Thursday, December 2, 2010

SUNDAY IS MARRIED NOW!

Want to know who is the lucky girl? Just press this link: www.harusini.blogspot.com

Wednesday, December 1, 2010

SEND OFF PARTY YA FLORA VICKY ILIVYOKUWA

Floravicky's Send Off Party: fungua hapa: www.harusini.blogspot.com

URBAN PULSE YAIVAMIA BBC

Diamond akifafanua jambo wakati akihojiwa na na Mtangazaji wa BBC, Idd Safe kuhusu Urban Tour
Frank (kushoto) akijadiliana na Diamond kabla ya kwenda hewani
Daimaond na mtangazaji wa BBC katika picha ya pozi
URBAN PULSE iliapata fursa nyingine ya kutembelea ofisi za BBC mjini London kwa ajili ya kupromote Urban Tour na Vita Dhidi ya Malaria kwa kushirikiana na msanii Diamond na Crew ya URBAN PULSE CREATIVE MEDIA.

Mr Blu To Rock Cape Town


Capetonians are eagerly waiting for the arrival of Tanzania’s ‘bad boy’ of music due to perform in Cape Town on the 18th of December.

The ‘Tabasamu’ singer is set to arrive in the mother city a week before his show, to visit local attractions and his schedule will include an interview with CBF on CTV. The show will take place at Seasons Music Boutique, 18 Bree Street, on Saturday the 18th of September. There to support him will be talented artists Side Msouth, Moja Shaba, F Bizzo, Makey, Eddy – One, SS and Crosby.

Tickets will be on sale a week before the show for R50, and if you get yours at the door it will cost you R60, so best you get your tickets before hand. For those who want to mingle with the superstar and sip on expensive champagne in a comfortable environment then it is bet you grab yourself a V.I.P ticket for R100.

All in all this is one show you do not want to miss, so come the 18th you know where you should be.

For further details and ticket sales please contact Michael on 083 685 1720 or Jayson on 021 422 5791.

Urban Pulse Yaandaa party


Utawala wa URBAN PULSE CREATIVE MEDIA Unapenda kuwashukuru wale wote ambao walijitolea kufika, kushiriki na kutoa support ya namna moja au nyingine wakati wa URBAN TOUR ili kusaidia kuchangia fedha za kupambana na vita dhidi ya Malaria Tanzania. Tour hii ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kkwa kupata publicity duniani kote na kuhamasisha watu mbalimbali ili kutambua umuhimu na namna ya kufanya ili kutokomeza ugonjwa huu kama ambapo kila mtu ataamua kuchukua majukumu na kufanya sehemu yake.

Itakuwa ni vigumu kutoa shukrani kwa kila mtu ila URBAN PULSE ingependa kutoa shukrani za dhati kwanza kabisa kwa Mwenyezi MUNGU ambaye alisaidia kufanikisha tour hii, Ubalozi wa Tanzania hapa UK Pamoja na staff wake,ASET(ASHA BARAKA & BARAKA MSILWA) Bloggers Wote waliosadia kutangaza show yetu ukianzia na MICHUZI,JIACHIE,MISS JESTINA,DJ CHOKA,TZ UK, HAKI NGOWI,GLOBAL PUBLISHERS, ABDALLAH MRISHO,KULIKONI UGHAIBUNI,HUNGA,MASHUGULI,KANUMBA,VINCENT KIGOSI,JENGATZ,MASHUGHULI,TA READING,LADY JAYDEE,MJENGWA,MTAA KWA MTAA,BONGO WIKEND na wengine wote.
TV & RADIO STATION zikiwepo BBC, BEN TV, BET,MTVBASE,AILTV, PRESENTERS: SPORAH, AYOUB MZEE, FRED MTOI, FRED MACHA, SAFINA,IDD SAFE, CHRIS GOLDFINGER NA JJ.
MA DJZ; CHAMBI,ASH,ANDREW,10 TONNES,JCOM,MOJA PAMOJA NA CHRIS GOLD FINGER

Hiyo basi Imeandaa party ya kutoa shukrani na kusherekea anniversary ya kwanza ya URBAN PULSE kwa wote jumamosi hii kuanzia 10pm- 4am. DJZ on the deck DJ CHAMBI &ANDREW

4th November 2010
CLUB AMBASSADOR
20 LONDON ROAD
BARKING, 1G11 8AJ

WOTE MNAKARIBISHWA
ASANTENI
URBAN PULSE CREATIVE

Monday, November 29, 2010

AHADI KAKORE KAOA JAMANI!

Mwenzenu Ahadi Kakore ameoa na siyo bachela tena. Kakore amemuoa Bulligrace Jumamosi Nov 23 katika kanisa la Azania Front na sherehe kufanyika Water Front jijini Dar es salaam. Hongera Kakore na karibu kwenye club mpya ya wanandoa!

ANKAL MICHUZI AWAPA NONDO WASANII

Ankal Michuzi akiwaonyesha wadau wa Jukwaa la Sanaa jinsi ya kuweka video kwenye U-Tube.
Ally Waziri wa Bendi ya Kilimanjaro ‘Wananjenje’ akichangia mada kuhusu Mchango wa Blogs Katika Kukuza Sanaa nchini.

Mdau wa Sanaa akimuuliza Ankal Michuzi swali.
Ankal Michuzi (Muhiddin Issa Michuzi) ambaye ni mmoja wa waasisi wa mitandao ya habari ya jamii (blogs) hapa nchini amewashauri wadau wa sanaa hasa wasanii kuanza kuingia kwa kasi kwenye matumizi ya teknolojia hiyo kwani ni njia kubwa ya kujitangaza na kuuza kazi za sanaa kote duniani.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa leo Jumatatu,Michuzi ambaye blog yake ya www.issamichuzi.blogspot.com imepata umaarufu mkubwa kutokana na kutembelewa na watu wengi aliweka wazi kwamba,blogs zimekuwa zikitembelewa na watu mbalimbali duniani hivyo wasanii hawana budi kuzitumia ili kujitangaza, kusambaza kazi zao na hata kujitambulisha katika masoko ya kimataifa.

Alisema kwamba, blogs tofauti na aina nyingine za vyombo vya habari inatumiwa kuhifadhi picha nyingi na kazi mbalimbali, kupata taarifa kuhusu tasnia ya sanaa, kupokea mawazo ya wateja wa kazi za sanaa na hata kuwa na wasaa wa kuwasiliana na wasanii wengine na hivyo kupanuka kimawazo na kiujuzi.

Akizungumzia historia ya blogs,Michuzi alisema kwamba ni teknolojia mpya hapa nchini na kwamba,ilianza kwa kuandika habari za kawaida lakini leo hii ni tegemeo katika kupasha habari kwa uharaka zaidi, kuwafikia watu wengi kuliko vyombo kadhaa vya habari na kimbilio la jamii kwani imekuwa kama sehemu ya jamii katika masuala mbalimbali.

Kwa ujumla Michuzi aliwataka wasanii na wadau wa Sanaa kuamka na kuanza kutumia teknolojia hiyo kwani wasanii mbalimbali duniani si tu wamekuwa wakitumia blog katika kujitangaza na kutambulisha kazi zao bali pia wamekuwa wakimilki mitandao na technolojia mbalimbali za mawasiliano.

Katika kuonesha kwamba, teknolojia hiyo ni muhimu Michuzi ameahidi kuwapa mafunzo ya bure wadau wa Jukwaa la Sanaa juu ya kufungua na kumiliki blog ambayo yataendeshwa Ijumaa ya Desemba 10,2010 kwenye Ukumbi wa BASATA.Wadau wote wa Sanaa mnakaribishwa.

Sunday, November 28, 2010