Saturday, October 13, 2007

USTAADH ANAPOFUMANIWA NDANI YA MWEZI WA RAMADHANI!

Mkazi mmoja wa Karakata jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina la Ustaadhi Hemed Mlawa, ameanza sikukuu ya Idd vibaya baada ya kufumaniwa akiwa gesti na mke wa jirani yake.

Tukio hilo lilitokea Jumatano saa 3.30 usiku katika nyumba ya kulala wageni (gesti) iitwayo Maridadi Bar & Guest House, iliyopo Kiwalani jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa mtoa habari, Mlawa licha ya kuwa ni muumini ya dini ya kiislamu katika eneo analoishi na kupewa pia cheo cha kuwa ustaadhi ana mke na mtoto mmoja.


Habari zilisema kuwa Mlawa ambaye ni muuza mkaa wa Karakata alikuwa akimsubua kwa kumtongoza mke wa jirani yake huyo aliyefahamka kwa jina moja la Rashid, kila mwanamke huyo alipokwenda kununua mkaa.


Mtoa habari huyo alisema kuwa, baada ya kuona anasumbuliwa kila mara, mwanamke huyo aliamua kumfahamisha mumewe (Rashid), ambaye alikasirishwa na kitendo hicho.


Kutokana na hali hiyo, Rashid aliwafahamisha ndugu zake kuhusu tabia ya muuza mkaa huyo na ndipo walimshauri wamshikishe adabu, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia ya ‘kuzengea’ wake za watu.


Mnyetishaji wetu alisema, kilichowatibua zaidi ni kwamba, licha ya Mlawa kuwa muislamu anayefunga Ramadhani pia ana mke na mtoto, aliendelea kumsumbua kumtaka kimapenzi mke wa mtu.


Habari zilisema, siku ya tukio Mlawa alimpigia simu mwanamke huyo na kumwambia kuwa afanye kila njia wakutane Buguruni baada ya futru.


“Mwanamke huyo alimfahamisha mumewe kuhusu ombi hilo, ambapo walishauriana kumwekea mtego na mipango ikaandaliwa,”

alisema mtoa habari wetu.


Mara baada ya kumaliza kufuturu, mwanamke huyo aliondoka kuelekea Buguruni, huku mumewe akitangulia eneo hilo la tukio kwa usafiri wake.


Habari zilisema kuwa muda mfupi baada ya mwanamke huyo kufika katika Kituo cha Mabasi cha Rozana Buguruni, Mlawa alimpigia simu na kumtaka amfuate Umoja Gest House, karibu na kituo cha mabasi cha Chama, anamsubiri.


Mwanamke huyo alipofika walichukuwa chumba namba 16B, na kuagiza soda, ambapo walianza kunywa huku wakipiga stori ndogondogo, bila kujua kuwa Rashid akiwa na vijana sita wakiwemo wapiga picha wetu walikuwa wakifuatilia zoezi hilo.


Wakati Rashid akiwa anasubiri mawasiliano ya mkewe ili wavamie chumbani humo, Mlawa alishtuka na kumtaka mke wa jamaa waondoke eneo hilo haraka, baada ya machale kumcheza.


“Walitoka nje ya gesti na kukodi taxi, Rashid pamoja na vijana wake wakiwemo wapigapicha wetu nao wakiwa na magari mawili na pikipiki moja, walianza safari ya kuwafuata,” alisema mtoa habari huyo.


Safari ya Mlawa na mwanamke huyo iliishia katika nyumba ya kulala wageni ya Malidadi Bar & Guest House, ambapo walichukuwa chumba namba 202.


Mtoa habari huyo aliongeza kuwa baada ya kuelekezwa chumba walichokuwemo, Rashid na wenzake walifika gesti hiyo ambapo mmoja alitinga mapokezi kama mteja, huku wengine wakipitiliza moja kwa moja hadi chumba husika na kugonga mlango.


Aidha baada ya kugonga, mlango ulifunguliwa ambapo Rashid na wapiga picha wake walitinga chumbani jambo lililomfanya Mlawa anyanyuke haraka kutoka kitandani na kukimbila bukta yake ili avae.


Hata hivyo, Rashid alimrukia na kuanza kumtandika makonde, hatua iliyokifanya chumba hicho kugeuka uwanja wa masumbwi kwani ustaadhi huyo naye alikuwa akirusha ngumi kama bingwa wa zamani wa ndondi duniani Michael Tyson.


Wapiga picha wakiwemo wa gazeti la Risasi walifanikiwa kumpiga picha kadhaa.


Meneja msaidizi wa gesti hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Alex alipofika chumbani humo, vurugu ilitulia na Mlawa alipohojiwa kwanini aliingia chumbani na mke wa mtu, alidai kuwa hakujua kama mwanamke huyo ameolewa.


Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na Rashid ambaye alidai kuwa Mlawa anafahamu kuwa mwanamke huyo ni mkewe na kwamba ni majirani.


Aidha meneja wa gesti hiyo aliita polisi wa kituo kidogo cha Kiwalani ambao walifika na kuwachukuwa Mlawa, Rashid na mwanamke huyo hadi kituoni kwa ajili ya kutoa maelezo.

Katika maelezo yake, Mlawa alikiri kufumaniwa na kuomba msamaha kwa maandishi

2 comments:

Anonymous said...

Huyo mama kama alikuwa amtaki huyo ustaadh angemuambia ukweli kuwa haiwezekani na kukaa kimya. Wale anaowakubali ambona hamwambii mumewe?

Anonymous said...

we anony hapo juu acha ushamba, siku zote unaripoti kitu kinachokukela sio unachokufurahia, uliona wapi mtu anaenda kwa daktari akiwa mzima?