adam na Hawa hakumjengea hospitali, zaidi ya kumpa miti na matunda.

Kwa mtizamo huo ulionao ‘mdau makini’ maradhi sugu yataendelea kuongezeka kila situ hadi pale utakapoacha kula vyakula ‘artificial’ na kuanza kutambua umuhimu wa kula ‘natural foods’. Kama unavyodai, Marekani unene ni tatizo kubwa, litaendelea kuwa hivyo mpaka pale mtakapoacha kula ‘junky foods’ na kuanza kula ‘natural foods’!!!!

Namalizia kwa kusema badilisha kauli yako na uwaombe radhi wasomaji kwa kusema kuwa ‘natural remedies’ hazina faida yoyote wakati watu wengi wamebadili maisha yao kiafya, ikiwemo mimi.

Ni kweli kwamba mimi siyo daktari, lakini kujua mwili wangu unataka nini siyo lazima niwe daktari, napaswa kujua kwa kusoma na kufuta wataalamu wetu wanavyotuambia, ambao wameshafanya utafiti wa kisayansi na kuuweka hadharani. Tabu ya binadamu ni ubishi na kufuata mazoea. Nachokifanya mimi ni kuwapa ufunuo watu ambao hawana fursa ya kuona na kusoma ufunuo wa mambo haya ambayo yapo tayari na wengi wamesaidiwa sana.

‘Mdau makini’, naomba pale ambapo umeona nimepotosha watu, niletee uthibitisho wa maandiko ya kiutafiti, kwani hata mimi mpaka leo bado naendelea kujifunza. Lakini nakuhakikishia nimejifunza vitu vingi sana vya kiafya na niko tofauti sana hivi sasa kiafya. Nimepunguza safari za hospitali kutoka mara mbili kila mwaka, hadi zero kwa miaka zaidi ya 5! Sikumbuki hata malaria mara ya mwisho nimeumwa lini, japo si lali na neti.

Aftrerall, natural remedies ni chakula tu, hivyo kama kweli hakina faida yoyote si utajisikia ukisha kula? Waliosema You are what You eat, walimaliza kila situ kuuelezea umuhimu wa vyakula!.

Anonymous said...

Kaka yangu husisikie la washamba we endelea kutuelimisha sie tunaohitaji kuyajua mambo kama haya unayotuletea. hao wabeba mabox wako uko wanateseka uwo ni wivu wanabaki kulopoka lopoka tu kuludi nyumbani wanaona haya wataludi vipi mikono mitupu wamebaki ku ha ha ha tu
viva Mrisho vivaaaaaaaaaa

Mdau Makini (Houston TX) said...

@ Anony wa November 19, 2010 1:30 AM

Siyo kila aliyeko huku anabeba maboksi. Wengine tuna kazi nzuri na maisha mazuri sana. Mimi ni daktari wa binadamu hapa Houston na haya mambo anayowanganya Mrisho hapa mengi ni utapeli tu. Nitamjibu vizuri baadaye na nitampa marejeo mengi yaliyotapakaa katika journals mbalimbali za kiakademia.

Si vizuri kuokota mambo kwenye google na kuanza kudanganya watu. Hiyo asali ni hatari sana hasa kwa watu wenye diabetes. Ngoja awadanganye muibugie mfe sijui mtasemaje. Naomba tu Mrisho awe na moyo wa kiume na asizizime comments zangu!

Mdau Makini (Houston TX) said...

NEW

@ Anony wa November 19, 2010 1:30 AM

Siyo kila aliyeko huku anabeba maboksi. Wengine tuna kazi nzuri na maisha mazuri sana. Mimi ni daktari wa binadamu hapa Houston na haya mambo anayowadanganya Mrisho hapa mengi ni utapeli tu. Nitamjibu vizuri baadaye na nitampa marejeo mengi yaliyotapakaa katika journals mbalimbali za kiakademia.

Si vizuri kuokota mambo kwenye google na kuanza kudanganya watu. Hiyo asali ni hatari sana hasa kwa watu wenye diabetes. Ngoja awadanganye muibugie mfe sijui mtasemaje. Naomba tu Mrisho awe na moyo wa kiume na asizizime comments zangu!

Anonymous said...

Huyo jamaa wa Houston Texas ana pointi. Kwa vile hizi articles huzifanyii utafiti wewe Mrisho, ni wazi kwamba unazipata mahali fulani.

Ili kukata mzizi wa fitina basi ukiziweka hapa toa na link ambako watu wanaopenda kuzisoma wazisome huko na kuona kama kuna tafiti zo zote.

Tatizo la Wabongo ni kwamba tumezoea kudesa sana na hatuna tabia ya kutoa source. Unakuta mtu anaandika jinsi ya kutumia asali kupunguza unene utafikiri hayo ni mawazo yake. Sema ulikoyatoa ili watu wanaotaka maarifa ya kweli wakasome huko kwa ufanisi zaidi.

Vinginevyo nashawishika kukubaliana na huyo Mdau.

Nategemea kwamba comment yangu hii itatoka...

Mrisho's Photography said...

Tatizo la baadhi ya wasomi wetu wa sasa, (modern academicians) bado wagumu sana kukubali vitu vya kale....nawaomba msome mambo haya ninayoandika kwani kuna articles nyingi sana zisizo na idadi na wala siyo suala la kuokoteza kwenye Google...kuna reliable sources na journals nyingi kwa kila makala ninazoandika. Si shindwi kuandika source na link zake katika makala hizo, lakini kumbuka kwamba makala zangu siwaandikii wasomi wa kwenye mtandao peke yake au wale wenye access na internet, bali naandika kwa ajili ya wasomaji wa magazeti mpaka mpaka kijijini Tanzania nzima...wasomi acheni uvivu someni kuhus vyakula...just google anything you want, you don't have to do research, it's done for u! Mbali na intrenet, kuna thousands ya vitabu vimeandikwa kuhusu hizi topic, mko dunia ipi kuona hiki nachokiandika mimi ni kitu kipya na hakiwezi kuandikwa na mtu kama Mrisho ambaye siye daktari?!!! Hebu hapo ulipo, search kuhusu honey on weight loss halafu chambua re liable articles uone utapa ngapi na zinazungumziaje suala hili......Come on guys, wake up!!

Anonymous said...

Kama wewe kweli ni daktali kwanini unakubali kuwa mtumwa kwanini husikludi kuitumikia nnchi yako kinachokuweka uko nini? kama kweli unayojifagilia ni kweli ludi nyumbani na jenga taifa lako husikae uko na kulaumu hawa waliokuwa uku wankituelimisha sisi wengine. wasomi walioendelea huwa wanasoma na kuludi nymbani wanaobaki uko ni walaláhoi watupu

Anonymous said...

Kaka Mrisho nakupongeza sana kwa kazi nzuri unayofanya. Mimi ni mmoja wa watu waliofaidika kwa kupunguza mwili kwa asali, utaratibu niliojiwekea huwa nakunywa mag tatu za maji ya uvuguvugu aliyochanganywa na asali na mdalasini kwa siku. nimefanikiwa kupunguza kilo 10. Naomba usikatishwe tamaa na watu wachache wasiokubali kutumia vitu vya asili. nakutakia kila la kheri

Anonymous said...

Kweli kupunguza unene inataka moyo,ngoja nijitahidi kufanya hyo then baada ya mwezi I believe i'll start seeing changes

Unknown said...

duuu kweli mm mwenyewe asali nshatumia saaaaana solution ni mazoezi na kupunguza vinono na maji mengi

Unknown said...

@mdau- we siyo daktar wala nn mbn unatuibia chenj

Dr kanyat said...

Dr kanyas mtaalamu wa tiba asili toka tanga anazo dawa za nguvu za kiume nankurefusha na kunenepesha uume ..anazo dawa za kuondoa kitambi wiki moja tu...mtafute dr kupitia 0764839091