Monday, December 10, 2007

WIKIENDA SHOWBIZ

Inspector apata shavu Sauzi.

Kutoka ndani ya kundi la TMK Halisi, msanii Haruna Kahena "Inspector Haroun" amepata dili ya kurekodi nchini Afrika Kusini kupitia studio za Da Face Production zilizopo Cape Town, kazi ambayo anatarajia kuifanya Desemba 15, mwaka huu, Shufaa Lyimo alipiga naye stori.

Akiongea kwa njia ya simu kutoka nchini humo "Babu" alisema kwamba amepata ofa hiyo baada ya kuonesha uwezo mkubwa katika shoo kadhaa alizofanya katika ziara yake inayoendelea nchini humo, kupitia studio hizo atafanya "track" kali ambazo atakuja kuzitambulsisha Bongo, siku chache baada ya kukanyaga kwenye Uwanja wa Ndege Mwalimu JK Nyerere, Dar es Salaam, Desemba 17, mwaka huu.

Akiizungumza ziara yake hiyo, msanii huyo alitamka kwamba ni mafanikio ya shule ya kutosha aliyoipata huko. "Jumamosi ya wiki iliyopita nilifanya shoo Cape Town, Desemba 6 niliondoka kuelekea Johannesburg ambapo nilipanda jukwaani Desemba 8, katika jiji la Pretoria. Kiukweli nimejifunza mambo mengi kutoka kwa wenzetu, pia nimeiwakilisha vyema Bongo Flava".

Aidha Inspector alisema kwamba atakaporudi Bongo atatoa zawadi ya Krismasi kwa mashabiki wake, ambayo ni shoo.


Jebby: Sasa nakwenda sawa na washikaji

Kwa mara ya kwanza, msanii kutoka ndani ya kundi la TMK Wanaume Family, Jenebi Mbaraka a.k.a Jebby anatarajia kuwaonesha masela wa Vingunguti jinsi alivyomudu kwenda sawa na wasanii wengine wa TMK Wanaume Family.

Ndani ya safu hii msanii huyo alisema kwamba atapiga ishu hiyo kunako shoo itakayokuwa ikiangushwa na kundi hilo, Ijumaa ya wiki hii ndani ya ukumbi wa Kongwa Bar, ukiwa ni muendelezo wa utambulisho wa albamu zao tatu, Kazi Ipo ya kundi zima, Katikati ya jiji ya Chegge na Bado mapema ya Stiko.

ÒWakati najiunga na kundi hilo nilikuwa bado sijasimama vizuri katika shoo, lakini sasa niko fiti, nakwenda sambamba na washika kama kawaida, siku hiyo watu wategemee kumuona Jebby mpya.

Naye muandaaji wa uzinduzi huo, George Alphonce alisema kwamba, kila kitu kuhusu shoo hiyo kiko safi, kinachosubiriwa ni siku ya tukio tu. "Washikaji wamepiga kambi Mkoani Tanga, wakijifua kwa ajili ya shughuli hiyo, wameahidi kufanya vitu tofauti na ilivyozoeleka hapo awali. Mashabiki wa Vingunguti watapata fulsa ya kujidai katika shoo hiyo kwa kiingilio cha shilingi elfu mbili mia tano tu".




Besta: Nasahau skendo zote, nakuja na DVD

Pamoja na kukumbwa na kashfa ya kupiga picha za utupu, msanii wa muziki wa Bongo Flava, kupitia kategori ya kizazi kipya, Besta Prosper ameiambia safu hii kwamba sasa anakuja upya, Mariam Mndeme alipiga naye stori.

Ndani ya Abby Cool & MC George Over The Weekend, Besta alitamka kwamba hivi sasa ameshasahau mambo hayo kwani ni vitu ambavyo havikuwa na ukweli wowote, hivyo haviwezi kumuumiza kichwa, zaidi vimempa ari ya kufanya kazi zaidi.

ÒHivi sasa napiga kazi, ninachotarajia kufanya hivi sasa ni kuachia DVD itakayokuwa na video za nyimbo zake tano, huku mmoja ukiwa umebeba jina la CD hiyo. Kila kitu kuhusu hilo kinakwenda vizuri, tayari nimesharekodi nyimbo tatu kati ya hizo tano, siku chache zijazo nitamalizia mbili zilizobaki. Video moja itakayotambulisha DVD hiyo itaanza kwenda hewani mapema mwezi huuÓ, alisema Besta.

No comments: