Friday, October 12, 2007

NDOA YA HOYCE THEMU YAZUA JAMBO!

Hoyce na 'my husband wake'

Ndoa ya Miss Tanzania 1998-1999, Hoyce Temu na Lawrence Sikutwa ambaye ni raia wa Zambia iliyofungwa kinyemela Bomani Kinondoni jijini Dar es Salaam hivi karibuni, imekumbwa na utapeli mkubwa na mambo mazito ya kuudhi, gazeti la Ijumaa limegundua.

Kwa mujibu wa habari kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni rafiki wa karibu na Hoyce ambaye ameomba hifadhi ya jina lake, ndoa hiyo ilifungwa Agosti 17, mwaka huu.

Habari zaidi zinasema kuwa muda mfupi baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo watu wasiojulikana (matapeli), wamechapisha kadi za mwaliko wa sherehe ya harusi ya mrembo huyo na kukusanya michango kutoka kwa watu mbalimbali maarufu jijini.

"Wakati sherehe ya ndoa ya Hoyce Temu na Sikutwa ikiwa bado kufanyika kumeibuka matapeli ambao wamechapisha kadi feki za mwaliko na kuzipitisha kwenye ofisi mbalimbali kukusanya fedha," alisema rafiki huyo.

Aliongeza kuwa, kitendo hicho kimemuudhi sana rafiki yake na kutoa tahadhari kwa watu kuwa macho na matapeli hao. "Kitendo cha kufichuka kwa mambo hayo mazito katika ndoa hiyo kimemuudhi Hoyce pamoja na familia yake," alisema mtoa habari huyo.

Mtoa habari huyo alisema rafiki yake huyo haitaji mchango kutoka kwa mtu yeyote na anatarajia kuwaalika watu wachache katika sherehe yake atakayoifanya nje ya jiji la Dar es Salaam.

Akiongea na mwandishi wetu mwanzoni mwa wiki hii kuhusu mipango yake ya sherehe kuingiliwa na matapeli, Hoyce alikiri kuwepo na kusema kitendo hicho kimemkera sana.

"Niliweza kubaini kuwepo kwa kadi hizo za michango baada ya kuletewa moja na rafiki yangu aliyepewa ili achangie sherehe hiyo ambaye aliitilia mashaka," alisema Hoyce.

Aliongeza kuwa hajachapisha kadi za michango na wala hatochangisha pia amewatahadharisha watu kuwa macho na matapeli hao wenye nia ya kuharibu sherehe yake aliyoipanga kuifanya hivi karibuni.

Akizungumzia kuhusu kuolewa, Hoyce alisema kuwa tayari amefunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na raia wa Zambia bila kuhitaji watu wengi.

Mrembo huyo aliongeza kuwa alifunga ndoa kabla ya send off kutokana na msiba wa mtoto wa mume wake na yeye kufiwa na mtoto wa kaka yake ambapo iliwalazimu kusafiri.

Hoyce Temu ni mrembo aliyewahi kupata mafanikio makubwa katika tasnia ya urembo baada ya kuingia kwenye kundi la warembo bora ishirini walioshiriki kinyang'anyiro cha kumtafuta mlimbwende wa Dunia mwaka 1990 na kuliletea sifa kubwa Taifa letu.


2 comments:

Anonymous said...

Nawaombea wapate mtoto wa kwanza wa kike, aolewee na mwanangu! All the best mates!!!

Anonymous said...

Mbon kiswahili chako kibovu? kuna ndo a inyofungwa kinyemela? kwani si halali?