Bushoke: Sasa kiutu uzima zaidi
Mchizi aliyeanzia safari yake ya muziki Mkoani Dodoma, ndani ya kundi la Makole Exgon, Rutta Bushoke ambaye alipotea kwa muda na kurudi kunako game hivi karibuni, amekuja kiutu uzima zaidi tofauti na awali wakati anatoka.
Uchunguzi uliofanywa na ShowBiz umegungua mchizi hivi sasa anafanya game kiutu uzima zaidi, hata ujumbe wa nyimbo zake upo katika kuipigania jamii masikini zaidi kama anavyosikika kupitia kazi yake mpya, ‘Dunia ni njia’ tofauti na zamani alipokuwa akifanya ngoma za mapenzi kwa sana.
Mbali na kazi za kiutu uzima, hata muonekano wake hivi sasa ni tofauti na zamani ambapo siku za nyuma alikuwa anafuga nywele nyingi kisha kunyoa upara, lakini sasa amerudi na nywele za kawaida huku akiwa ameachia masharubu na ndevu kwa mbali.
Baada ya safu hii kujiuliza mwaswali mawili matatu kuhusu ujio wake, ikapata jibu kwamba inawezekana msela amejifunza vitu vingi sana kuhusu muziki alipokuwa amejichimbia Afrika Kusini ambako baba yake Mzee Maxmilian Busoke anafanyia kazi.
Besta Kuipa shavu Miss Shinyanga kesho
Msanii Besta Prosper ni miongoni mwa wasanii watakaojiachia ukumbini siku ya kinyang’anyiro cha kumtafuta mrembo wa Shinyanga (Miss Shinyanga) kitakachofanyika kesho Jumamosi, ndani ya Ukumbi wa NSSF uliyopo mkoani humo.
Akipiga stori na safu hii, Mratibu wa shughuli hiyo, Asela Magaka alisema kwamba mbali na Besta, mkali wa nyimbo za asili, Wanne Star naye atazingua kwa burudani ya kutosha huku warembo hao pia wakionesha uwezo wao wa kulimiliki jukwaa kupitia staili mbalimbali za kucheza muziki.
“Mshindi wa kwanza katika shindano hilo ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ataondoka na kitita cha shilingi 1,000,000, wa pili atajipatia shilingi 500,000, huku wa tatu akiondoka na shilingi 250,000,” alisema Asela.
Mratibu huyo amewataka wakazi wa Shinyanga na vitongoji vyake waende kumshuhudia mrembo mpya wa Mkoa huo ambaye atarithi taji la Helga Gabriel Miss Shinyanga 2007.

No comments:
Post a Comment