Monday, October 15, 2007

Nature ala shavu Big Brother


Baada ya kuibuka na tunzo ya Channel O, kupitia video yake ya Mugambo kwenye sherehe zilizofanyika Johannesburg, Afrika Kusini wiki iliyopita, msanii Juma Kassim Kiroboto Nature amekula shavu la kupiga shoo katika fainali kubwa za shindano la Big Brother Afrika linaloendelea nchini humo.

Akiongea na Abby Cool & MC George Over The Weekend muda mchachae baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K Nyerere, huku akiwa na tunzo hiyo mkononi, Nature alisema kwamba mbali kufanikiwa kuibuka na ushindi huo pia amepata dili ya kwenda kupiga shoo siku ya fainali ya shindano la Big Brother itakayofanyika siku chache zijazo.

'Natarajia kwenda tena Afrika Kusini Novemba 4 kwa ajili ya shoo moja ya Big Brother, nawashukuru sana Watanzania na wote walionipigia kura mpaka kufanikiwa kuleta heshima nyumbani' alisema msanii huyo ambaye katika tuzo hiyo aliwamwaga wasanii kibao kutoka Afrika Mashariki.

No comments: